Askofu Mwamakula na matembezi ya hiyari Nchi nzima

Askofu Mwamakula na matembezi ya hiyari Nchi nzima

Hoja yako ni nini hapa? Rejea niliyemjibu kisha uoanishe na ulichoniquote.
Uliyemquote kakumbushia kuhusu uwepo wa corona,sasa wewe kutaja mechi ya simba na yanga ulikuwa na maana gani?
 
Uliyemquote kakumbushia kuhusu uwepo wa corona,sasa wewe kutaja mechi ya simba na yanga ulikuwa na maana gani?

Niliyemquote kaonyesha kuwa maaandamano ni hatari kwakuwa kuna corona, mimi nimemjibu hiyo hofu yake ya Corona kwenye mikusanyiko haihusu mechi za simba na yanga?
 
Niliyemquote kaonyesha kuwa maaandamano ni hatari kwakuwa kuna corona, mimi nimemjibu hiyo hofu yake ya Corona kwenye mikusanyiko haihusu mechi za simba na yanga?
Huwezikujua pengine hata huko kwenye mechi za simba na yanga pia huwahusia kwa kuwakumbusha uwepo wa corona,au wewe unakusudia kuwa kwa sababu watu wanaenda kwenye mechi ya simba na yanga hali ya kuwa kuna corona basi pia ni sawa tu na kwenda kwenye maandamano hata kama kuna corona?
 
Mheshimiwa Dkt. John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Amani iwe kwako!

Mheshimiwa Rais! Mimi Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula, nisimamaye katika zamu yangu kama Mtumishi wa Mungu katika zamani hizi za utawala wako kama Sauti ya Haki katika nchi, ninatuma ujumbe huu kwako, washauri wako na Watanzania kwa ujumla wao (Habakuki 2:1).

Kwamba mimi Askofu Mwamakula nimesukumwa kutoka moyo wangu na nafsi yangu kuongoza "Matembezi ya Hiyari" katika nchi nzima yenye lengo la kuuhamasisha Umma wa Tanzania kuhusu umuhimu wa Kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Kuandika Katiba Mpya. "Matembezi ya Hiyari" yatafanyika katika mikoa yote ya Tanzania na wilaya zake zote katika kipindi chote cha mwaka 2021.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa 28 Oktoba 2020, mimi nilitoa tamko kupitia Vyombo vya Habari kuwa Uchaguzi haukuwa Huru na wala haukuwa wa Haki. Hivyo, pamoja na mambo mengine nikatoa wito wa Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi itakayosimamia Uchaguzi mwingine na chaguzi nyingine zitakazofuata. Ni dhahiri kuwa tunapozungumzia Tume Huru ya Uchaguzi suala la Katiba Mpya haliwezi kuepukika!

Ninapenda Mheshimiwa Rais utambue kuwa kwa mtazamo wetu, tangu matokeo ya Uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamekuwa na maumivu makubwa, uhasama mkubwa na chuki isiyoelezeka miongoni mwa Watanzania! Ukweli huu hauwezi kuelezwa kwako wazi na watu wako wa karibu kwa sababu ya unafiki walionao kwako kwa lengo la kulinda maslahi yao binafsi, nk. Hata hivyo, Vyombo vya Usalama (ikiwemo Taasisi ya Usalama wa Taifa) vinajua ukweli huo na hata viongozi wa dini walio karibu na utawala wako wanajua kuhusu ukweli huo. Ushahidi mmojawapo wa hayo ni mamia ya wapinzani waliorundikwa katika Magereza karibu katika kila Mkoa au Wilaya nchini.

Mheshimiwa Rais, hali hii ya uhasama, chuki na hofu katika nchi haiwezi kuachwa kuendelea. Ni lazima sote kwa pamoja tutafute njia nzuri ya kuliponya taifa. Lakini kama kila mtu na kila taasisi wana hofu ya kutoa sauti na kuelezea hisia na ukweli hadharani, tutakuwa taifa gani sisi? Je, ni kweli kuwa sisi sote tu wanafiki katika nchi? Je, ni kweli kuwa sisi sote tupo kwa ajili ya kutafuta maslahi binafsi katika nchi? Je, ni kweli kuwa sisi sote hatuwezi kuuona uhalisia wa mambo katika nchi? Je, ni kweli kuwa sisi sote tunaogopa kuuawa na watu wasiojulikana endapo tutausema ukweli pasipo kuogopa? Je ni kweli kuwa sisi tunaogopa kuandamwa taasisi zetu endapo tutapaza sauti? Je, ni kweli kuwa sisi sote tunaogopa mali zetu kuguswa na familia zetu kutikiswa endapo tutasema ukweli? Je, ni kweli kuwa sisi sote tunaogopa 'kung'olewa' katika nafasi zetu za uongozi katika taasisi zetu endapo tutafumbua vinywa vyetu? Je, ni kweli kuwa sisi wengine ambao tutachukua hatua za kuieleza jamii ukweli tutakuwa sio wazalendo kwa nchi? Je, uzalendo kwa nchi ni pamoja na kutokumueleza ukweli kiongozi? Je, ni kweli kuwa Mheshimiwa Rais hawezi kupokea ushauri nje ya washauri wake? Sisi wengine tunaamini kuwa jibu la maswali hayo hapo juu ni HAPANA!

Ni kwa sababu hiyo, tunaamini kuwa "Matembezi ya Hiyari" yatatoa fursa kwa umma kutoa hisia zao kuhusiana na jambo muhimu sana katika nchi. Kwamba suala la Mjadala wa Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Kuandikwa kwa Katiba Mpya litaleta umoja wa kitaifa ambao kwa sasa haupo lakini pia litawapa matumaini watu kuhusu kushiriki kwa Uchaguzi mwingine. Matumaini hayo yataleta utulivu katika nchi lakini pia yataupa utulivu utawala wako katika ngwe hii ya mwisho kwako! Kinyume na hapo utakuwa ni muendelezo wa uhasama, chuki, vitisho, vurugu na kuathiriwa kwa uchumi wa nchi.

"Matembezi ya Hiyari" hayana lengo la kuvuruga utulivu na shughuli za uzalishaji katika nchi kwa kuwa yatakuwa na nguvu kubwa ya kimaadili na hayapita katika njia au barabara ambazo zinaendelea kujengwa, nk. Ndio maana tumeelekeza watembeaji kutokuzidi 20 kwa kundi moja na kuwapo kwa nafasi ya umbali wa nusu kilomita au kilomita moja katika ya kundi na kundi.

Ni kwa sababu hiyo, tunatarajia kuwa Vyombo vya Dola havitatumiwa kuzuia au kuvuruga Matembezi hayo iwe kwa kumsumbua Askofu au kuwasumbua watakaokuwa wanaambatana na Askofu au watembeaji wengine! Tunatumaini pia kuwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wakuu wa Polisi wa Wilaya hawatatumika kuzuia Matembezi hayo bali wanaweza kuwa sehemu kwa kuhudhuria na kuangalia usalama pale inapobidi.

Tunaamini kuwa kama Serikali yako na Vyombo vya Dola hawatatumia nguvu kuzuia vuguvugu hili la umma linaloongozwa na Askofu, basi Mheshimiwa Rais utaweza kumaliza muda wa uongozi wako salama. Lakini kama Serikali na Vyombo vya Dola watatumia mamlaka yao vibaya kwa kumzuia Askofu na kuwadhuru washiriki ambao wanakusudia kutembea kwa amani basi Serikali yako haiwezi kuwa na mwisho mwema na hata baada ya mwisho wenu kufika hamtaweza kufurahia maisha baada ya utawala wenu kumalizika!

Mwisho ninapenda kukujulisha kuwa nitazindua "Matembezi ya Hiyari" katika Majimbo ya Uchaguzi ya Ubungo na Kibamba katika Wilaya ya Ubungo katika tarehe nitakayoitangaza! Matembezi haya yanajulikana pia na Jumuiya ya Kimataifa ambayo itayafuatilia kwa ukaribu sana kutokea ndani na nje ya nchi!

Ni imani yangu kuwa Mungu atasema na nafsi ya Rais na kwamba Mungu atanilinda sawasawa na Neno lake (Zaburi 121). Lakini hata hivyo, hata kama Mungu katika hekima yake isiyoweza kuhojiwa ataruhusu mabaya yanaipate sitaweza kuogopa na nitaongoza Matembezi ya Hiyari kwa kuwa dhamiri yangu mbele za Mungu hailaumiki kuhusiana na jambo hili (Isaya 6:8-13).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Askofu nani sijui, ningekushauri kabla hujatangaza hayo "maandamano" yako ungewauliza Mange na Lissu kwanini "maandamano" yao hayakufanikiwa. Ushauri wangu kwako, utafanikiwa sana kama hayo "maandamano" yako utayafanyia humu JF, lakini huku "site" utaishia kuaibika.
 
Huwezikujua pengine hata huko kwenye mechi za simba na yanga pia huwahusia kwa kuwakumbusha uwepo wa corona,au wewe unakusudia kuwa kwa sababu watu wanaenda kwenye mechi ya simba na yanga hali ya kuwa kuna corona basi pia ni sawa tu na kwenda kwenye maandamano hata kama kuna corona?

Ficha ujinga wako.
 
Askofu nani sijui, ningekushauri kabla hujatangaza hayo "maandamano" yako ungewauliza Mange na Lissu kwanini "maandamano" yao hayakufanikiwa. Ushauri wangu kwako, utafanikiwa sana kama hayo "maandamano" yako utayafanyia humu JF, lakini huku "site" utaishia kuaibika.
Kwani muitiko wa haya maandamano huko site ukoje?
 
Askofu nani sijui, ningekushauri kabla hujatangaza hayo "maandamano" yako ungewauliza Mange na Lissu kwanini "maandamano" yao hayakufanikiwa. Ushauri wangu kwako, utafanikiwa sana kama hayo "maandamano" yako utayafanyia humu JF, lakini huku "site" utaishia kuaibika.
Kama kawaida maandamano ni hapa jf mkuu, tunaanzia jukwaa moja hadi lingine. Sijui lini tunaanza
 
Mungu akubariki sana baba askofu.

