Askofu Mwamakula na matembezi ya hiyari Nchi nzima

Hivi muitiko ukoje huko uraiani kuhusiana na haya maandamano?
 
Tangu zama za kale manabii , walimu wa dini na makuhani walikuwa na jukumu la kuwaonya waziwazi watawala ambao walikuwa wanakengeuka, Yohana Mbatizaji alifanya vivyo hivyo hadi ikapelekea kifo chake baada ya mke wa mtawala kuchukizwa baada ya kuambiwa ukweli wa maovu yake. Anachofana askofu ni sahihi kabisa, mtawala anapokwenda kinyume na kiapo chake cha utii wa kiti ni lazima aonywe na aambiwe ukweli. Askofu - kweli imekuweka huru - Mwana kondoo ameshinda - Tutatembea tu kudai uhuru na haki zetu
Tofautisha mawili.

Kwanza ni theocracy. Hapa mamlaka ya nchi yanatoka kwa MUNGU, na viongozi wa dini ni wasaidizi wa Mungu. Kwa kiwango hiki: "Anachofana askofu ni sahihi kabisa, mtawala anapokwenda kinyume na kiapo chake cha utii wa kiti ni lazima aonywe na aambiwe ukweli [kupitia mdomo wa nabii]." Tanzania sio theocracy.

Pili, ni democracy: Hapa mamlaka ya nchi yanatoka kwa UMMA, na viongozi wa dini ni sehemu ya umma, kila kiongozi akiwa na kura moja kama raia na sio kama kiongozi wa dini. Kwa kiwango hiki: "Anachofana askofu" SIO "sahihi kabisa." Tanzania ni democracy.

Uaskofu wake pembeni, bado anayo mamlaka yake ya URAIA kuongoza hayo maandamano anayotaka yafanyike.

Mwisho: Sheria ya Vyama vya Kijamii, pamoja na marekebisho yake ya 2019, inasema kuwa kiongozi wa dini anayo mamlaka juu ya waumini waliomo katika REJESTA YA KANISA LAKE, na sio juu ya mtu mwingine yeyote.

Askofu Mwamakula analifahamu hili vema, na anajua kuwa kutumia kofia ya uaskofu kuitisha maandamano haya ni kuvunja sheria hiyo.

In fact, hata TBC wanapowaleta viongozi wa dini na kuwapa air time ili walihutubie Taifa zima, bila kujali raia yupi ni mfuasi wa kingozi wa dini gani, wanakuwa wanavunja sheria hii. Mamlaka ya kuhubiri aliyo nayo kiongozi wa dini yanapaswa kuishia kwenye uzio wa Kanisa lake kama sio msikiti wake.

Karibuni Sumbawanga.
 
Anayetaka kushiriki anaruhusiwa bila kujali chama, kabila ama dini yake, lakini anayeona huyo Askofu ni kikwazo kushiriki anaweza kuanzisha njia yake yoyote aitakayo, ili mradi lengo ni kudai katiba mpya na sio kubatizwa.
Huo ndio mgawanyiko ninaozungumzia
 
Huo ndio mgawanyiko ninaozungumzia
Ulitakaje labda, maana huyo Askofu hajamzuia mtu yoyote kudai katiba mpya. Au unataka huyo askofu aendelee kusubiri mpaka apitakane mtu aliye neutral? Je huyo mtu asipotokea? Na huyo mtu neutral anangoja nini kuanzisha hayo madai?
 
Kwanza ni theocracy. Hapa mamlaka ya nchi yanatoka kwa MUNGU, na viongozi wa dini ni wasaidizi wa Mungu. Kwa kiwango hiki: "Anachofana askofu ni sahihi kabisa, mtawala anapokwenda kinyume na kiapo chake cha utii wa kiti ni lazima aonywe na aambiwe ukweli [kupitia mdomo wa nabii]."

Pili, ni democracy: Hapa mamlaka ya nchi yanatoka kwa UMMA, na viongozi wa dini ni sehemu ya umma, kila kiongozi akiwa na kura moja kama raia na sio kama kiongozi wa dini. Kwa kiwango hiki: "Anachofana askofu" SIO "sahihi kabisa."

Uaskofu wake pembeni, bado anayo mamlaka yake ya URAIA kuongoza hayo maandamano anayotaka yafanyike.

Mwisho: Sheria ya Vyama vya Kijamii, pamoja na marekebisho yake ya 2019, inasema kuwa kiongozi wa dini anayo mamlaka juu ya waumini waliomo katika REJESTA YA KANISA LAKE, na sio juu ya mtu mwingine yeyote.

Askofu Mwamakula analifahamu hili vema, na anajua kuwa kutumia kofia ya uaskofu kuitisha maandamano haya ni kuvunja sheria hiyo.

