Askofu Nzigilwa: Rugemalira alitoa fedha za matoleo

Askofu Nzigilwa: Rugemalira alitoa fedha za matoleo

Pesa zilizoingizwa kwenye account ya bank ya Mkombozi zililipiwa koda na taarifa ya bank ilishawekwa hadharani kwenye vyombo vya habari na tuliijadili sana hapa Jf.

Pesa ambazo hazijalipiwa kodi ni zile zilizopitishwa kwenye account ya bank ya Stanbic ndizo tunazotakiwa kushinikiza banki isifiche iweka wazi kama ilivyofanya bank ya Mkombozi.

Watu wameamua kuchanganyikiwa. Asante kwa maelezo
 
We candid scope hivi ile account ya askofu ilifunguliwa mda mchache baada ya pesa kupigwa au ilikuwepo kabla?baada ile pesa imeendelea kuwa active au dormant.?tukipata majibu ya maswali haya tutajua ukweli.sio kutetea tu upuuzi
 
Hatari, wala siamini mtu kujitetea kwa Akaunti binafsi kutumika???
 
Kwa kweli njia ya mwongo ni fupi sana; unachokisema kinaweza kuwa kweli lakini hakimsaidii Askofu huyu kwa namna yeyote, labda kwa mtu anayeangalia mambo kwa juu juu tu. Kwa mfano, amesema na imewekwa katika mandishi kwamba alishtukia tu pesa nyingi iko kwenye account yake..!!! ndipo akauliza ni za nini......!!!!; kwa namna yeyote ile hakuna pesa ya ufadhili itakayotolewa pila kuwepo mazungumzo na mhusika.

Askofu atubu tu, maisha yaendelee.....

Acha uvivu soma taarifa vizuri. Aliombwa acc.
 
Kwenye thread hii nimeona unafki wa Wakatoliki wenzangu, wengi wanajifanya hawajui kama mkombozi ni benki yetu wakatoliki na taasisi zetu zote zina akaunti hapo. Huyu Askofu ni muhuni tu sawa na wahuni wengine.
 
We candid scope hivi ile account ya askofu ilifunguliwa mda mchache baada ya pesa kupigwa au ilikuwepo kabla?baada ile pesa imeendelea kuwa active au dormant.?tukipata majibu ya maswali haya tutajua ukweli.sio kutetea tu upuuzi

Soma maelezo yafuatayo utapata jibu sihitaji kurudiarudia jibu ambalo nilishaliweka hadharani mara kadhaa

Nijaribu kufafanua kidogo hapa
Watumishi wa kanisa ambao ni wachungaji iwe Maaskofu, mapadre au mashirika ya watawa wa kiume au kike huruhusiwa kuwa na account, lakini account hizo huwa wazi na kujulikana kwa mhasibu mkuu wa jimbo kuna baadhi huita TG (Treasure General) na wengine Procurator
. Katika account hizo binafsi ndimo mafao ya posho za utumishi wao huwekwa humo na na ndizo zinazotumika kwa matumizi binafsi kama mavazi, na kujikimu kimaisha. Ila baadhi ya mashirika ya watawa hairuhusiwi kuwa na account binafsi ila accont ya shirika tu.

Kuna wahisani wanaosaidia maendeleo katika kanisa iwe nyanja za afya, elimu, utume nk hupenda kutoa pesa zao na kuzielekeza kupitia kwa mtumishi wa kanisa iwe askofu au padre kadiri ya usimamizi wa miradi na shughuli alizo nazo na hata kwa mashirika ya watawa. Kwa kawaida pesa hizo huweza kuwekwa kwenye account yake binafsi na kisha matumizi yake kuyaelekeza kwenye shughuli iliyokusidiwa na wahisani. Hii hufanyika kwa malengo ya kuaminiwa mtumishi huyo ili pesa ifanye kazi kwa shughuli iliyokusudiwa na wahisani huhitaji kujua ufanisi wa mradi wanaoufadhilia.

Mfano jimbo Katoliki Njombe Mhashamu Askofu Alfred Maluma hupewa misaada kadhaa kujenga vinu vya vinavyoendeshwa na nguvu ya maji kuzalisha umeme katika parokia na vijiji kadhaa ambapo Rais Kikwete alienda kufungua mmoja wa mradi huo Tarafa ya mawengi huko Ludewa, wahisahi hupitisha pesa hizo moja kwa moja kwa Askofu na askofu huelekeza kwenye mradi uliokusudiwa.

Kawaida maaskofu si watu wa kujilimbikizia mali na matanuzi binafsi katika jimbo, hata huduma za usafiri ni mali ya kanisa na kipindi wanapomwendea baba wa milele account yake inakuwa mali ya kanisa hata gari atumialo ni mali ya kanisa ndio utaratibu wa kanisa Katoliki.

CC;
Matola
 
Kwa kweli njia ya mwongo ni fupi sana; unachokisema kinaweza kuwa kweli lakini hakimsaidii Askofu huyu kwa namna yeyote, labda kwa mtu anayeangalia mambo kwa juu juu tu. Kwa mfano, amesema na imewekwa katika mandishi kwamba alishtukia tu pesa nyingi iko kwenye account yake..!!! ndipo akauliza ni za nini......!!!!; kwa namna yeyote ile hakuna pesa ya ufadhili itakayotolewa pila kuwepo mazungumzo na mhusika.

Askofu atubu tu, maisha yaendelee.....
Assume kama ungekuwa umeingiziwa wewe ungeendelea kupiga kelele?
 
Jaribu kusoma na kuelewa mstari kwa mstari Askofu kasema ni matoleo na kwa uelewa wangu matoleo huwa yanatolewa kanisani, labda atengue kauli na kusema ulikua mchango kwa ajili ya huduma ya Askofu kwa kanisa na ndio maana ikawekwa kwa account yake binafsi na si ya kanisa, kama unagoma kunielewa usitoke mapovu lamba ndimu kimya kimya

sorry nikifika nyumbani kwenye pc nita highlight hiyo mistari vizuri
 
Huyu mpuuzi anafikiri anaongea na watoto au?

soma bandiko no5 hapo juu,ukitaka kujua kaulize pia kama miradi ya makanisa haipo inayoendeshwa chini ya padre mmoja mmoja? kama hili ni geni kwako karibu jimboni kwetu ntakuonyesha wengine wengi tu ili ikufungue macho
 
Wewe wacha kujitoa akili huyo Pengo mwenyewe akitaka pesa huwa anatuomba sisi parokia zote za Dar kila muumini tumchangie shilling 200 tu je unajuwa tupo wakatoliki wangapi Dar? Ukipata jibu ndio ujuwe Pengo hana shida na pesa za wezi kwa sababu tunampa pesa ya kutosha.
 
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa amevunja ukimya akisema ni kweli alipokea Sh40.4 milioni kutoka kwa mmiliki wa Kampuni ya VIP, James Rugemalira zikiwa matoleo ya kusaidia uendeshaji wa kanisa.

Askofu Nzigilwa ni mmoja wa watu waliopata fedha kutoka kwa Rugemalira anayehusishwa kugawa kwa watu mbalimbali mabilioni ya shilingi yanayohusishwa na fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow wakiwamo wabunge, mawaziri na viongozi wa dini.

Tayari baadhi ya viongozi wa Serikali wamewajibika kwa ama kutumia vibaya madaraka yao au kupokea fedha hizo kinyume cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

Kupitia taarifa yake ya kurasa tatu kwa vyombo vya habari, Askofu Nzigilwa alielezea uhusiano wake na familia ya Rugemalira ulivyoanza na jinsi ambavyo amekuwa akitoa sadaka na michango mbalimbali ya hali na mali.

“Kanisa linategemezwa na nguvu ya Roho Mtakatifu anayeliongoza kupitia michango ya watu. Hivyo, kwa waumini kutoa michango na matoleo kwa kanisa na watumishi wake ni jambo la kawaida katika desturi za imani yetu tangu nyakati za mitume,” alisema askofu huyo.

Alisema uhusiano wake na familia ya Rugemalira ulianza mwaka 2008 alipopangiwa katika Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozari Takatifu, Makongo Juu akiwa Paroko Msaidizi, Rugemalira akiwa muumini katika parokia hiyo.