MATAGA pivyu vitawabana mbona!
[emoji23][emoji23][emoji23] wabanwe vyupi kwaajili ya haya maandamano ya baba askofu? Aisee
 
Askofu nani sijui, ningekushauri kabla hujatangaza hayo "maandamano" yako ungewauliza Mange na Lissu kwanini "maandamano" yao hayakufanikiwa. Ushauri wangu kwako, utafanikiwa sana kama hayo "maandamano" yako utayafanyia humu JF, lakini huku "site" utaishia kuaibika.
Nadhani huyu askofu ni sawa na lisu, ni aina ya watu ambao kwa namna fulani mishipa ya kuonea aibu haifanyi kazi.
 
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Nina maswali machache:

1. Wale wasiokubaliana na hoja kuwa "mwanakondoo ameshinda" wanaalikwa kushiriki maandamano kwa kutumia kivutio gani?

2. Wale wasiotaka kumfuata "mwanakondoo" wanaalikwa kushiriki maandamano kwa kutumia kivutio gani?

3. Maandamano haya yana tofauti gani na yale maandamano ya operesheni UKUTA ya mwaka 2016 iliyoanzishwa na Chadema na baadaye kuzimwa na vyombo vya ulinzi na usalama?

4. Kwa nini maandamano haya yaratibiwe kwa kutumia kofia ya uaskofu wakati hoja inahusu Katiba ya nchi isiyofungamana na dini yoyote?

5. Taarifa rasmi imekwishatolewa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kutoa ulinzi kwa waandamanaji?

6. Katiba Mpya inayodaiwa itakuwa na maudhui gani?

7. Katiba mpya inayodaiwa itapatikana kwa mujibu wa mchakato gani wa kisheria?

Yafaa Askofu Mwamakula atumie mbinu halali ili kufukuzia lengo halalai.

Falsafa ya lengo lolote linaweza kuhalalisha mbinu yoyote, yaani Caiphas Principle (John 11:50), sio falsafa nzuri hata kidogo.

Na kujibu kosa kwa kufanya kosa sio mbinu ya kuzalisha haki, maana mtoto wa dhuluma ni dhuluma.

Ni hayo tu kwa sasa.
 
Kwahiyo mtu akiwa askofu haki zake za kiraia na kisiasa hupokwa?
Hajapokwa, ila tu ni kwamba chances za kufanikiwa ni very slim kutokana na religious profile ya Tanzania. Mobilizer wa kitu kama hii anatakiwa awe neutral, asiyeegemea dini yoyote. Ndipo ataweza kupata kukubalika na watu wa dini zote.
 
Tangu zama za kale manabii , walimu wa dini na makuhani walikuwa na jukumu la kuwaonya waziwazi watawala ambao walikuwa wanakengeuka, Yohana Mbatizaji alifanya vivyo hivyo hadi ikapelekea kifo chake baada ya mke wa mtawala kuchukizwa baada ya kuambiwa ukweli wa maovu yake

Anachofana askofu ni sahihi kabisa, mtawala anapokwenda kinyume na kiapo chake cha utii wa kiti ni lazima aonywe na aambiwe ukweli

Askofu - kweli imekuweka huru - Mwana kondoo ameshinda - Tutatembea tu kudai uhuru na haki zetu
 
Utakuta hili gazeti amendika kisha akaliposti kwenye account yake ya mtandaoni alafu anategemea Rais itamfikia.
tayari kashasoma - unapokuwa Rais wa nchi post kama hizi ni lazima zikufikie mapema mno
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hyuo askofu feki Mwamakula inabidi apimwe mkojo maana anaweza kuwa anavuta bangi
unaweza kutisha watu lakini huwezi kutisha wato wote - Askofu anaongozwa na roho mtakatifu - na hiyo courage aliyonayo who knows imetoka wapi? yawezekana inatoka kwa Muumba mwenyewe, yeye ni mjumbe tu anafikisha alichotumwa, kama ilivyokuwa kwa kina Yona na wengineo

CDM ushawanyamazisha, sasa pambana na mjumbe wa Mungu - over
 
Hata Lissu ilikuwa mpango wa Mungu.
 
Hajapokwa, ila tu ni kwamba chances za kufanikiwa ni very slim kutokana na religious profile ya Tanzania. Mobilizer wa kitu kama hii anatakiwa awe neutral, asiyeegemea dini yoyote. Ndipo ataweza kupata kukubalika na watu wa dini zote.

Anayetaka kushiriki anaruhusiwa bila kujali chama, kabila ama dini yake, lakini anayeona huyo Askofu ni kikwazo kushiriki anaweza kuanzisha njia yake yoyote aitakayo, ili mradi lengo ni kudai katiba mpya na sio kubatizwa.
 
Back
Top Bottom