Askofu Shoo ataka kanisa liongozwe kwa kanuni ili kuepuka migogoro

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo,amelitaka kanisa hilo liongozwe kwa misingi ya kanuni,sheria na taratibu ambazo wamejiwekea ili kutokuingia katika matatizo na migogoro.

Askofu Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa hilo, amesema kumekuwepo na baadhi ya Dayosisi chache za kanisa hilo ambazo misingi ya utawala bora na demokrasia ilipuuzwa na kujikuta zikiingia katika migogoro.

Mkuu huyo wa kanisa ameyasema hayo leo Jumatano Agosti 23,2023,akitoa taarifa ya muktasari ya utekelezaji katika mkutano mkuu wa 21 wa kanisa hilo unaofanyika katika Chuo Kikuu cha Makumira,kinachomilikiwa na kanisa hilo.

Amesema kuwa migogoro hiyo iliyotokea katika baadhi ya dayosisi ilikuwa, kupanuka na kugusa kanisa zima, akitolea mfano Dayosisi ya Kusini na Jimbo lake la Mufindi, Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (Lushoto) na Dayosisi ya Konde.

"Niwaombe kanisa letu liongozwe kwa misingi ya kanuni,sheria na taratibu ambazo tumejiwekea na tukitunza hizo mimi sioni sababu ya kauingia katika matatizo,niimeshuhudia katika dayosisi nyingi zikiendesha shughuli zake na kubadili aina ya viongozi kwa njia ya demokrasia kufuata amani na utulivu," amesema.

"Zimekuwepo dayosisi chache ambazo misingi ya utawala bora na demokrasia ilipuuzwa kwa hiyo kujikuta zikiingia katika migogoro na baadaye migogoro hiyo kupanuka na kugusa kanisa zima. Tunamshukuru Mungu kwamba Kanisa kupitia Halmashauri Kuu, tulishirikiana na dayosisi husika na kutatua migogoro hiyo," amesema.

Askofu Shoo amesema kuwa mambo madogomadogo ambayo yamebaki yanaendelea kushughulikiwa na dayosisi hizo na kuwa zipo dayosisi zingine zilizopata migogoro ya ndani lakini ilitatuliwa kabla ya kusambaa sana kama ilivyokuwa kwa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Dayosisi ya Konde.

Mwananchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom