Mzee Mwanakijiji, Habari za leo, kwa wale wote Great 'Thinkers' and Singers bila kuwasahau sinkers!, Mimi naomba nichokoze fikra zako tu kidogo! Mimi binafsi suala kama hili kwa kuwa lipo mikononi mwa Polisi na Mahakama tuwaachie Professionals wafanye kazi yao yes! Professionals yaani Polisi, Usalama wa Taifa, Mahakama itakapowafikia, unless hauna kabisa imani na mfumo tulionao nchini, hapo unakuwa huna la kufanya bali kuchaguwa nchi nyingine ya kwenda kuisha wakati hii tuliyonayo inaboresha miundo yake. Kwani Wachina husema Aliyemuoa Mama ndiye Baba, hata kama humpendi ndiya baba yako huyo lazima umuheshimu hata akiwa tahira!
kwanza naomba kuweka angalizo dogo tu!
Ugomvi wa chatu na mamba waamulia wanini? ndiyo maana katika ujumbe wangu mwingine nimesema waachie professionals wafanye kazi zao.
Nadhani kwa kazi za Kipolisi kawaida everyone is a suspect unless proved otherwise! Waliohusika naamini kama hivyo vyombo tulivyonavyo vinafanya kazi vizuri vitawapata tu!
Sasa naomba tuingie kwenye scenario yako ya post yako hapo juu ya 'if or if or if and only if' naomba tukoke nje ya boksi na tuanze kulitazama hili suala ki-novel novel, Yes kwa 'if, if,,,, and only if'
- Tuchukulie kuwa kuna NGO (s), au Taasisi yeyote ambayo ni cover ya Serikali au kundi X, ambayo ina mawasiliano na Ubalozi wa nchi U,V,W. ambao wana Case officers and Field Officers na wamepenya na kufanya shughuli zao ndani ya Tanzania. Lengo lao ni kuchochea Vurugu na kuifanya Tanzania isiwe nchi ya amani kama ilivyo, iliwaweze kupata manufaa aidha ya kiuchumi au Kisiasa kwa kupita kundi lao ambalo wanalisaidia! Kumbuka kuwa hapa tupo kwenye 'ifs' huu wote ni utunzi tu siyo ukweli.
- Hizo nchi kwa kupitia NGOs, Case officers, and Stations Chiefs and Field Officers wao, wamefanikiwa kupenya kwenye Media, NGOs, na hata Vyama vya Siasa! Yes vyama vya Siasa $%^$^&&W%(**%^, ambao wanataka kuchochea vurugu ili washike dora kwa gharama yeyote!
- Je unatashangaa kuona NGO au NGOs kuhakikisha kuwa wanahamasisha vurugu ili waendelee kupata fedha kutuka kwa Case Officers wao? nadhani tuliwahi kushuhudia NGOs zinahamasihs maandamano katika baadhi ya nchi, kzishinikiza serikali zilizopo madarakani, kwa Tanzania sijuwi kama imwkwisha tokea, lakini sitashangaa kama hii scenario ya 'if and only if' ikawa inafanya kazi pia.
- Sasa Turudi kwenye issue ya Dr. Ulimboka, Je nini role ya NGOs na vikundi vya haki za binadamu, je ni kutetea maslahi na haki ya Watanzania kupata tiba, au kuchochea Madaktari wagome ikiwa pamoja na wao kuwa ndiyo wa Kwanza alfajiri kutambua kuwa Dr. Ulimboka wamemlimboka na yupo Mabwepande, kwa kweli namuonea huruma na Mungu amsaidie apone haraka, lakini pia nawaonea huruma Watanzania wengine wanaokufa kwa kukosa tiba.
- Hivyo kwa kutumia tathmini yako ya if,if,if and only if tuwaachie Professionals wafenye kazi zao, inawezekana hata waliokimbilia kujifanya wanamuokoa ndiyo wao walimlimboka ili wanendelee kupata misaada, tusije tukawabebesha watu dhambi zisizo zao! kama ambavyo mimi nimejaribu kufanya hapa kwa kujifanya Great Thinker, kumbe mimi ni singer tu.
- Tuwaache Polisi na wahusika wengine watuletee majibu. Umetaja masaa 72 tangu kesi, Je huko Marekani kesi ya JFK majibu yalikwisha toka?