Askofu Nzigilwa: Rugemalira alitoa fedha za matoleo

Askofu Nzigilwa: Rugemalira alitoa fedha za matoleo

Kama utaratibu wa account binafsi hutumika na unajulikana kwa viongozi wao na kama ni kweli sheria zao zinaruhusu, mimi sioni shida..... maama mwisho wa siku atajustify mapato yake.... provided bandiko la 5 liko kweli..... tusihukumu kama hatujui ukweli halisi.... tuendelee kutafuta ukweli kama bandiko la 5 ni la uwongo then askofu ana makosa kama ni la kweli then askofu hana kosa...
 
Kosa la Tibaijuka ni kutokana na kutofuata maadili ya utumishi wa umma katika serikali ya Tanzania ambapo alitakiwa kutoa taarifa kwa body ya maadili kitu ambacho hakukifanya na hoja hiyo ndiyo aliyoisema Kikwete na kumwondoa kwenye nafsi ya uwaziri.

Kwa upande wa Maaskofu taratibu katika kanisa zinaruhusu kutokana na baadhi ya wahisani kutoa misaada kupitia kwa watumishi wanaowaamini.
​sasa nadhani ni muda muafaka wa utetezi wake uendane na kuweka wazi matumizi ya hizo fedha alizopokea yamekwenda vipi???
 
“Niliwasiliana na Rugemalira na kumwambia nimeona kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yangu, naye akaniambia hayo ni matoleo yake ambayo anaamini yatasaidia katika shughuli zetu za kitume na kichungaji. Nikamshukuru kwa ukarimu huo mkubwa,” alibainisha Askofu huyo.



Teh teh eti shuguli zetu za Kitume......Mtume mpigaji huyu.
 
hahah kuna vitu vinachekesha san ujie ingekua ya kanisa ingeingizwa kwenye account ya kanisa jaman mbona tunatoaga sadaka na cjawah ckia hela ya kanisa inaingizwa kwenye ac ya askofu au mchungaji
 
jkk8
jkk2
images

Nijaribu kufafanua kidogo hapa

Watumishi wa kanisa ambao ni wachungaji iwe Maaskofu, mapadre au mashirika ya watawa wa kiume au kiume huruhusiwa kuwa na account, lakini account hizo huwa wazi na kujulikana kwa mhasibu mkuu wa jimbo kuna baadhi huita TG (Treasure General) na wengine Procurator
. Katika account hizo binafsi ndimo mafao ya posho za utumishi wao huwekwa humo na na ndizo zinazotumika kwa matumizi binafsi kama mavazi, na kujikimu kimaisha. Ila baadhi ya mashirika ya watawa hairuhusiwi kuwa na account binafsi ila accont ya shirika tu.

Kuna wahisani wanaosaidia maendeleo katika kanisa iwe nyanja za afya, elimu, utume nk hupenda kutoa pesa zao na kuzielekeza kupitia kwa mtumishi wa kanisa iwe askofu au padre kadiri ya usimamizi wa miradi na shughuli alizo nazo na hata kwa mashirika ya watawa. Kwa kawaida pesa hizo huweza kuwekwa kwenye account yake binafsi na kisha matumizi yake kuyaelekeza kwenye shughuli iliyokusidiwa na wahisani. Hii hufanyika kwa malengo ya kuaminiwa mtumishi huyo ili pesa ifanye kazi kwa shughuli iliyokusudiwa na wahisani huhitaji kujua ufanisi wa mradi wanaoufadhilia.

Mfano jimbo Katoliki Njombe Mhashamu Askofu Alfred Maluma hupewa misaada kadhaa kujenga vinu vya vinavyoendeshwa na nguvu ya maji kuzalisha umeme katika parokia na vijiji kadhaa ambapo Rais Kikwete alienda kufungua mmoja wa mradi huo Tarafa ya mawengi huko Ludewa, wahisahi hupitisha pesa hizo moja kwa moja kwa Askofu na askofu huelekeza kwenye mradi uliokusudiwa.

Kawaida maaskofu si watu wa kujilimbikizia mali na matanuzi binafsi katika jimbo, hata huduma za usafiri ni mali ya kanisa na kipindi wanapomwendea baba wa milele account yake inakuwa mali ya kanisa hata gari atumialo ni mali ya kanisa ndio utaratibu wa kanisa Katoliki.



