Waziri Mkuu awataka Wananchi kujilinda na Magonjwa kwa kunawa mikono na kuvaa Barakoa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Watanzania wana jukumu kubwa la kumuenzi Balozi John Kijazi kwa kutenda yale yote mema aliyokuwa akitenda.

Aidha, amesema jukumu jingine ni kuendelea kuiombea familia yake, hasa katika kipindi hiki kigumu.

Akitoa salamu za serikali kwenye mazishi ya Balozi John Kijazi amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuliombea Taifa kama ambavyo Rais Dkt. Magufuli alihimiza jana, na kwamba jana Waislamu walitimiza, leo Wasabato na kesho anaamini wengine wataendelea.

Amesema serikali inawapenda wananchi wake na inaendelea kufuatilia magonjwa yote, lakini wananchi waendelee kuchukua tahadhari ikiwemo kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa.

Kuhusu ugonjwa wa Corona amesema inafahamika kwamba hii ni vita na imeanzia kwa wakubwa na bado inaendelea, hivyo ni vyema wananchi wakajiridhisha na vitu wanavyotumia ikiwemo barakoa, kama ambavyo Rais Magufuli amewahi kutahadharisha

BF884DDF-4C64-4716-9215-00BA98A6DB77.jpeg
 
Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, leo amewataka watanzania kuchukua hatua za kujikinga na magonjwa mbalimbali kwa kuvaa barakoa.

Amesema ni vyema watanzania wakavaa barakoa wanazotengeneza wao wenyewe ikiwa ni pamoja na kushona kwa vitambaa vyao, hasa wakiwa kwenye mikusanyiko, ili kujiepusha na zile zinazotoka nje zinazoweza kuwa sio nzuri kiafya.

My Take.
Naona sasa watanzania wote kwa umoja wetu tumeshajua Corona ipo, kilichobaki ni kuchukua hatua za kujilinda, asilaumiwe mtu tena.
 
Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo anewataka watanzania kuchukua hatua za kujikinga na magonjwa mbalimbali kwa kuvaa barakoa.

Amesema ni vyema watanzania wakavaa barakoa wanazotengeneza wenyewe ikiwa ni pamoja na kushona vitambaa vyao ili kujiepusha na zile zinazotoka nje zinazoweza kuwa sio nzuri kiafya.

My Take.
Naona sasa watanzania wote kwa umoja wetu tumeshajua Corona ipo, na sasa kilichobaki ni kuchukua hatua za kujilinda.
Waziri mkuu mwoga mwoga kama huyu wa nini sasa? Tangu shangazi watishiwe viboko basi hata kusema ukweli imekuwa shida? Kuna tatizo gani hadi tuvae Barakoa? Yaani kutamka neno Corona sasa hivi ni Uhaini?
 
Back
Top Bottom