Askofu Shoo, Wabunge Timotheo Mzava wa Korogwe na Dkt. Pallangyo wa Arumeru wanalichafua kanisa au wanachafuliwa?

Hili kanisa si ndo lile ambalo lilisema Makonda atafaa kumrithi Mwendazake au nmefananisha. Si ndo Hilo Hilo lilikaa kimya wakat Tundu Lissu anapigwa Risasi.
Aisee Dkt Shoo unamuonea bure na kanisa analoongoza, Shoo alipinga waziwazi ushenzi wa Mwendazake, Aliyesema Makonda anafaa ni yule Kadrinali Pengo
 
Kama Anna na Mzava waliishi kama mume na mke Kwa zaidi ya miaka miwili, hapo Kuna presumption of marriage.

Anna ana pingamizi halali, asikilizwe.
Inasemekana huyo ana alishakubali kuachana hadi kwa barua kabisa na saini juu lakini wapambe wake wakaja mshauri akaenda kuoindua meza tena
 
Sasa kama kanisa halina mamlaka ya kusikiliza hoja zake,

Kwanini Huwa wanaruhusu nafasi ya kupokea mapingamizi.

Hayo ndio mapingamizi yenyewe na lazima wayatolee uamuzi.

Wakimruhusu aende mahakamani hiyo ndoa itafungwa kweli
Labda huelewi kitu nilichoandika, pingamizi lenye mashiko ni kama kuna ndoa iliyofungwa kanisani au msikitini au serikalini yaani kama anayepinga ana cheti Cha ndoa halali Cha serikali au kimila ambayo imeshuhudiwa na kufanyika mbele ya kiongozi wa kimila Ila sio mnachukuana tu mnafanya umalaya halafu kanisa lisikilize pingamizi.

Ndoa nyingine ni utaratibu binafsi ambao hautambuliki kikanisa. Sasa kama umeishi kwenye utaratibu ambao hautambuliki kanisani huwezi kuleta malalamiko na kanisanlikusikilize lizuie ndoa .

Nia na madhumuni no kuzuia dhambi ya uzinzi kama mnataka kubariki tendo takatifu basi fuateni Baraka za kanisa otherwise itakuwa no mmeishi katika taratibu za kishetani.

Huwezi kuclaim haki wakati haujatenda haki. Walikuwa wapi miaka yote kurudi kundini kutubu na kubariki mahusiano yao ili yatambulike kikanisa?

Pingamizi kutambulika kama kuna subsisting valid marriage inayotambulika na kanisa otherwise sasa hata demu uliyemla mwaka juzi ataleta pingamizi, Jirani anayekutamani ataleta pingamizi, etc.
 
Mbunge wa Korogwe Vijijini Timotheo Mzava anatarajiwa kufunga ndoa na Binti wa Mbunge wa Arumeru Mashariki Dr. Jonh Pallangyo. Ndoa hii inalalamikiwa na mtu anayetambulika kwa jina la Anna na wachungaji huko Arusha na Tanga wanafahamu upo mgogoro. Mgogoro huu nimeusoma kwenye gazeti kwamba Mzava ameishi na mwanamke kinyumba kwa miaka mitatu na amezaa naye mtoto Kisha akamwacha na kuanza mahusiano na mtoto wa Mbunge mwenzie.

Mimi sina shida na mahusiano mapya ila kwa mujibu wa Taarifa zilizotolewa na Raia Mwema na nikiwa Kama muumini wa kikristo nimeona Kama kanisa halifanyi kazi yake Kama linavyopaswa kufanya. Kanisa linachafuka kwa kuandikwa vibaya kwenye magazeti lakini pia skendo ikihusisha watu wenye vyeo na fedha kwenye jamii.

Tunapoona haya yanaandikwa kwenye vyombo vya habari na kwa kuwa yanagusa imani zetu za dini pamoja na nyumba za ibada, tunalazimika kuwaomba viongozi wa dini watoke adharani kukana tuhuma hizi zilizoelekezwa kwao au kuzikubali na kuzirekebisha kwa kuzingatia maandiko na Katiba ya kanisa.

Utaratibu wa kanisa upo wazi, kabla ya kufunga ndoa lazima ndoa itangazwe siku 21 na likitokea pingamizi Basi lipatiwe ufumbuzi na TAASISI husika, je inakuwaje Kuna pingamizi na taratibu za kufunga ndoa next week kwa mujibu wa gazeti zinaendelea.

