Habari zenu wanaMMU. Nina mpenzi wangu ambae nnategemea kuwa atakuwa baba watoto ila ana tatizo (mimi naliita tatizo). Ni kwamba yeye ni mfanyakazi wa kampuni moja binafsi,ni kawaida yake huwa anakuja kwangu mara nyingi nampikia chakula.
Anaweza akatoka kazini anapitia kwangu anakula then anaenda kwake.
Hakuna siku utamsikia anasema dia hela hii hapa kanunue mchele au hata yeye mwenyewe kwamba anapokuja abebe walau maji ya uhai, hana muda huo kabisa. Gharama zote nazijua mimi. Tena anaweza kudiriki hata kusema chakula nlichopika ye hakipendi.
Sasa nauliza eti huyu mtu majukumu anayajua? Hata tukiingia ndoani si atanitwisha majukumu yote huyu? Au labda nyie wenzangu mnaonaje tabia hii, ni ya kawaida?