In fact, hata TBC wanapowaleta viongozi wa dini na kuwapa air time ili walihutubie Taifa wanakuwa wanavunja sheria hii. Mamlaka ya kuhubiri aliyo nayo kiongozi wa dini yanapaswa kuishia kwenye uzio wa Kanisa lake kama sio msikiti wake.

Karibuni Sumbawanga.
 
Ulitakaje labda, maana huyo Askofu hajamzuia mtu yoyote kudai katiba mpya. Au unataka huyo askofu aendelee kusubiri mpaka apitakane mtu aliye neutral? Je huyo mtu asipotokea? Na huyo mtu neutral anangoja nini kuanzisha hayo madai?
Mimi nimeweka tu fact mezani kuwa huyo askofu hatopata ufuasi wenye uwakilishi wa kitaifa kwa wazo lake hilo.
 
Mheshimiwa Dkt. John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Amani iwe kwako!

Mheshimiwa Rais! Mimi Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula, nisimamaye katika zamu yangu kama Mtumishi wa Mungu katika zamani hizi za utawala wako kama Sauti ya Haki katika nchi, ninatuma ujumbe huu kwako, washauri wako na Watanzania kwa ujumla wao (Habakuki 2:1).

Kwamba mimi Askofu Mwamakula nimesukumwa kutoka moyo wangu na nafsi yangu kuongoza "Matembezi ya Hiyari" katika nchi nzima yenye lengo la kuuhamasisha Umma wa Tanzania kuhusu umuhimu wa Kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Kuandika Katiba Mpya. "Matembezi ya Hiyari" yatafanyika katika mikoa yote ya Tanzania na wilaya zake zote katika kipindi chote cha mwaka 2021.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa 28 Oktoba 2020, mimi nilitoa tamko kupitia Vyombo vya Habari kuwa Uchaguzi haukuwa Huru na wala haukuwa wa Haki. Hivyo, pamoja na mambo mengine nikatoa wito wa Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi itakayosimamia Uchaguzi mwingine na chaguzi nyingine zitakazofuata. Ni dhahiri kuwa tunapozungumzia Tume Huru ya Uchaguzi suala la Katiba Mpya haliwezi kuepukika!

Ninapenda Mheshimiwa Rais utambue kuwa kwa mtazamo wetu, tangu matokeo ya Uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamekuwa na maumivu makubwa, uhasama mkubwa na chuki isiyoelezeka miongoni mwa Watanzania! Ukweli huu hauwezi kuelezwa kwako wazi na watu wako wa karibu kwa sababu ya unafiki walionao kwako kwa lengo la kulinda maslahi yao binafsi, nk. Hata hivyo, Vyombo vya Usalama (ikiwemo Taasisi ya Usalama wa Taifa) vinajua ukweli huo na hata viongozi wa dini walio karibu na utawala wako wanajua kuhusu ukweli huo. Ushahidi mmojawapo wa hayo ni mamia ya wapinzani waliorundikwa katika Magereza karibu katika kila Mkoa au Wilaya nchini.

Mheshimiwa Rais, hali hii ya uhasama, chuki na hofu katika nchi haiwezi kuachwa kuendelea. Ni lazima sote kwa pamoja tutafute njia nzuri ya kuliponya taifa. Lakini kama kila mtu na kila taasisi wana hofu ya kutoa sauti na kuelezea hisia na ukweli hadharani, tutakuwa taifa gani sisi? Je, ni kweli kuwa sisi sote tu wanafiki katika nchi? Je, ni kweli kuwa sisi sote tupo kwa ajili ya kutafuta maslahi binafsi katika nchi? Je, ni kweli kuwa sisi sote hatuwezi kuuona uhalisia wa mambo katika nchi? Je, ni kweli kuwa sisi sote tunaogopa kuuawa na watu wasiojulikana endapo tutausema ukweli pasipo kuogopa? Je ni kweli kuwa sisi tunaogopa kuandamwa taasisi zetu endapo tutapaza sauti? Je, ni kweli kuwa sisi sote tunaogopa mali zetu kuguswa na familia zetu kutikiswa endapo tutasema ukweli? Je, ni kweli kuwa sisi sote tunaogopa 'kung'olewa' katika nafasi zetu za uongozi katika taasisi zetu endapo tutafumbua vinywa vyetu? Je, ni kweli kuwa sisi wengine ambao tutachukua hatua za kuieleza jamii ukweli tutakuwa sio wazalendo kwa nchi? Je, uzalendo kwa nchi ni pamoja na kutokumueleza ukweli kiongozi? Je, ni kweli kuwa Mheshimiwa Rais hawezi kupokea ushauri nje ya washauri wake? Sisi wengine tunaamini kuwa jibu la maswali hayo hapo juu ni HAPANA!