Endapo muumini atabainika kufanya uzinzi na ushahidi kuwepo (kwa mazingira haya ushahidi ni mtoto wa mzava na Anna) muumini lazima asimame mbele ya kanisa na kutubu Kisha kurejeshwa kundini ndipo taratibu za ndoa ziendelee, huyu Mzava hajawahi kufanya haya.

Panapowekwa pingamizi mweka pingamizi uitwa na suluhu upatikana, kwenye hili hakuna hiyo suluhu. Je, siku ya ndoa Anna akisimama akasema anapingamizi ndoa itafungwa? Kanisa halina walinzi, je siku hiyo familia hizi mbili zitakuja na walinzi kanisani kwa sababu Wana nafasi serikalini na Wana fedha? Kwanini Mkuu wa KKKT usubiri hadi Hali ichafuke kwenye hekalu wakati una nafasi yakusimama imara na kuzitetea nguzo za imani?

Nikuombe wewe na viongozi wa kanisa msiruhusu mambo haya kufanyika sirini, tokeni adharani msafishe kanisa kwenye tuhuma hizi za wanasiasa kutumia madara na pesa kupindisha utaratibu wa kanisa.

Tendeni haki, Kama Mzava na Pallangyo Wana haki tokeni adharani tuelezeni kwa haki yao ni ipi, na Kama huyo mwanamke Anna ana haki na mtoto wake kuweka pingamizi sikilizeni pingamizi ilo. Msipowatendea wenye fedha na madaraka Kama mnavyowatendea watu wa chini dhambi hii italipasua kanisa. Wapo waumini wametengwa kwa zinaa, Wapo waumini ndugu zao wamezikwa bila kanisa kushiriki kisa tu alikuwa ajarudishwa kundini, Wapo watu wametengwa na huduma za kanisa baada ya kubainika Wana vimada au mke zaidi ya mmoja lakini watu hao wote kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa na waumini wa Hali ya chini.

Matajiri na wenye nyadhifa hakuna sehemu mmewatenga Wala kukataa kuwazika. Simamieni misingi ya kanisa acheni kuwaona waumini flani Wana haki kuliko wengine.

Natumai utamwomba Mwenyenzi Mungu akusaidie kuliponya kanisa pale ambapo walio chini yako wamekuwa wakipotoka. Nakupenda nakutakia tafakuri njema huku ukilinda imani na kanisa ulilokabidhiwa.
Sijawahi kuona post ya kipumbavu kama hii kwanza kabisa ujue kabisa halihusiki na uzinzi wenu na ujue kabisa kwamba mahusiano ya sasa yamekuwa ni janga .swali LA kujiuliza ni je huyo Anna aliishije miaka mitatu na mwanaume hadi kuzaa,mtoto? Je huyo mwanaume alishampeleka kwao kumtambulisha? Alilipa mahari? Mila na tamaduni za kiafrica zinasemaje huu ya uchumba? Au ndoa? Tatizo lenu wadada mmezidi kujiachia hivyo hivyo mkizani kwamba kuzaa ndio kupata ndoa isitoshe Pete za uchumba feki wengine mnavishana bar halafu eti mnajiita wanandoa wakati hata familia zenu hawajui kama unaishi na mwanaume.ifike mahali mabinti muwe na adabu kaa kwa utulivu subiri kijana afike kwenu ajitambulishe ndio uambatane naye hata kama sio kwa harusi lakini heshima inakuwepo. Huyo Anna kwa ukweli unaaonekana ni Hawara sio make na atafahamika tu kama mzazi mwenzake na sio make Wa ndoa kwa hiyo akae kwa kutulia .sharia ya ndoa ingekuwa inatambua wadada waliozalishwa bado ndoa nyingi zingezuiliwa. Pia ukumbuke kwamba hata huyo mtoto Wa mbunge naye angekuwa na mimba wakaja wrote Wawili bado huyo mwanaume anaruhusiwa kuchagua mmoja kati yao na kufunga naye ndoa kwakuwa mapenzi hayalazimishwi. Ukumbuke pia kwamba mawaziri wengi na wabunge wengi waliacha wakezao Wa jamani Tena wenye watoto wengi tu kisa wake zao sio wasomi na wakaoa wanawake wengine wasomi Tena kwa ndoa halali za kanisani . mbona hamjawahi kuwaongelea? Au umemuona huyo binti Wa palanjo tu? Inawezekana umetumwa kuvuruga kabisa au ndoa ya huyo binti lakini hutaweza. Huyo binti simfahamu lakini namtakia baraka zote Mungu amtangulie . watanzania tupinguze majungu kama Anna ana haki aende mahakamani kama kuna Mali wamechuma pamoja atapewa share yake
 