CC; lancanshire

Maelezo yako ni mazuri sana na nashukuru kwa taarifa yako. lakini tatizo ambalo mimi binafsi naliona hapa, nadhani hata baba Askofu Nzigilwa hajaliona, na wewe pia naona hujaliona - tatizo siyo hasa kule kuingiziwa fedha. tatizo ni fedha hizo zimetoka kwa nani. Pamoja na kwamba Rugemalira alionekana kama muumini mzuri anayechangia michango mingi, kulikuwa na haja ya kuwa makini sana naye, hasa kwa kutambua kwamba IPTL ambayo ndio inamwingizia fedha nyingi nadhani kuliko miradi yake yote, ni MKATABA WA KIFISADI unaonyonya rasilimali kutoka kwa wanyonge kwenda kwa watanzania wachache, watawala wakiwemo ndani. kama mkataba wa IPTL ungekuwa halali kabisa, wala huyu ndugu asingepata mabilioni ya kugawa kama njugu. kwa kumpokea ndugu Rugemalira na kupokea misaada yake, Kanisa linatumika kama chombo cha kumtakatisha madhambi yake - siyo kwa toba, kama Yesu alivyofanya kwa Zakayo [Lk. 19:1-10] ambaye ni sawa kabisa na Rugemalira - bali kwa rushwa. Ingawa Yesu alikula pilau ya Zakayo, iliyotokana na fedha ya ufisadi, lakini Zakayo alitubu na kuacha ufisadi, na kurejesha kwa wote aliowadhulumu. na ndivyo Maaskofu wetu inawabidi wafanye hivyo. kama wanakuwa na mahusiano na Mafisadi au mawakala wao, basi iwe ni kwa kuwakomboa watubu na kufanya malipizi.

Tukio hili liamshe Kanisa, ili lijione kwamba sasa lipo wapi. Kanisa linatakiwa kuwa pamoja na wanyonge, likiwa katika mapambano dhidi ya Unyonyaji na ukandamizaji. lakini sasa limetekwa na kuwa chombo cha wanyonyaji na wakandamizaji. Kwa kuwa Mungu mwenyewe alisema kwamba "milango ya kuzimu haitalishinda" [Mathayo 16:18], naamini kwamba Mungu anazo njia zake za kulisafisha kanisa lake. Viongozi wetu wa dini wajihadhari wasijekuwa sehemu ya "taka itakayosafishwa"
 
Je awakuwa na account ya kanisa?sasa iweje pesa hiyo iwekwe katika account ya mtu binafisi?pia je baada ya kuwa kupokea pesa hiyo ktk account yake aliwaeleza viongozi wa kanisa au parokia?maana michango yote utangazwa mwisho wa ibada ikiwa ni pamoja na hayo matoleo
 
Upumbavu wako ni kufananisha credibility ya Mzee wa Upako a.k.a Tranfoma a.k.a chuma cha reli a.k.a homa ya Jiji na Askofu wa kanisa katoliki. Uko very wrong
Nahisi level yako ya kufikiri na kuchanganua mambo iko juu sana, ngoja nikae na upumbavu wangu wewe muelevu sikuwezi
 
Wananchi wamekuwa na imani na maaskofu ila kwa hili sifuri tu acha kuhadaa watu,mbona maaskofu wa makanisa mengine hawakupewa matoleo hayo???? walimu wanadai shilingi ngapi??? hali ya huduma msingi za binadamu ikoje?? mfano afya, maji, barabara, elimu na mengine??? nyie mwajiita wasodhambi kumbe unafiki mtupu jehanamu inawangoja

very low think twice.
 
Huwezi kuzuia padre au askofu kuwa na acount binafsi, hata tu kule uhasibu wa jimboni kila mtumishi yaani padre hata askofu ana account yake.

Kuna baadhi ya maeneo yako mbali na ofisi za jimbo, mfano jimbo kuu la Tabora watumishi wa kanisa wanaoishi Sikonge muhimu kuwa na account zao bank ya pale sikonge kuliko gharama ya kwenda hadi makao makuu ya mkoa na jimbo kuu Tabora. Jaribu kuona jambo hili kipana zaidi. Na hakuna kosa la wazi kuingiziwa pesa kwenye account binafsi kwa vile ni jambo lililozoeleka hivyo toka kwa wahisani mbalimbali sababu ya mtumishi wa kanisa kuaminiwa.

asante kwa tafakari nzito tatizo watu humu wanakomenti kishabiki.
 
Je awakuwa na account ya kanisa?sasa iweje pesa hiyo iwekwe katika account ya mtu binafisi?pia je baada ya kuwa kupokea pesa hiyo ktk account yake aliwaeleza viongozi wa kanisa au parokia?maana michango yote utangazwa mwisho wa ibada ikiwa ni pamoja na hayo matoleo
nadhani baadhi ya maswali yako yanajibiwa na bandiko la 5 mkuu...
 
Je awakuwa na account ya kanisa?sasa iweje pesa hiyo iwekwe katika account ya mtu binafisi?pia je baada ya kuwa kupokea pesa hiyo ktk account yake aliwaeleza viongozi wa kanisa au parokia?maana michango yote utangazwa mwisho wa ibada ikiwa ni pamoja na hayo matoleo

soma bandiko #5
 
Nijaribu kufafanua kidogo hapa
Watumishi wa kanisa ambao ni wachungaji iwe Maaskofu, mapadre au mashirika ya watawa wa kiume au kiume huruhusiwa kuwa na account, lakini account hizo huwa wazi na kujulikana kwa mhasibu mkuu wa jimbo kuna baadhi huita TG (Treasure General) na wengine Procurator
. Katika account hizo binafsi ndimo mafao ya posho za utumishi wao huwekwa humo na na ndizo zinazotumika kwa matumizi binafsi kama mavazi, na kujikimu kimaisha. Ila baadhi ya mashirika ya watawa hairuhusiwi kuwa na account binafsi ila accont ya shirika tu.