Ni kwa sababu hiyo, tunaamini kuwa "Matembezi ya Hiyari" yatatoa fursa kwa umma kutoa hisia zao kuhusiana na jambo muhimu sana katika nchi. Kwamba suala la Mjadala wa Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Kuandikwa kwa Katiba Mpya litaleta umoja wa kitaifa ambao kwa sasa haupo lakini pia litawapa matumaini watu kuhusu kushiriki kwa Uchaguzi mwingine. Matumaini hayo yataleta utulivu katika nchi lakini pia yataupa utulivu utawala wako katika ngwe hii ya mwisho kwako! Kinyume na hapo utakuwa ni muendelezo wa uhasama, chuki, vitisho, vurugu na kuathiriwa kwa uchumi wa nchi.

"Matembezi ya Hiyari" hayana lengo la kuvuruga utulivu na shughuli za uzalishaji katika nchi kwa kuwa yatakuwa na nguvu kubwa ya kimaadili na hayapita katika njia au barabara ambazo zinaendelea kujengwa, nk. Ndio maana tumeelekeza watembeaji kutokuzidi 20 kwa kundi moja na kuwapo kwa nafasi ya umbali wa nusu kilomita au kilomita moja katika ya kundi na kundi.

Ni kwa sababu hiyo, tunatarajia kuwa Vyombo vya Dola havitatumiwa kuzuia au kuvuruga Matembezi hayo iwe kwa kumsumbua Askofu au kuwasumbua watakaokuwa wanaambatana na Askofu au watembeaji wengine! Tunatumaini pia kuwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wakuu wa Polisi wa Wilaya hawatatumika kuzuia Matembezi hayo bali wanaweza kuwa sehemu kwa kuhudhuria na kuangalia usalama pale inapobidi.

Tunaamini kuwa kama Serikali yako na Vyombo vya Dola hawatatumia nguvu kuzuia vuguvugu hili la umma linaloongozwa na Askofu, basi Mheshimiwa Rais utaweza kumaliza muda wa uongozi wako salama. Lakini kama Serikali na Vyombo vya Dola watatumia mamlaka yao vibaya kwa kumzuia Askofu na kuwadhuru washiriki ambao wanakusudia kutembea kwa amani basi Serikali yako haiwezi kuwa na mwisho mwema na hata baada ya mwisho wenu kufika hamtaweza kufurahia maisha baada ya utawala wenu kumalizika!

Mwisho ninapenda kukujulisha kuwa nitazindua "Matembezi ya Hiyari" katika Majimbo ya Uchaguzi ya Ubungo na Kibamba katika Wilaya ya Ubungo katika tarehe nitakayoitangaza! Matembezi haya yanajulikana pia na Jumuiya ya Kimataifa ambayo itayafuatilia kwa ukaribu sana kutokea ndani na nje ya nchi!

Ni imani yangu kuwa Mungu atasema na nafsi ya Rais na kwamba Mungu atanilinda sawasawa na Neno lake (Zaburi 121). Lakini hata hivyo, hata kama Mungu katika hekima yake isiyoweza kuhojiwa ataruhusu mabaya yanaipate sitaweza kuogopa na nitaongoza Matembezi ya Hiyari kwa kuwa dhamiri yangu mbele za Mungu hailaumiki kuhusiana na jambo hili (Isaya 6:8-13).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Msalaba unakushinda unataka katiba. Lala huko subiri sadaka
 
Jamani hili zee linalojifanya askofu, limeshaonja hela za mabeberu, basi kila uchao ni kuja na matamko ya ajabu sana, hivi wa Mzee kazi yako hasa ni ipi? Kuna jambo unalitafuta.
 
Mwanzo mzuri.
Na wewe umeshafanyaga sherehe ya Mh Jakaya kuondoka madarakani? Maana Ulisema hujawahi kuona rais hafai kama yeye, leo tena unasemaje? Ina maana wewe kwa asili ni jitu la kupingapinga tu, ovyo kabisa wewe.
 
Huko kupinga kila kitu ni matokeo ya chuki walizopandikiza,najua wao wanakataa hili ila ukweli ukiwachunguza hao jamaa utaona kinachowasukuma ni chuki na si kwamba ni wakosoaji tu kama wanavyojiita na kwamba wanataka kuona hayo wanayokosoa yakirekebishwa. Chuki ndio huwafanya wapinge kila kitu kwa sababu huwezi kuona jambo zuri kwa unayemchukia na lengo kwao ni kuchafua na si kukosoa ili pasahishwe na ndio maana hata pakisahishwe walipokosoaga bado watapinga pia.
 
Baada ya kukataliwa na Wamorovian naona unahaha kutafuta waumini kwa mbinu mbadala ya kuishi na mihemko ya kisiasa.
Uroho wa madaraka unamsumbua. Kanisa kuu la Moravian walimkataa akajitenga na kuanziasha branch yake ya Moravian uamsho. Huko anaona hakuna waumini wengi na mileage ni ndogo. Sasa ameamua kuja na Plan C ili ajitangaze zaidi
 
Back
Top Bottom