Alisema akiwa katika parokia hiyo, walikuwa na ujenzi wa nyumba ya mapadri na mikakati ya ujenzi wa kanisa jipya la parokia hiyo na katika shughuli zote hizo, Rugemalira na waumini wengine walikuwa ni wachangiaji wazuri.

“Hata baada ya kuteuliwa kuwa Askofu Msaidizi tumekuwa tunashirikiana na kuwasiliana na familia ya Rugemalira katika masuala mbalimbali ya kikanisa na kijamii,” alisema.

Mamilioni yaingia
Kuhusu fedha hizo, Askofu Nzigilwa alisema katika moja ya mawasiliano yao Februari mwaka jana, Rugemalira alimuomba namba ya akaunti yake ya Benki ya Mkombozi ili aweke matoleo yake... “Kwa kuniomba akaunti hiyo nilijua anataka kuweka matoleo ya fedha; lakini kiasi alichokuwa amenuia kukiweka sikukijua mpaka nilipoangalia Bank Statement na kuona kampuni ya VIP Engineering imeingiza Sh40.4 milioni katika akaunti hiyo Februari 27, 2014.

“Niliwasiliana na Ndugu Rugemalira na kumwambia nimeona kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yangu; naye akaniambia hayo ni matoleo ambayo anaamini yatasaidia katika shughuli zetu za kitume na kichungaji. Nikamshukuru kwa ukarimu huo mkubwa,” alisema.

Alisema matoleo hayo yalipokewa kwa moyo mnyofu kutoka kwa mtu anayefahamika kwa ukarimu wake katika kusaidia Kanisa na watumishi wake. “Biashara na kampuni anazomiliki Rugemalira kwa mujibu wa sheria za nchi haviwezi kumpa shaka mtu anayemfahamu uwezo wake au kampuni yake kutoa mchango mkubwa kama huo.”

Kazi za matoleo

Huku akisema tangu apokee fedha hizo hakuna mamlaka yoyote iliyowahi kumhoji Askofu Nzigilwa alisema matoleo ya waumini hutumika katika shughuli na uendeshaji wa jimbo, parokia na taasisi zake; katika miradi maalumu iliyokusudiwa na pia kwa kadri ya matakwa na lengo la mtoaji.

Chanzo:
Mwananchi

manii naona kwa maelezo hyo bora angekaa kimya tuu..
 
Hawa maaskofu ni wezi tu kama wezi wengine. Account binafsi ni ya nini wakati mtu unatunzwa na kanisa hadi toilet paper ya chooni unapewa bure?
Naweza sema kuwa kanisa katoliki ni lichafu mara mia moja ya maharamia waliomo ndani ya serikali ya Kikwete. Hilo linaonekana kwa serikali kujaribu kufunika aibu yao kwa kuwawajibisha baadhi ya wanufaika na pesa ya wizi lakini sii kwa kanisa katoloki. Hili kanisa limekubuhu na dhamira yake iliisha kufa kale hata kabla ya serikali ya Tanganyika kuwepo. Limekosa mamlaka ya kiuadilifu ya kukemea maovu na sisi raia popote tutakapowakuta mnakemea uovu tutawakataa kw kuwaambia 'shut up you hypocrite'
Nani asiyetambua kuwa maaskofu wamelambishwa rushwa ya pesa za escrow ili kuyamazia pesa hizo chafu kupitishiwa kwenye bank ya kanisa?
.
 
Kanisa halina akaunti mpaka akuingizie mwenye akaunti binafsi.wezi wakubwa nyie maaskoffu.

Na kwanini hakuweka wazi kanisani kama ilivyozoeleka kuwa muumini akitoa matoleo yake ht km hataki ajulikane kwa jina lkn taarifa huwa inatolewa tu kwamba tumepokea kiasi fulani toka kwa muumini mmoja.
 
