At least amechelewa sanaaaa arudi saa ngapi

LOL. Michelle, atarudi alikotoka, na atarudi mazima! kwa nini usimfungulie ujue kilichomsibu?

mwaka mzima nitake kujua kinachomsibu kila siku?? sijui kwanini sitishiki na hilo la mwanaume kuondoka mazima.....mi poa tu!
 
sasa wewe na house girl..hamtoshi...
Bado na mimi nioshe vyombo ndo ufurahi???????
Kwani uwepo wako nyumbani ni wa hizo kazi hata majadiliano mazuri juu ya mipango ya maendeleo ya familia yanahitaji nafasi na muda mzuri wa kuyajadili hayo
 
Karaha za nini maisha yenyewe mafupi haya Michelle mpendwa wangu,hivi wanajua hata maana ya ndoa hawa jamani,kuna tofauti gani kati ya mwenye mume na asiye naye,nadhani siku nikijua hiyo tofauti ntatafuta mume wa kunioa kinyume chake kulia na kucheka yote ni makelele...

same here my dear....ningekupa majibu ya tofauti ya mwenye nae na asiye nae...ila nina uhakika tutaanza thread ndani ya thread....wenye roho zao wavumilie tu jamani....!!
 
"At most," sio "at least."


Si umemwelewa lakini mkuu?

Pili hiyo inaweza kuwa sahihi pia.....akisema 'at least' anamaanisha ivo ivo amechelewa sana arudi walau mida ya saa ngapi....? "at least saa tano usiku" inamaanisha amechelewa saana basi walau saa tano usiku awe ameshafika....
 
mwaka mzima nitake kujua kinachomsibu kila siku?? sijui kwanini sitishiki na hilo la mwanaume kuondoka mazima.....mi poa tu!

me like that Michelle....hoja sio kutisha au kutishika....hoja hapo ni plain truth kwamba kwa kufanya hivyo unacultivate mazingira ya kuondoka mazima....that said, hivi hapa tunaongelea ishu ya mwaka mzima eeh?:wink2: then that becomes a problem..
 
sasa wewe na house girl..hamtoshi...
Bado na mimi nioshe vyombo ndo ufurahi???????
hii kali kweli umeoa mkeo aje kuosha vyombo,ningekuwa muolewaji ningekuomba unioe maana ningekunyoosha,ningekupigia ngoma hiyo mwenyewe ungekata kiuno na ungeenda kuwa mume kwa maana ya mume sio muoshewa vyombo.
 
Si umemwelewa lakini mkuu?
Kama yeye ni mwelewa akisahihishwa atashukuru na kujifunza. Wewe unachemka halafu unasema "si umemwelewa."

Huwezi kusema "at least amechelewa." Tumia "at most."
 
mnaweza kujadili na kupanga muda utakao kuwa mwafaka kutokana na kazi ya mwanaume pia kama mwanaume anatumia vinywaji vyenye vilevi
 
tatizo huwa tunanganganiaga kubadili watu walio na meno 32 tayari huwa ni ngumu sana,sijui kwanini huwa hatupendi kuelewa na kujifunza hilo si kazi rahisi mpaka aamue mwenyewe na tena ukiweka mdom0 ndo huwa hawaachi tabia zao mbovu ni kama anapigilia misumari kwenye vidonda ule matapishi yako mwenyewe
 
ivi michelle sugu ikikomaa huwa inauma tena au inakuwa ngozi iliyokufa ni sawa sawa na moyo wa binadamu ukiumizwa sana inabakia moyo uliokufa kihisia na mapenzi kwisha unaishi kwa kujihami na roho isiyojali wala kuthamini hisia za mwingine


ha ha ha....nitakuwa nalia kimoyomoyo......mwanaume ninayempenda hawezi lala nje nikawa na amani ila lazima nijikaze kupinga tabia yake....
 
Akirudi kachelewa mi hufungua geti alafu namcheki machoni nijue kama ametoka kuchakachua au la. Aaah. Kuchelewa si issue, tunacho hofu ni kuwa ulikuwa na nani usiku mwingi?
 
Akirudi kachelewa mi hufungua geti alafu namcheki machoni nijue kama ametoka kuchakachua au la. Aaah. Kuchelewa si issue, tunacho hofu ni kuwa ulikuwa na nani usiku mwingi?

Wewe nawe asee ni GT bana.
Hebu watafutie hawa madogo session ya ushauri wa kijamii!
 
Back
Top Bottom