Atanitambua wallahi, hawezi kunichukulia mke wangu.!

Naunga mkono hoja; yaani mtambuzi anataka kutuambia mke au mume kutembea hovyo ruksa kwa kuwa hakuna anaye mmiliki. Hizo ni theory kwenye real life tutaendelea kuwa na wivu hacha tuitwe wajinga.

na wajinga ndio waliwao nyumba kubwa upo hapo,hivyo endeeleeni kuitwa wajinga.
 
Hiyo siyo kauli yangu mimi Mtambuzi, bali ni kauli ambayo inawezekana hata wewe umewahi kuisikia au kuitoa pale unaposikia au kupata tetesi kuwa kuna mtu anatembea na mkeo au mpenzi wako. Mimi naamini kwamba, ni watu wenye utambuzi tu, ndio wanaoweza kupokea habari au tetesi za aina hiyo kwa namna tofauti. Kuhemkwa na kupagawa kamwe hakuwezi kumtokea mtu mwenye utambuzi, bali subira na busara zitatawala fikra zake katika kuutafuta ukweli wa taarifa hizo.

Unapomsikia mtu anasema, ‘napigana, sikubali kabisa mke wangu au mpenzi wangu achukuliwe na fulani.’ Inawezekana mtu huyo akawa sahihi, lakini hebu tujiulize, ni kwa nini hakubali?Mtu kama huyu inawezekana anasema hakubali kwa sababu anaamini kwamba, huyo mwanamke ni mali yake. Lakini itakuwaje mali yake wakati kumbe inaweza kuhama na kwenda kwa mwingine kwa hiari yake! Mimi naamini kwamba mali yako ni kile tu unachoweza kukiamulia kiwe vipi na kwa nini. Binadamu hawezi kuwa mali yako. Utakuwa unajidanganya bure.

Binadamu anao utashi na ampende nani ni suala analopanga yeye, siyo suala analopanga huyo anayedai kuwa ni mali yake. Unaposikia kwamba, mke au mpenzi wako anachukuliwa na fulani na ukathibitisha, kutokubali kwako kutakusaidia kitu gani? Ndio hukubali, lakini unadhani kutokubali kwako kutabadilisha ukweli huo wa mkeo au mpenzi wako kumegwa? Hakuna kitakachobadilika na ukweli utabaki kuwa hivyo!
Au pale mkeo au mpenzi wako anaposema, ‘sikutaki tena, sina haja na wewe,’ sasa wewe unawezaje kusema, ‘sikubali ni lazima niwe na wewe, na ukienda kwa mwingine utanitambua, wewe na huyo anayekupa kibri.’ Ameshasema ‘sikutaki,’ inawezekana vipi wewe udhani kwamba atabadili utashi wake?

Inashangaza kidogo kuona mwanaume anagombana kwa sababu ya mwanamke. Huyu mwanamke unayegombewa ni binadamu na siyo gari wala nyumba ama mali yoyote, lakini unakuta mwanaume anabeba visasi na kuleta tafrani kwa sababu ya huyu kiumbe mwanamke. Unaweza kushangaa mtu anawekwa ngeu, kuuawa au kuburuzwa mahakamani kwa sababu ya ugomvi wa kugombea mwanamke. Bila kujali sababu ambazo zitatolewa, bado mimi nasema huo ni ujinga mkubwa kwa mtu kung’ang’ania kupendwa.

hii heading ya thread yako nilifikiri umefumania mtu kumbe story.
 
Back
Top Bottom