Soma maelezo yafuatayo utapata jibu sihitaji kurudiarudia jibu ambalo nilishaliweka hadharani mara kadhaa

Nijaribu kufafanua kidogo hapa
Watumishi wa kanisa ambao ni wachungaji iwe Maaskofu, mapadre au mashirika ya watawa wa kiume au kike huruhusiwa kuwa na account, lakini account hizo huwa wazi na kujulikana kwa mhasibu mkuu wa jimbo kuna baadhi huita TG (Treasure General) na wengine Procurator
. Katika account hizo binafsi ndimo mafao ya posho za utumishi wao huwekwa humo na na ndizo zinazotumika kwa matumizi binafsi kama mavazi, na kujikimu kimaisha. Ila baadhi ya mashirika ya watawa hairuhusiwi kuwa na account binafsi ila accont ya shirika tu.

Kuna wahisani wanaosaidia maendeleo katika kanisa iwe nyanja za afya, elimu, utume nk hupenda kutoa pesa zao na kuzielekeza kupitia kwa mtumishi wa kanisa iwe askofu au padre kadiri ya usimamizi wa miradi na shughuli alizo nazo na hata kwa mashirika ya watawa. Kwa kawaida pesa hizo huweza kuwekwa kwenye account yake binafsi na kisha matumizi yake kuyaelekeza kwenye shughuli iliyokusidiwa na wahisani. Hii hufanyika kwa malengo ya kuaminiwa mtumishi huyo ili pesa ifanye kazi kwa shughuli iliyokusudiwa na wahisani huhitaji kujua ufanisi wa mradi wanaoufadhilia.

Mfano jimbo Katoliki Njombe Mhashamu Askofu Alfred Maluma hupewa misaada kadhaa kujenga vinu vya vinavyoendeshwa na nguvu ya maji kuzalisha umeme katika parokia na vijiji kadhaa ambapo Rais Kikwete alienda kufungua mmoja wa mradi huo Tarafa ya mawengi huko Ludewa, wahisahi hupitisha pesa hizo moja kwa moja kwa Askofu na askofu huelekeza kwenye mradi uliokusudiwa.

Kawaida maaskofu si watu wa kujilimbikizia mali na matanuzi binafsi katika jimbo, hata huduma za usafiri ni mali ya kanisa na kipindi wanapomwendea baba wa milele account yake inakuwa mali ya kanisa hata gari atumialo ni mali ya kanisa ndio utaratibu wa kanisa Katoliki.

CC;
Matola

WAMUACHE ASKOFU WETU MAILI 100 ...Kama unataka toa maoni batizwa kwanza

NIJUAVYO MIMI SIO KOSA KWA PESA KUPITIA KWA MTAWA ...KWA KUWA MALI ZOTE ZA WATAWA NA MAPADRE NI MALI YA KANISA ..KANISA LINA ACCESS 24/7 YA KUONA STATEMENT YA MTUMISHI WA MUNGU ....HAKUNA HOFU KWA AJILI KILA ANACHOFANYA NI MALI YA KANISA NA WAKRISTO
SHULE NYINGI NA HOSPITALI ZIMEJENGWA NA WAFADHILI KWA PESA KUPITIA MOJA KWA MOJA KWA WAMISIONARI HUSIKA ....WAKATILIKI HATUNA SHAKA NA WATUMISHI WETU
NA PIA TUNATAMBUA NI WANADAMU KAMA SISI.....ILA MAENDELEO TULIYOFANYA NI MAKUBWA SANA ..
KWA MFANO TOKA RAIS MWINYI ALIPORUHUSU KANISA KUWEKEZA ..NDANI YA MIAKA 10 TU KANISA LIMEFANIKIWA KUJENGA VITEGA UCHUMI VUNGI KULIKO VILE ILIVONYANGANYWA ...HADI WAKATI FULANI IKAMFANYA CARDINAL POLCARP PENGO KUMWAMBIA RAIS MKAPA KUWA KANISA HALINA TENA SHIDA SANA YA KURUDISHIWA VITEGA UCHUMI VYAKE ...LABDA VILE VYENYE MAENEO YA KUABUDU ..KWA KUWA WANAAMINI VIMECHAKAA NA GHARAMA YA KUKARABATI NI BORA WAENDELEE KUJENGA VIPYA
 
Sasa kinachofuata hapo ni kueleza kama hizo hela zilienda kusaidia kanisa au alijenga nyumba ya binti kule Kinyerezi. Kwa kuhonga hawa hawajambo.
 
Back
Top Bottom