Askofu Munga: Mkataba wa Bandari umetusaidia kuwajua Viongozi zaidi

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,933
31,178
Ameandika Baba Askofu Stephen Munga

MKATABA WA BANDARI UMETUSAIDIA KUJUANA ZAIDI

"Na hivi ndivyo tunavyoweza kutambua wazi kati ya walio watoto wa Mungu na walio watoto wa shetani. Mtu ye yote asiyetenda lililo haki si wa Mungu; wala asiyempenda ndugu yake si wa Mungu."
(1 Yohana 3:10)

Kwanza, Nimekubali kuwa ndugu hujuana vizuri wakati wa matatizo na migogoro. Hata uliodhani wanakuheshimu utawasikia wakikutukana. Wasiostahil8 kutukana walijaribu kumvunjia heshima Profesa Shivji wakisahau kwamba wapo watu heshima zao hazivunjwi kirahisi.

Pili, Mgogoro wa bandari umetufanya tujuane vizuri Watanzania. Baadhi ya watu walitiwa kiza fahamu na adabu zao wakabaki kama waliosimama uchi hadharani. Tukumbuke kuwa kujaribu kufunika ukweli na kufukia haki ni kama kuzima moto kwa petroli.

Tatu, Uzalendo na maadili mema tuliyojidai tunataka kuyajenga katika jamii yetu juhudi hizo tumezimwagia matope. Hata viongozi wa dini wenye dhamana ya kuadibisha jamii wametumika kwa uongo na majungu. Utamwambiaje mtoto asitukane wakati mwenyewe ni mtukanaji. Tusiwaharibie watoto maisha kwa ajili ya ulafi wa leo.

Nne, Tumedhalilishana kwa hoja zisizo na ufahamu wa kina. Wapo watu ambao akipewa kipande cha mkate aweza kutukana kijiji kizima. Hekima ni pamoja na kujua la kuzungumza kwa wakati ufaao na kwa kiasi kifaacho.

Hitimisho, hivi ni vita vikubwa kwani ni mvutano baina ya kweli na uongo; haki na dhuluma; wema na uovu; giza na nuru; na uzalendo na usaliti. Mpaka tutakapofika mwisho tutakuwa tumejuana vizuri. Kwamba asiyetenda lililo haki si wa Mungu; wala asiyempenda ndugu yake si wa Mungu.
 
Kuwa na viongozi hawa ni matokeo yetu,raia ni wajinga huwezi kuwa na viongozi wema.
 
Na memorandum of understanding kati ya makanisa na serikali ambapo wakristo wanakomba pesa za walipa kodi kifisadi je? Munga kaa kimya.
 
Bandari zetu za Tanganyika tunazitaka!

Eti kumeingizwa na somo la kiarabu kwa mitaala yetu ili kutuandaa watanzania kwamba, tutakaa na warabu milele na inatupasa tujue kuongea nao kiarabu

Tunataka bandari zetu
 
Bandari zetu za Tanganyika tunazitaka!

Eti kumeingizwa na somo la kiarabu kwa mitaala yetu ili kutuandaa watanzania kwamba, tutakaa na warabu milele na inatupasa tujue kuongea nao kiarabu

Tunataka bandari zetu
yule mama ni mshenzi sana, hao waarabu sijajua wamempa nini hadi ameanza kufanya mambo ya ajabu katika nchi kiasi hiki..!!
 
Andiko likapate Baraka zake,
Andiko likatutangulie ktk Vikao vyetu tarajiwa….,
Andiko likapate kuzitawala ndimi zetu,
Andiko likapate kumulika Akili zetu,
Andiko likapate kutufunua fahamu zetu,
Andiko likapate kuwasimamia wenye dhamana.

Aksante Baba Askofu,
 
Mzee Wasira anasemaje? Mzee Malecela is fully supporting the move ya mama. Ila ikumbukwe alifanyiwa ikhisani sana kwenye msiba wa mwanaye.
 
Back
Top Bottom