Askofu mkuu Ruwa'ichi anasema corona bado ipo, amesihi tuendelee kuvaa barakoa, tunawe mikono, tufuate kanuni za afya

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,325
Askofu mkuu wa jimbo katoliki la Dar es Salaam amewasihi waumini kufuata taratibu za kisayansi kupambana na corona.

Askofu ameomba tusaidiane na Mungu kupambana na corona.

Askofu amesisitiza kuwa corona bado ipo na kuwasihi waumini waendelee kuvaa baracoa, kunawa mikono na maji tiririka pamoja na kupunguza mikusanyiko isiyo ya lazima.

Ndugu zangu tuchukue tahadhari, covid inatisha na inaua kwa haraka sana.


 
Kuishi kwa tahadhari, ni Jambo linaloanzia kwenye mamlaka za nafsi yako kwa kushirikiana ba wadau kama Dini, Serikali, Asasi, Watalaamu wa afya, ndugu, jamaa na marafiki.
Kwani sisi tunamsikiliza zaidi yupi?
 
..sijui SERIKALI watakuwa na kauli gani baada ya tamko hili.

..hatukupaswa kuacha kuvaa barakoa, na kunawa mikono.
 
Baada askofu kufariki kanisa linamgeuka mfalme !! Kosa kubwa Kabisa kuwekwa mfukoni mwa jiwe ...Raid wa TEC mfukoni
 
IMG-20210127-WA0000.jpg
IMG-20210127-WA0001.jpg
 
Serikali haijamzuia mtu kuvaa Baraka au kunawa maji tiririka, kama unataka kuvuta hewa chafu uliyoitoa nje hilo lipo ndani ya uwezo wako...sisi wengine tunamtanguliza Mungu mbele!
 
..sijui SERIKALI watakuwa na kauli gani baada ya tamko hili.

..hatukupaswa kuacha kuvaa barakoa, na kunawa mikono.
Tamko litakuja na vijembe kama ni hili!

Kuna madhehebu hawajui kusali, yanatumiwa na mabeberu, yanachafua nchi!
Nireteeeenii Gwajimaa!
Niireeeeeeteeeeerniii Gwajiima!
Niiireeeeeeeeeteeeeeniiiiii Gwajimaaaa!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Serikali haijamzuia mtu kuvaa Baraka au kunawa maji tiririka, kama unataka kuvuta hewa chafu uliyoitoa nje hilo lipo ndani ya uwezo wako...sisi wengine tunamtanguliza Mungu mbele!
Rais ndie mkuu wa nchi na mkuu wa serikali. Kama yeye anapongeza watu kutokuvaa barakoa, wewe kwa akili zako ndogo kama za panya unaenlewa nini?
 
KWANI KUNA MTU YOYOTE AU KIONGOZI YOYOTE ALIEZUIA WATU WASINAWE WA KUVAA BARAKOA??
Iwapo rais ambae ndie mkuu wa nchi anapongeza watu wasiovaa barakoa, anasema korona haipo, watu wengine watavaa barakoa kwa sababu gani kama mkuu wa nchi anasema korona haipo.

Wewe kwa akili zako finyu unafikiri tatizo liko wapi?
 
Leo kuna mtu anazindua shamba kijijini kwake ngoja tusikilizie kama ataliongelea na hili jambo
 
Iwapo rais ambae ndie mkuu wa nchi anapongeza watu wasiovaa barakoa, anasema korona haipo, watu wengine watavaa barakoa kwa sababu gani kama mkuu wa nchi anasema korona haipo.

Wewe kwa akili zako finyu unafikiri tatizo liko wapi?
Raisi yupi kapongeza watu wasivae barakoa?? Kama unamzungumzia JPM, kumbuka ndie alieshauli watu wavae barakoa hats za kushona, ndipo watu waliwwza kujipatia kipato kwa kushona barakoa kuachana na zile za wazungu zilizokuwa na garama ya hali ya juuu. Sasa watu wamekazana kwamba watu walizuiliwa kuchukua tahadhali juuu ya korona, nani kawazuia?? Huyu huyu raisi wetu magufuli, ndie aliengia madarakani na kukuta Tanzania nzima kipindupindu kimeshamili kila kona, kwa hekima na ubunifu wa raisi wetu, alipendekeza usafi ufanyike kila mahali kila jumamosi ya mwisho wa mweziii. Jeeee watu na we we ukiwemo bado wanamwitikio huo kwa moyo mumojaaa?? Sasa mnataka raisi afanye nini tena?
 
Lazima ieleweke mtu anavyokuwa alerted kuhusu jambo ndivyo umakini wake unapoongezeka juu ya kujikinga na tatizo hilo, zaidi kama hiyo alert inatoka kwa kiongozi mwenye kutambulika kwenye jamii yake.

Tatizo hapa kwetu kuna kiongozi mkuu yeye bado mpaka leo anasema Corona hakuna, na cha ajabu zaidi wameibuka watu wanautetea huo msimamo, kwanini useme Corona hakuna wakati watu wako wanaugua na wengine kufa?

Lazima ieleweke wazi, kukiri tatizo fulani lipo ndio njia ya kwanza kuanza kupambana nalo, lakini kama bado hukubali unakuwa wa kwanza kuyumbisha juhudi za kupambana nalo.

Kwasababu utakuwa unawachanganya watu wako kwingine wanasikia ipo, wakirudi kwako unawaambia haipo, na kulingana na nafasi yake kuwa kubwa kimamlaka ana uwezekano mkubwa wa kupata uungwaji mkono matokeo yake wengi watateketea.

Kwa hili jamii yote inatakiwa iwe kitu kimoja, ili mapambano dhidi ya Corona yafanikiwe, vinginevyo hali itaendelea kuwa mbaya huko mahospitalini, huku tukidanganyana huku jf hakuna tatizo ni mafua tu yale.

Natumai hizi sauti zinazoanza kusikika sasa toka kila upande zitawafungua wengi masikio na ufahamu wao waijue hali halisi na wachukue tahadhari, kudanganyana sasa basi.
 
Serikali haijamzuia mtu kuvaa Baraka au kunawa maji tiririka, kama unataka kuvuta hewa chafu uliyoitoa nje hilo lipo ndani ya uwezo wako...sisi wengine tunamtanguliza Mungu mbele!
Imeandikwa "Usimjaribu Bwana Mungu wako". Chukua tahadhari!
 
KWANI KUNA MTU YOYOTE AU KIONGOZI YOYOTE ALIEZUIA WATU WASINAWE WA KUVAA BARAKOA??
Hawajazuia kweli ila wamezuia kupashana habari utaishia pabaya. Unakumbuka yule dada sijui Malecela alisema sijui kuna ugonjwa gani akaishia kuondolea na kuhutumiwa kibaraka. Serikali ni wajibu wake kutoa miongozo kwa watu wake na kauli ya serikali ni nzito vinginevyo ni sawa na dereva uko makini barabarani lakini mwingine anavunja sheria tu anakugonga unakufa wewe makini lenye fujo linapona. Uwazi katika suala hili utatusaidia huko mbele ya safari lakini kama tumeamuwa kuishi kama kisiwa tuendelee tu huko mbele tutanyosheana vidole tu.
 
Back
Top Bottom