Atayaweza majukumu huyu kweli?

Atayaweza majukumu huyu kweli?

Kwani we ukienda kwake hutakuwa unakula au utakuwa waenda na chakula chako?
 
Habari zenu wanaMMU. Nina mpenzi wangu ambae nnategemea kuwa atakuwa baba watoto ila ana tatizo (mimi naliita tatizo). Ni kwamba yeye ni mfanyakazi wa kampuni moja binafsi,ni kawaida yake huwa anakuja kwangu mara nyingi nampikia chakula.

Anaweza akatoka kazini anapitia kwangu anakula then anaenda kwake.

Hakuna siku utamsikia anasema dia hela hii hapa kanunue mchele au hata yeye mwenyewe kwamba anapokuja abebe walau maji ya uhai, hana muda huo kabisa. Gharama zote nazijua mimi. Tena anaweza kudiriki hata kusema chakula nlichopika ye hakipendi.

Sasa nauliza eti huyu mtu majukumu anayajua? Hata tukiingia ndoani si atanitwisha majukumu yote huyu? Au labda nyie wenzangu mnaonaje tabia hii, ni ya kawaida?

ulishamweleza mahitaji yako ? inawezekana anafikiri una hela za urithi ndiyo sababu hashituki, jaribu kumshitua kidogo utaona anatoa fedha zaidi ya unavyifuikiria
 
Wanaume bwana,,,,,, mtelezo sio mzuri mwambie atimize wajibu wake hawezi kimbia.

Na kama akikimbia baada ya kumweleza ukweli au akilipuka pamoja na wewe kumweleza kwa lugha rahisi, basi pia hakufai kwa sababu msingi wa uhusiano thabiti ni maelewano na uwezo mlionao katika kutatua matatizo yenu kwa mazungumzo.
Kama hauko huru kuzungumza nae au yeye hayuko huru kukusikiliza basi huo uhusiano bado ni mchanga hamfahamiani vizuri na mjipe muda wa kufahamiana au hamuendani, yani wote mnaishi kwa kuficha uhalisia wa maisha yenu au tabia zenu.
Uhusiano mzuri ni ule ambao mtu anakuwa huru kutoa mawazo yake na kusikilizwa na pia kufikia muafaka bila shari au hata ikitokea, inasuluhishwa bila kuhusisha mtu wa tatu labda kwa maswala kama kukosa uaminifu na yenye nature hiyo.
 
Ganda la ndizi full kuteleza...!zero cost..afu nyie wadada mbona mnakuwa conscious hadi kwny vitu vidogo
 
Habari zenu wanaMMU. Nina mpenzi wangu ambae nnategemea kuwa atakuwa baba watoto ila ana tatizo (mimi naliita tatizo). Ni kwamba yeye ni mfanyakazi wa kampuni moja binafsi,ni kawaida yake huwa anakuja kwangu mara nyingi nampikia chakula.

Anaweza akatoka kazini anapitia kwangu anakula then anaenda kwake.

Hakuna siku utamsikia anasema dia hela hii hapa kanunue mchele au hata yeye mwenyewe kwamba anapokuja abebe walau maji ya uhai, hana muda huo kabisa. Gharama zote nazijua mimi. Tena anaweza kudiriki hata kusema chakula nlichopika ye hakipendi.

Sasa nauliza eti huyu mtu majukumu anayajua? Hata tukiingia ndoani si atanitwisha majukumu yote huyu? Au labda nyie wenzangu mnaonaje tabia hii, ni ya kawaida?
Nina uhakika kuna makubalianao au mazoea ambayo mlianzishiana hapo mwanzoni ndiyo maana anajiamini kwa lolote, sidhani kama alikurupuka tu
 
kwa kweli tabia zake sio promising,lakini put that issue on table,hakuna mkamilifu hata mmoja huo ndio udhaifu wake kama utaubeba songambele,hata ukienda kwa mtu mwingine atakua na udhaifu mwingine hali kadhalika!love your man and let love take care of other things!
 
Heeeeee mbona anakula basi, si asubiri atoe mahari ndo aje kula?! Hajui vile vyakula vinanunuliwa?? Mmmh uso umeumbwa na haya! Kila siku unakula una nawa unaondoka..! Mwanaume?!!!! Mfyuuuuuuu!