Kuna wahisani wanaosaidia maendeleo katika kanisa iwe nyanja za afya, elimu, utume nk hupenda kutoa pesa zao na kuzielekeza kupitia kwa mtumishi wa kanisa iwe askofu au padre kadiri ya usimamizi wa miradi na shughuli alizo nazo na hata kwa mashirika ya watawa. Kwa kawaida pesa hizo huweza kuwekwa kwenye account yake binafsi na kisha matumizi yake kuyaelekeza kwenye shughuli iliyokusidiwa na wahisani. Hii hufanyika kwa malengo ya kuaminiwa mtumishi huyo ili pesa ifanye kazi kwa shughuli iliyokusudiwa na wahisani huhitaji kujua ufanisi wa mradi wanaoufadhilia.

Mfano jimbo Katoliki Njombe Mhashamu Askofu Alfred Maluma hupewa misaada kadhaa kujenga vinu vya vinavyoendeshwa na nguvu ya maji kuzalisha umeme katika parokia na vijiji kadhaa ambapo Rais Kikwete alienda kufungua mmoja wa mradi huo Tarafa ya mawengi huko Ludewa, wahisahi hupitisha pesa hizo moja kwa moja kwa Askofu na askofu huelekeza kwenye mradi uliokusudiwa.

Kawaida maaskofu si watu wa kujilimbikizia mali na matanuzi binafsi katika jimbo, hata huduma za usafiri ni mali ya kanisa na kipindi wanapomwendea baba wa milele account yake inakuwa mali ya kanisa hata gari atumialo ni mali ya kanisa ndio utaratibu wa kanisa Katoliki.

Nimekusoma
 
Kwa utetezi wa baadhi ya great thinkers eti sio vibaya matoleo yakatolewa kwenye account binafsi ya Askofu, basi kumbe Ruge hata ile kodi kumbe angeilipa kwa account ya Mwigulu Nchemba. Nafikiria kwa kelele tu.
 
Kama utaratibu wa account binafsi hutumika na unajulikana kwa viongozi wao na kama ni kweli sheria zao zinaruhusu, mimi sioni shida..... maama mwisho wa siku atajustify mapato yake.... provided bandiko la 5 liko kweli..... tusihukumu kama hatujui ukweli halisi.... tuendelee kutafuta ukweli kama bandiko la 5 ni la uwongo then askofu ana makosa kama ni la kweli then askofu hana kosa...

Nimekusoma. Watu hawataki kutafuta ukweli wanataka kuburuzwa na wanasiasa uchwara
 
A
Unauliza kosa liko wapi kweli wewe kipofu hizi pesa zilikua mali ya askofu au mali ya kanisa.panua ubongo huo

Pesa ni mali ya Rugemalila ambazo ulikuwa mgao wa hisa yake na akaamua zipitishiwe bank ya Mkombozi na azielekeze anakotaka kadiri ya anavyotaka mwenye mali. Kwa vile Rugemalila hakuwa na haja na pesa hizo akaamua kuzielekeza kwenye matumizi ya huduma za umma kupitia watu anaowafahamu akiwemo askofu mtajwa hapo juu, askofu Kialini na Tibaijuka. Pesa hizo zililipiwa kodi kadiri ya maelezo ya bank ya mkombozi.

Jambo ambalo untakiwa kujenga hoja lisilofafanuliwa ni pesa zilizopitishiwa bank ya Stabnbic ambazo hazijaelezwa toka account ya ESCROW mnufaika alikuwa nani na kuanza kuwagawia ambao imebaki siri na hazikulipiwa kodi.
 
Kwa utetezi wa baadhi ya great thinkers eti sio vibaya matoleo yakatolewa kwenye account binafsi ya Askofu, basi kumbe Ruge hata ile kodi kumbe angeilipa kwa account ya Mwigulu Nchemba. Nafikiria kwa kelele tu.

Kweli unafikiria kwa kelele
 
ndo mana sikuliona kosa la Tibaijuka kuingiziwa fedha hizo hizo kutoka kwa mwanahisa huyo huyo na Rais akampiga chini ndo mana narudia tena aondoe utumbo wake hapa
nadhani utakuwa umenielewa
Nakumbuka wakati wa mavuno jimbo kuu la dsm,Parokia mbalimbali zilitangaza kuwa wamefanikiwa kupata mavuno kiasi fulani na pesa imewekwa account ya jimbo kuu na ilitangazwa.Walichopewa maaskofu wetu ni pesa ambayo aliyepewa ana kuwa huru kuitumia kwa apendalo yeye na kama ingeingizwa kwenye account ya parokia kusingekuwa na shaka.Kosa la Tibaijuka ni la kimaadili, aliingiziwa pesa kwenye account binafsi na alitakiwa autangazie uma au awataarifu tume ya maadili na zawadi hiyo yaweza kuwa mali ya serikali.Aliingiziwa asubuhi na jioni akatoa na haijulikani alipeleka wapi......Baadaye oooh nimelipa deni...too late!!!
 
Back
Top Bottom