Pesa kwenye account ya Rugemalila zilizotoka bank Kuu kwenye account ya ESCROW zilikuwa halali ya malipo ya ubia ya mtajwa na sharti la bank ya Mkombozi ilikuwa pesa haitatoka hadi ilipiwa kodi na ndivyo ilviyofanyika.Rugemalila ilikuwa pesa yake halali tokana na ubia kwenye mradi wa umeme. Kama yalikuwa malipo zaidi ya ilivyotakiwa ni makosa ya wanasheria wa serikali, mfanya biashara ye yote anaangalia faida ataipataje na mteja jukumu lake kulinda gharama zisiwe juu.
Rugemalila pato lake kwa kuwa ni kubwa alivyozoea aliamua kuelekeza pesa hizo kwenye shughuli za umma, na ili pesa ifanye kazi iliyokusudia kuna watu anaowaamini watazifanyia kazi kwa manufaa ya umma ndio maana alielekeza kwa maaskofu ambao wanafanya maendeleo ya umma bila kinyongo wala kuwa na bodi za kugawiana pesa.
Kosa la kuingiziwa pesa hizo lipo wapi wakati mtoaji Rugemalila ni pesa yake halali tokana na ubia wa uzalishaji umeme?
Bank ya Stanbic ndiyo inayotakiwa kulalamikiwa kwa kutotoza kodi pesa toka acc. ya ESCROW na ndio maana inafisha taarifa tokana na kosa hilo.