Atanitambua wallahi, hawezi kunichukulia mke wangu.! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atanitambua wallahi, hawezi kunichukulia mke wangu.!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 24, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hiyo siyo kauli yangu mimi Mtambuzi, bali ni kauli ambayo inawezekana hata wewe umewahi kuisikia au kuitoa pale unaposikia au kupata tetesi kuwa kuna mtu anatembea na mkeo au mpenzi wako. Mimi naamini kwamba, ni watu wenye utambuzi tu, ndio wanaoweza kupokea habari au tetesi za aina hiyo kwa namna tofauti. Kuhemkwa na kupagawa kamwe hakuwezi kumtokea mtu mwenye utambuzi, bali subira na busara zitatawala fikra zake katika kuutafuta ukweli wa taarifa hizo.

  Unapomsikia mtu anasema, 'napigana, sikubali kabisa mke wangu au mpenzi wangu achukuliwe na fulani.' Inawezekana mtu huyo akawa sahihi, lakini hebu tujiulize, ni kwa nini hakubali?Mtu kama huyu inawezekana anasema hakubali kwa sababu anaamini kwamba, huyo mwanamke ni mali yake. Lakini itakuwaje mali yake wakati kumbe inaweza kuhama na kwenda kwa mwingine kwa hiari yake! Mimi naamini kwamba mali yako ni kile tu unachoweza kukiamulia kiwe vipi na kwa nini. Binadamu hawezi kuwa mali yako. Utakuwa unajidanganya bure.

  Binadamu anao utashi na ampende nani ni suala analopanga yeye, siyo suala analopanga huyo anayedai kuwa ni mali yake. Unaposikia kwamba, mke au mpenzi wako anachukuliwa na fulani na ukathibitisha, kutokubali kwako kutakusaidia kitu gani? Ndio hukubali, lakini unadhani kutokubali kwako kutabadilisha ukweli huo wa mkeo au mpenzi wako kumegwa? Hakuna kitakachobadilika na ukweli utabaki kuwa hivyo!
  Au pale mkeo au mpenzi wako anaposema, ‘sikutaki tena, sina haja na wewe,' sasa wewe unawezaje kusema, ‘sikubali ni lazima niwe na wewe, na ukienda kwa mwingine utanitambua, wewe na huyo anayekupa kibri.' Ameshasema ‘sikutaki,' inawezekana vipi wewe udhani kwamba atabadili utashi wake?

  Inashangaza kidogo kuona mwanaume anagombana kwa sababu ya mwanamke. Huyu mwanamke unayegombewa ni binadamu na siyo gari wala nyumba ama mali yoyote, lakini unakuta mwanaume anabeba visasi na kuleta tafrani kwa sababu ya huyu kiumbe mwanamke. Unaweza kushangaa mtu anawekwa ngeu, kuuawa au kuburuzwa mahakamani kwa sababu ya ugomvi wa kugombea mwanamke. Bila kujali sababu ambazo zitatolewa, bado mimi nasema huo ni ujinga mkubwa kwa mtu kung'ang'ania kupendwa.
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi mbona suala hili lipo wazi japokuwa umejitahidi kuli complicate lakini linaeleweka wazi mapenzi yameumbwa kama kilivyo kifo hivyo moja ya character ya mapenzi ni wivu. Wivu unakuja baada ya mtu kukubali, au hata kama hujakukubali lakini unampenda basi hutapenda mtu huyo awe na mtu mwingine. Mbona hujiulizi hili, watu wana wake zaidi ya mmoja lakini akihisi mke wake mmoja anakwaruriwa nje inakuwa nongwa! Jaribu kujifunza maumbile ya mapenzi yakoje kiasili na ukondoa nadharia ya kiltu unachoweza kukiongombea ni kike ulichonacho.
   
 3. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Human nature - Michael Jackson.
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hayo mapenzi niliyoyazungumia ni yale mapenzi ya ukweli na si yale mkataba au unayopewa condition before mfano mimi nina mume/mpenzi hivyo kama unataka kubaliana na hali hii. Hilo linaweza kupunguza asili ya umbile la penzi.
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mzee wa Rula sija-compicate wala nini...... Nilichosema ni kwamba, hakuna binadamu anayeweza kummiliki binadamu mwingine, hilo jambo haliwezekani kamwe, sisi binadamu tunaweza kumiliki vitu kama nyumba, gari nk. mke au mume kumilikiwa, ni dhahiri hapo kutakuwa hakuna upendo. Upendo ni hiyari na siyo lazima, kama kutakuwa na kumilikiana yaani mmoja kujiona ana haki ya kummiliki mwingine, hapo kutakuwa na tatizo. badala ya kuwa watu wawili waliopendana, kunakuwa na mtu na mtumwa wake.
  Haya sasa unammlikli lakini anakwambia hakutaki. Je utafanya nini? ukilazimisha utaingia kwenye matatizo, sasa shida zote hizo ni za nini?

  Kama ukisoma mada yangu na kutafakari kwa mazaoea unaweza kuwa sahihi, kwa sababu sisi tumefundishwa tangu utotoni kuwa mwanamke anatakiwa kumilikiwa na mwanaume, na ndio maana anachumbiwa, analipiwa mahari na kisha kuolewa........ wote tumefundishwa hivyo. lakini kama utasoma mada hii na kuitafakari kwa jicho la tatu, utauona ukweli ninaouzungumzia..............
   
 6. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi,

  Tatizo umechanganya kuchukuliwa nje na Mapenzi. Kuchukuliwa nje kwa mke haina maana kwamba hana mapenzi na mme au mpenzi wake! Zimeshatajwa sababu nyingi sana; kweli kukosekana kwa mapenzi ni mojawapo; ila zipo sababu zingine nyingi tu! Mke anaweza kutoka nje katika juhudi za kusaka cheo, fedha, n.k. pamoja na kuwa bado ana mapenzi na mme wake!

  Wivu ni response inayosababishwa na woga wa kupoteza kile kilicho chako. Wivu kwenye mapenzi ni 'natural' na unatakiwa uwepo. Pasipo na wivu hakuna mapenzi ya ukweli, kuna mchezo wa kuigiza (Kumbuka ndoa maalfu ya Prince Charles na Diana ambapo ilifikia wakati Prince Charles anamlengeshea Diana kwa marafiki zake!! Matokeo yake wote twayajua - Mapenzi ni very delicate handle with care)

  Vile vile wanaume wanajua kuwa wanawake wakati mwingine hushawishiwa na hao wanaume wa nje au na marafiki zao hata kama bado wana mapenzi na waume zao bado anatoka nje.

  Sasa ukifikiria gharama za kuvunja ndoa (gharama za kihisia, gharama za mali, gharama za kijamii, n.k.) ni lazima kupambana kulinda ndoa. Na katika kupambana ni vizuri ukahakikisha kuwa pande zote zinazoshiriki katika WIZI huo zinajua kuwa zinajulikana. Mara nyingi njia hii husaidia!

  Hivi unafikiri response sahihi kwa suala kama hili ni kumweleza tu mke? Ni kweli kupambana ni tatizo, ila kumfanya mwanaume mwenzio ajue kuwa wizi wake unafahamika na anayeibiwa, ni mojawapo ya mbinu sahihi za kulinda mapenzi.

  Kumbuka kwenye ndoa kunakuwa na ma-bifu mengi sana; lakini kuwepo kwa ma-bifu haya hakuna maana kuwa mapenzi yameisha ingawa ma-bifu haya huweza kusababisha wapenzi kutoka nje!
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Duh.....kaazi kweli kweli
  Kipima pembe, hakuna mahali nimechanganya hapo bana.............
  Nimesema kama umesikia mke mpenzi kamegwa au amemegwa nje, na mtu huiyo kuhemkwa na kuleta tafrani kama ataua mtu au kudhuru mtu... wote tunajua matokeoya jambo hilo, wivu unaweza kuwepo sawa, lakini kwanini kuwe na wivu? wivu maana yake ni choyo tulicho nacho sisi wanadamu kutokana na kujifunga zaidi na wenzetu. mtu anafika mahali anapoteza urazini kwa sababu tu ya mihemko ya kile wanachoita kupenda. Mtu mwenye mapenzi ya kweli hawezi kuwa na mihemko, kwa sababu anatumia akili badala ya hisia.

  Haya kuna hili nalo, Mke au mpenzi anakwambia hakutaki, amekuchoka na hana mapenzi na wewe tena, lakini wewe unasema hukubali na unaleta tafrani........... ili iweje? kama hakupendi hakupendi tu, mtu halazimishwi kupenda bana..............................
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,544
  Trophy Points: 280
  nimepita hapa
   
 9. MASELE

  MASELE JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  biblia inasema kijana atawaacha wazazi wake na kuambatana na mkewe na wote hao watakuwa mwili mmoja that means mwanamke anamilikiwa na mme na mme pia anamilikiwa na mke ila nje ya maneno ya Mungu ni tamaa za kimwili na ugumu wa mioyo wa watu. agano la kale inaruhusiwa mme kumuacha mkewe ikiwa hajapendezwa/ kufurahishwa naye lakini agono jipya Yesu mwenyewe anasema mtu asimwache mme/mkewe ispokuwa kwa dhambi ya uzinzi na alicho kiunganisha MUNGU mwanadamu asikitenganishe, sasa mke kama anakuambia hakutaki hapo atakuwa anapingana na maandiko matakatifu, na heri mtu yule anayeachwa maana mbele za MUNGU hana hatia. hilo ni upende mmoja wa shilingi mke na mme (ndoa) upande mwingine wa shilingi mke/mme asiye rasimi (hawala n.k) mwanaume ukipigana kwa ajiri ya mchumba/ hawala hata mimi nitakushangaa maaana bahari bado ipo waweza kuvua samaki mwingine.
   
 10. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Una ndoa? Mtu akichukua mkeo utafanyaje?
   