Acheni kijana aoe

Haya mambo ya kuharibiana wakati ndoa zenyewr ni za manati hayana tija
 
Umeongea point
Ila ujifunze kutumia paragraphs - maana bila ya hivyo, utakua ni upumbavu pia
 
Labda huelewi kitu nilichoandika, pingamizi lenye mashiko ni kama kuna ndoa iliyofungwa kanisani au msikitini au serikalini yaani kama anayepinga ana cheti Cha ndoa halali Cha serikali au kimila ambayo imeshuhudiwa na kufanyika mbele ya kiongozi wa kimila Ila sio mnachukuana tu mnafanya umalaya halafu kanisa lisikilize pingamizi.

Ndoa nyingine ni utaratibu binafsi ambao hautambuliki kikanisa. Sasa kama umeishi kwenye utaratibu ambao hautambuliki kanisani huwezi kuleta malalamiko na kanisanlikusikilize lizuie ndoa .

Nia na madhumuni no kuzuia dhambi ya uzinzi kama mnataka kubariki tendo takatifu basi fuateni Baraka za kanisa otherwise itakuwa no mmeishi katika taratibu za kishetani.

Huwezi kuclaim haki wakati haujatenda haki. Walikuwa wapi miaka yote kurudi kundini kutibu na kubariki mahusiano yao ili yatambulike kikanisa?
Kisheria Ana ana hoja na nimezitaja.

1. Matunzo ya mtoto.

2. Machumo ya ndoa.

Ingawa Hana Cheti Cha ndoa ila Kwa kukaa kwake Kwa zaidi ya miaka miwili na kupata mtoto na jamaa akienda mahakamani atafanikiwa.

Hoja yako imeegemea hisia za kiimani, huliangalii kisheria.

Unasahau kwamba Makanisa na Misikiti ni mawakala tu wa Serikali , ila serikali ndio ina mamlaka ya Ndoa zote hapa nchini.

Sasa wakisikiliza ushauri wa mtu kama wewe hiyo ndoa haitafungwa maana akikimbilia mahakamani ataisimamisha.

Hivyo busara ni kumuita na kulimaliza pale pale, kabla hajakwenda kuzua balaa jingine.
 
Mwacheni huyu mpare aingie chakike maana wameru alikua anawasikia kwenye redio.
Sasa atawajua LIVE bila chenga.
 
Kisheria Ana ana hoja na nimezitaja.

1. Matunzo ya mtoto.

2. Machumo ya ndoa.

Ingawa Hana Cheti Cha ndoa ila Kwa kukaa kwake Kwa zaidi ya miaka miwili na kupata mtoto na jamaa akienda mahakamani atafanikiwa.

Hoja yako imeegemea hisia za kiimani, huliangalii kisheria.

Unasahau kwamba Makanisa na Misikiti ni mawakala tu wa Serikali , ila serikali ndio ina mamlaka ya Ndoa zote hapa nchini.

Sasa wakisikiliza ushauri wa mtu kama wewe hiyo ndoa haitafungwa maana akikimbilia mahakamani ataisimamisha.

Hivyo busara ni kumuita na kulimaliza pale pale, kabla hajakwenda kuzua balaa jingine.
Sasa hayobanadai mahakamani sio kanisani unabishana na mtu aliuekaa kwenye tasnia ya Sheria toka 2006
 
Hiyo huwa haifanyiki kama unavyodhani tu, atasikilizwa na kuulizwa sababu na ikibainika hakufunga ndoa kanisani au nilizotaja ndoa itaendelea kufungwa kanisa halishauri mambo ya Sheria no dini tu nadhani unanielewa. Otherwise ukibisha zaidi am not ready to argue anymore maana utakuwa wewe unajua zaidi
 
Unaweza kusoma post zote nilizoandika kwa ufahamu zaidi
 
Kwa tafsiri yako lakini.
Wewe ni mwanasheria au nabishana na layman!? Nakuelimiaha hutaki Tena bila fee note. Sasa kama huelewi so unaweza hata kugoogle sio unabisha unreasonably anyways wataelewa wengine we endelea kukaa na mwanamke ulidhani umemuoa siku ataolewa unabaki umedata mlangoni kwa kanisa.
 
