Hapa duniani hakuna mtu anayeishi maisha magumu kama yule aliyefiwa na mama yake mzazi.
Ni bora ya mtu asiye na pesa, atahangaika atatafuta na ipo siku atazipata hata kama ni uzeeni atapata tu lakini ukimpoteza mama ndio imetoka hiyo. Mama hautaweza kumtafuta, mama hana mbadala, mama ni mmoja tu, ukimkosa huyo uliyenae hujikumpata mama mwingine.
Mtu asiye na mama anakuwa kwenye wakati mgumu sana hasa nyakati za:
1. GRADUATION 2. HARUSI 3. ANAPOPATA MAFANIKIO
Katika hayo matukio ndio ambapo kila mtu anakumbuka sana mama yake, utakapokuwa kwenye harusi unawish mama yako angekuwepo, utakapokuwa kwenye graduation unawish mama yako angekuona unapomaliza chuo.
Mtu anapomzungumzia mama yake basi nawewe unawish mama yako angekuwepo, mtu akipigiwa simu na mama yake unatamani mama yako angekuwepo labda angekupigia simu.
Mtu asiye na mama kila akikumbuka mama yake alipokuwa akimuita, akimfulia nguo, akimnyoshea nguo, akimuwekea chakula na kumfundisha mambo mengi ya kimaisha ataishia kulia tu.
Uchungu wa kumkosa mama hauna kifani wanajamiiforums, ukimkosa mama unaweza ukajiuliza unaishi ili iweje sasa?
POLENI WOTE MLIOFIWA NA MAMA ZENU PIA NISAMEHENI KWA KUWAKUMBUSHA MACHUNGU NA KUWATOA MACHOZI.
Dr.
MCHUNGUZI HURU (PhD)