 11. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #11
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  na akichukua mumeo utafanyaje?
   
 12. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Unauliza majibu!!!!!!
   
 13. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Unajua watu huwa wanaduhuru mahawara kwa kuwa mara nyingi ndio chanzo cha ndoa zao kuharibika, WEWE UNAYEJITIA FUNDI/HODARI WA KUFANYA KARUFUNDI KWA MKE/MUME WA MWENZIO.

  Matokeo yake, wewe jiandae kwa lolote, hata ukichomwa kisu saa 6 za mcha ni halali yako, umeyataka mwenyewe. Kibaya zaidi, polisi wakijua umeuawa kwa ajili ya mke/mume wa mtu, hawana habari na hiyo case, it is closed chapter kwa kuwa umeyataka mwenyewe, usiwaongezee kazi isiyo na tija.
   
 14. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja; yaani mtambuzi anataka kutuambia mke au mume kutembea hovyo ruksa kwa kuwa hakuna anaye mmiliki. Hizo ni theory kwenye real life tutaendelea kuwa na wivu hacha tuitwe wajinga.

   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi kisheria huwezi kumliki binadamu na hata katika mapenzi hakuna kitu cha kumiliki. Kinachoonekana kukuchanganya ni KUMILIKI & KUTAWALA. Huwezi kumliki mwanamke hata kama umemtolea mahali lakini unaweza kumtawala kimaamuzi, na utawala una mwisho akiamua kukataa kutawaliwa chini ya mwavuli wa pendo habari ndiyo imekwisha.
   
 16. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi,

  Kwenye mapenzi kwanza kabisa hakuna busara kwa sababu mapenzi ni hisia. Mtu anapompenda mtu mwingine si kwa sababu amejiambia akilini kuwa "ngoja nimpende huyu". Hii inakuja tu kwa sababu mapenzi yanatoka kwenye 'subconscious' na ni hisia zaidi kuliko akili.

  Mapenzi ya ukweli yanakuwa na wivu; bila wivu ni maigizo na matokeo ya maigizo wengi tunayajua. Mfano wa mapenzi ya maigizo maalfu ni kama ilivyokuwa kati ya Prince Charles na Princess Diana. Kuna wakati ilifikia kuwa Prince Charles alikuwa anamlengeshea Diana kwa rafiki zake ili wamchukue; yaani hapo hapakuwa na mapenzi bali maigizo.

  Mapenzi ya ukweli kama nilivyosema hapo juu ni hisia; hivyo mtu unaweza kumpenda mtu ambaye wala yeye hakupendi na unajua kama hakupendi; ila unashindwa kujitoa kwenye kumpenda. Ndo maana mwanamke anaweza kumwambia mwanaume kuwa hampendi ila yule mwanaume akaendelea kung'ang'ania tu.

  Kwa hiyo ndugu yangu, mapenzi si kitu cha kupangwa; ni hisia zinazotoka ndani. Mojawapo ya kitu ambacho mapenzi yanakuja nacho ni wivu!

  Kwa nini kuwe na wivu? Wataalam wengi wanakubaliana kuwa inaonekana wivu una faida katika mapenzi. Wale wanaofuatilia mambo ya zamani sana wanasema inaonekana huko zamani watu waliokuwa na wivu wa mapenzi walikuwa favoured na natural selection (evolution). Ndo maana tukarithi genes za wivu hadi leo karibu watu wote wenye mapenzi ya ukweli huonesha wivu vile vile.

  Hakuna sababu kubwa inayoonekana kuchangia kuwepo kwa wivu mbali na ukweli kuwa inaonekana tu wivu tumeurithi; ni response ambayo huwezi kuipangia ije saa ngapi. Unaweza kujidhibiti kwa kutumia akili, ila wivu upo pale pale!!
   
 17. Legend Hax

  Legend Hax Member

  #17
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Ki ukwel hawa viumbe ni complicated na wanafanana sana ndo maana hata kwenye bible wameandikwa sana hasa kwenye kitabu cha yoshua bin sira kwa wanao soma bible na nnahis hata kwenye Quaran pia, ki ukwel huwez ukamgombania mwanamke wakat ye ndo mwenye uamuzi,JE HUJAWAHI KUONA MWANAMKE MZURI ANACHUKULIWA NA MTU WA HARI YA CHINI? That's why unashauriwa kua "MPENDE SANA MWANAMKE WAKO LAKIN USIMWAMINI HATA KIDOGO"
   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  namuacha amchukue, si amekubali kwa hiyari yake kuchukuliwa............. nitakachofanya ni kuachana kw akufuata taratibu za kisheria ili kuepuka usumbufu hapo baadae, kwani najua hapo mapenzi yamekwisha, sasa kla nini nilazimishe kupendwa?
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Okada unajidanganya, ukiuwa kwa ugoni imekula kwako.....................
   
 20. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Lakini bado mie nasema wa kukutambua ni mkeo; kama kweli anakupenda kwa nini agawe kitumbua chako kwa wengine?
   
Loading...