Askofu Shoo, Wabunge Timotheo Mzava wa Korogwe na Dkt. Pallangyo wa Arumeru wanalichafua kanisa au wanachafuliwa?

Mkuu, alichoeleza ndugu mwenye uzi na anachoshauri ni haki ya kusikilizwa kwa wenye pingamizi, kwamba wasikilizwe na uamuzi utolewe. Uamuzi ni pamoja na kuliona pingamizi lililowekwa kuwa halina mashiko. Kanisa haliwezi kukaa kimya au kuamua tu bila kuwasikiliza wapingaji.

Ndicho anachoshauri mwanajamvi mwenzetu hapa. Masuala ya pingamizi kusimama au kushindwa hayo ni ya kimaamuzi baada ya usikilizaji wa pingamizi
Hawa Huwa wanaitwa Slow Learners, taratibu tu atakuelewa.
 
Sijawahi kuona post ya kipumbavu kama hii kwanza kabisa ujue kabisa halihusiki na uzinzi wenu na ujue kabisa kwamba mahusiano ya sasa yamekuwa ni janga .swali LA kujiuliza ni je huyo Anna aliishije miaka mitatu na mwanaume hadi kuzaa,mtoto? Je huyo mwanaume alishampeleka kwao kumtambulisha? Alilipa mahari? Mila na tamaduni za kiafrica zinasemaje huu ya uchumba? Au ndoa? Tatizo lenu wadada mmezidi kujiachia hivyo hivyo mkizani kwamba kuzaa ndio kupata ndoa isitoshe Pete za uchumba feki wengine mnavishana bar halafu eti mnajiita wanandoa wakati hata familia zenu hawajui kama unaishi na mwanaume.ifike mahali mabinti muwe na adabu kaa kwa utulivu subiri kijana afike kwenu ajitambulishe ndio uambatane naye hata kama sio kwa harusi lakini heshima inakuwepo. Huyo Anna kwa ukweli unaaonekana ni Hawara sio make na atafahamika tu kama mzazi mwenzake na sio make Wa ndoa kwa hiyo akae kwa kutulia .sharia ya ndoa ingekuwa inatambua wadada waliozalishwa bado ndoa nyingi zingezuiliwa. Pia ukumbuke kwamba hata huyo mtoto Wa mbunge naye angekuwa na mimba wakaja wrote Wawili bado huyo mwanaume anaruhusiwa kuchagua mmoja kati yao na kufunga naye ndoa kwakuwa mapenzi hayalazimishwi. Ukumbuke pia kwamba mawaziri wengi na wabunge wengi waliacha wakezao Wa jamani Tena wenye watoto wengi tu kisa wake zao sio wasomi na wakaoa wanawake wengine wasomi Tena kwa ndoa halali za kanisani . mbona hamjawahi kuwaongelea? Au umemuona huyo binti Wa palanjo tu? Inawezekana umetumwa kuvuruga kabisa au ndoa ya huyo binti lakini hutaweza. Huyo binti simfahamu lakini namtakia baraka zote Mungu amtangulie . watanzania tupinguze majungu kama Anna ana haki aende mahakamani kama kuna Mali wamechuma pamoja atapewa share yake
Uko sahihi kabisa.
 
Mkuu kuishi miaka miwili au zaidi ni kigezo pekee? Have they aquired the reputation of being husband and wife!? Na ukumbuke hiyo presumption of marriage is rebuttable.
Hapana, kuishi miaka miwili tu sio kigezo pekee. Mimi nilikuwa najibu hoja yako kwa maana akirudi kusoma kifungu ulichomuelekeza, jibu litakuwa ni kuishi miaka miwili pekee ndio kigezo maana kifungu tajwa hakina maneno mengine zaidi ya aliyoyasema.
 
Wewe ni mwanasheria au nabishana na layman!? Nakuelimiaha hutaki Tena bila fee note. Sasa kama huelewi so unaweza hata kugoogle sio unabisha unreasonably anyways wataelewa wengine we endelea kukaa na mwanamke ulidhani umemuoa siku ataolewa unabaki umedata mlangoni kwa kanisa.
Sasa bwana Mwanasheria,
Ikatokea huyo Binti akaenda mahakamani bado ndoa itafungwa??
 