Hiyo huwa haifanyiki kama unavyodhani tu, atasikilizwa na kuulizwa sababu na ikibainika hakufunga ndoa kanisani au nilizotaja ndoa itaendelea kufungwa kanisa halishauri mambo ya Sheria no dini tu nadhani unanielewa. Otherwise ukibisha zaidi am not ready to argue anymore maana utakuwa wewe unajua zaidi
Mkuu, alichoeleza ndugu mwenye uzi na anachoshauri ni haki ya kusikilizwa kwa wenye pingamizi, kwamba wasikilizwe na uamuzi utolewe. Uamuzi ni pamoja na kuliona pingamizi lililowekwa kuwa halina mashiko. Kanisa haliwezi kukaa kimya au kuamua tu bila kuwasikiliza wapingaji.

Ndicho anachoshauri mwanajamvi mwenzetu hapa. Masuala ya pingamizi kusimama au kushindwa hayo ni ya kimaamuzi baada ya usikilizaji wa pingamizi
 
Ukifuatilia kuna post nimeelezea naona yeye ana yake anayojua tu na hataki tumuelezee kitaalamu the way ilivyo.

Mpaka wajue hakuwa na cheti na hawajawahi kufunga ndoa kanisani it goes without saying kwamba watakuwa wamemsikiliza sasa mambo huwezi kuandika gazeyi humu 😃

Naona anabisha tu, ni sawa mtu aseme nilikuwa nimevaa suruali sasa nilivua chupi si Ina maana alivua trouser trouser haihitaji kuwa Rocket scientist au uelezewe
 
Kama Anna na Mzava waliishi kama mume na mke Kwa zaidi ya miaka miwili, hapo Kuna presumption of marriage.

Anna ana pingamizi halali, asikilizwe.
Mkuu kikanisa presumption ni uzinifu uliokubuhu waroma wanaita usuria, wasahili wanaita uhawara.
Hana pingamizi juu ya ndoa hiyo bali ana haki juu ya matunzo ya mwanaye afate proper forum na sio magazeti.
NB: sifurahishwi na gazeti tajwa siku hizi limegeuka lakidaku.
Mwisho kabisa Dk. Shoo kama Askofu wa dayosisi na askofu mkuu tz ana mambo mengi ya msingi yakufanya hilo jambo laweza kutatuliwa na mchungaji wa ushirika husika au muinjilisti lakini mimi napendekeza wazee wa kanisa
 
Kwa nyongeza, tungeeleweshana kidogo mapingamizi yanayoweza kuwa na mashiko kupinga NDOA

  1. Iwapo wanaooana wana undugu wa damu uliokatazwa kisheria mf kaka na dada, baba na mtoto;
  2. Iwapo mmoja wa wanandoa hana akili sawasawa, hivyo kufanya uwepo wa free consent kuwa na shaka;
  3. Iwapo mmoja wa wanaotaka kuoana ana ndoa halali inayotambulika isiyoruhusu ongezeko la wake (wake wengi);
  4. Iwapo wanaokusudia kuoana hawajafika umri unaoruhusiwa kisheria kufanya hivyo;
  5. Iwapo mmoja wa wanaotarajiwa kuoana hajahiyari kufanya hivyo (anafanya tu kwa kuogopa vitisho nk) - ingawa hii kuthibitisha kwake....

N.k
 
Nope, presumption huwa inakuwa invoked mahakamani kwa ajili ya kumsaidia mwanamke apate mgawanyo wa mali kwa mchango aliotoa walipokuwa wanaishi pamoja.

Ina fact Sheria haitambui hiyo kwamba ni marriage but inakuwa presumed tu for purposes of mgawanyo wa mali na custody ya mtoto/ watoto.

Ina other way hiyo ni concubinage tu (umalaya) na huwezi hata kwenda kanisani kusema uliishi nae sababu kabisa haliruhusu umalaya. Hii Ina maana ya kwamba kanisa halina Mamlaka ya kusikiliza malalamiko hayo Bali huyo mhusika anapaswa aende mahakamani kuomba apewe mgawanyo wa mali na custody ya watoto kama itaonekana kweli aliishi na kupata status ya kuwa mke kwa kutambulika na majirani pamoja na kuishi na mwanaume kwa miaka mitatu mfululizo basi Mahakama huinvoke presumption of marriage ONLY for purposes za kumgawia mali tu.
Well elaborated, hii doctrine of presumption of marriage watu wengi sana wanaitafsiri ndivyo sivyo
 
Back
Top Bottom