Ni ajabu na kweli eti
 
Mmh hapa kunakitu kilichojificha mbona hali hii siyo ya kawaida.Jaribu kutafuta namna nzuri ya kumwambia ukweli wote uone atasemaje .Hapa ni kumwambia ukweli tu kwa busara zaidi .Ukiona anauchukia ukweli unaomwambia mkifunga ndoa sijui kama itadumu kweli.Mwambie ukweli lakini tumia busara sana.

Asante sana ila nikutoe wasiwasi hakuna kilichofichika labda yeye kama anacho
 
Hahaaa atakuwa Jaluo hilo...wabahiri sana halafu wana dharau. Sepa mapema, hawafai hao. Hata ukimkopa elfu 10 atakudai. Kaa nae mbali

Kama ulikuwepo ila dharau sijaona labda km anazo za chinichini
 
Mh.. Hapo naona kuna hatari. Kama mtu hata kuchangia chakula anachokula hakumbuki, atakumbuka kweli kukuletea hata kijizawadi? Wadada mnapenda vijichokuleti..vi ais krimu.. mara vi naitdress.. vipafyum.. Utapata kitu hapo? Atakutoa out kweli huyo? Na bado unamuambia kiaina lakini waaala.. haiimuingii akilini? hapo kuna shida. Ukizingatia hiki ndio kipindi ilibidi aku-impress? Mwe! Halafu watu wa hivyo bwana.. huwa ni ngumu sana kubadilika!

Kwa hiyo nisitegemee mabadiliko?
 
Ujue kuna wanaume wana nature ya kulelewa eeh huyo mmoja wapo!!! Em siku moja mwambie dia leo sijapika sina hata unga ndani.. !! Kama ajakwambia 'kakope' !!
 
Kwa nini unamuona kuwa yeye ndiye mwenye tatizo badala ya kujiona wewe ndiye mwenye tatizo?
1. Kwa nini umeshindwa kumwambia kuhusu hili? Siku zote unamwangalia anakuja, anakula anaondoka. Yeye ameshaona kuwa huo ndio utaratibu wa maisha kwa sababu hukuwahi kumwambia kuwa anavyofanya si vizuri.
2. Kama unaiona hii tabia yake kuwa ni mzigo na bado unaendelea kuwa naye, basi inabidi ujichunguze kuona kama u mzima

Inawezekana na mimi nina matatizo pia lkn yeye kama mtu mzima hawazi kuwaza hadi aambiwe?
 
kabla ya kuleta malalamiko yako hapa jukwaani umeishawahi kuongea nae kuhusu hii kitu au umekurupuka tu?kama unajitosheleza pengine mwenzio anaona hana haja ya kubebana na misosi.wakati mwingine inabidi ufikirie mambo kwa mapana yake,unaweza kushangaa akaja kuwa msaada mkubwa sana kwako katika mambo makubwa na ya muhimu kabisa kuliko hata huo msosi unaouligia kelele.unadhani asipokula kwako hana sehemu nyingine ya kula?au elf 3 ya ugali samaki inamkosa hadi adoee kwako?THINK BIG SISTER.LIFE IS MORE THAN JUST FOOD

Asante
 
Kuna topic fulan hapa iliwekwa na mwanaume akiomba ushauri juu ya mke wake ambaye hachangii chochote yaani hadi hela ya lunch kazini na vocha anaomba ilhali naye ni mwajiriwa, watu mlimponda sana eti analalamika vitu vidogo.

Jana kuna Topic ya jamaa aliyeibiwa Tsh 5000 Dodoma kwa mpenzi wake nayeye vivyo hivyo mlimponda. Hivi wanawake wamewapa nini nyinyi wanajukwaa?

Mwanamke akifanya lawama kwa mwanaume, mwanaume akifanya lawama kwa mwanaume...why? kuweni waungwana.

Wanaume aina ya huyu wa kwangu ni wachache mno ndio maana tunashangaa ukizingatia ninyi ndo vichwa vya nyumba
 
Back
Top Bottom