Hapa tunachanganya haki mbili
1. Kufunga ndoa kikiristo ni haki ya Bwana Mzava na Haipingiki hata mbinguni
2. Haki ya uzinzi na machumo yake - ni haki ya Mzava na ex wake wagawane kama kuna walichochuma wakati wakinyanduana na uasherati hiyo kama hawakubaliani waende mahakamani sio kanisani. Ndoa kufungwa haizuii madai hayo.
Mzinzi aache ndoa ifungwe aendelee na madai yake.
 
Mkuu kikanisa presumption ni uzinifu uliokubuhu waroma wanaita usuria, wasahili wanaita uhawara.
Hana pingamizi juu ya ndoa hiyo bali ana haki juu ya matunzo ya mwanaye afate proper forum na sio magazeti.
NB: sifurahishwi na gazeti tajwa siku hizi limegeuka lakidaku.
Mwisho kabisa Dk. Shoo kama Askofu wa dayosisi na askofu mkuu tz ana mambo mengi ya msingi yakufanya hilo jambo laweza kutatuliwa na mchungaji wa ushirika husika au muinjilisti lakini mimi napendekeza wazee wa kanisa
Kiimani huko Sina shida Nako, hiyo ndiyo ni makosa ila ,

Kisheria Binti anahoja , pingamizi lake lisikilizwe.
 
Sasa huyo Anna anang'ang'ania nn. Mpuuzi kweli. Mkiambiwa musiishi na wanaume kabla ya ndoa hamueelewi. Unaishia kuzalishwa na basi. Nani anawadanganya kuishi na mtu miaka hata 40 ndo inakufanyeni kuwa wanandoa. Nianze tu kwenda kupinga ndoa wakati cheti sina cha ndoa tulikua tukiishi kama mahawara. Mambo mengine kujidhalilisha tu. Muhimu apate child support tu.
 
Kiimani huko Sina shida Nako, hiyo ndiyo ni makosa ila ,

Kisheria Binti anahoja , pingamizi lake lisikilizwe.
Lisikilizwe wapi ndugu
Kanisani!!?? Huko nimekupa position kuwa sio mke wa ndoa hivyo pingamizi lake halina mashiko.

Kiserikali, afate proper avenue kuomba maintanance ya mtoto ambayo ni haki yake na mwanaye.
 
Basi hapo huyo ex wa bwana mzava yuko totally desperated...sisi wazee wa kula tunda kimasikhara hapo tunashika bega tu na tumaneno tuchache tuchache twa kumkandia bwana mzava
 
Washauri wapeleke pingamizi la haki kwa askofu / Mchungaji, wekeni viambatanisho halali.

Wakilazimisha ndoa kuendelea kutangazwa wahini mahakamani.

Hawa wanaume ni vizuri nao wawajibishwe siyo kuja kuwaita singles mother wakati wao ndio sosi.

Ikibidi tafuteni mwanasheria makini alale nao mbele.

Goodmorning my JF.
 
Kama Anna na Mzava waliishi kama mume na mke Kwa zaidi ya miaka miwili, hapo Kuna presumption of marriage.

Anna ana pingamizi halali, asikilizwe.

Hata kama ana pingamizi halali hawezi kulazimisha mapenzi. Nadhani Anna aendelee na maisha yake kwa amani kabisa. Mapenzi ni hiyari hayalazimishwi, bora kuvunja hayo mahusiano ya sasa yasiyo na mdoa kuliko kuja kuteseka ndoani
 
Washauri wapeleke pingamizi la haki kwa askofu / Mchungaji, wekeni viambatanisho halali.

Wakilazimisha ndoa kuendelea kutangazwa wahini mahakamani.

Hawa wanaume ni vizuri nao wawajibishwe siyo kuja kuwaita singles mother wakati wao ndio sosi.

Ikibidi tafuteni mwanasheria makini alale nao mbele.

Goodmorning my JF.
Sasa Kama alitaka kuolewa, ilikuaje akatanguliza mtoto?

Ulaghai and playing victims has been ulaghai wa miaka yote wa gender fulani
 
Lakini lazima tukubali pia kwamba Mzava sasa sio tena yule Mfanyakazi wa Halmashauri, kwahiyo lazima na yeye ale Vitu vya hadhi yake. Anna angemvumilia tu waendelee kulea mtoto lakini amuache apate furaha
Nonsense!!
 
Kama Anna na Mzava waliishi kama mume na mke Kwa zaidi ya miaka miwili, hapo Kuna presumption of marriage.

Anna ana pingamizi halali, asikilizwe.
Ana ndoa ya kiserikali, haitambuliki kidini.
Hivyo ndoa yake kidini itakuwa hii ya sasa
 
Back
Top Bottom