#COVID19 Kigoma: RC apiga marufuku mikusanyiko. Sehemu zote zinazotoa huduma Watu wavae Barakoa na kunawa mikono

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema kutokana na kuwepo kwa wimbi la tatu la ugonjwa wa corona amesitisha shughuli zote za misongamano isiyo ya lazima kuanzia leo Julai23, 2021.

Akizungumza leo Ijumaa Julai 23, 2021 mjini hapa, amesema misongamano yenye ulazima tahadhari ya kutosha ichukuliwe bila kuathiri shughuli za kiuchumi na shughuli za kitaifa.

Amesema anawaelekeza wakuu wa wilaya na waganga wakuu wa wilaya zote mkoani humo kuhakikisha wanatekeleza maagizo yaliyotolewa na wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, yanatekelezwa kwa kufata katika ngazi zote kwa mujibu wa sheria ya afya ya jamii no 1 ya Mwaka 2009 na kuweka utaratibu mzuri kwa wale wanaoomba vibali vya shughuli zenye ulazima.

"Maeneo yote ya taasisi za kiserikali, maeneo yote ya kutoa huduma mbalimbali kama benki,nyumba za ibada na hospitali watu wazingatie kanuni walizopewa na wataalamu wa afya kwa kuvaa barakoa,kuwa na maeneo ya kunawa mikono yenye maji safi ya kutiririka,"amesema Andengenye.

Amesema elimu iendelee kutolewa kwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo sokoni, mashuleni na sehemu zenye mikusanyiko na kwenye vituo vya mabasi ambapo wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhakikisha si tu kwamba hawajazi abiria lakini wahakikishe wasafiri wanavaa barakoa na kunawaka mikono wakati wa safari zao.

Mwananchi
 
Hivi ni nani mwenye mamlaka ya kutangaza hali ya emergency fulani kisheria na kikatiba?

Mama Samia Suluhu Rais wa JMT na Amiri Jeshi mkuu ndiye mwenye mamlaka kisheria na kikatiba kutangaza hali yoyote ya dharula ktk nchi au sehemu fulani ya nchi na kuweka wazi hatua zunazopaswa kuchukuliwa.

Sasa Waziri fulani tu na labda DC au RC wanatoa wapi haya mamlaka? Rais Samia umelala na unaupiga mwingi tu huku ukiacha nchi ikiwa kwenye auto pilot gear.
 
Hivi ni nani mwenye mamlaka ya kutangaza hali ya emergency fulani kisheria na kikatiba...?

Mama Samia Suluhu Rais wa JMT na Amiri Jeshi mkuu ndiye mwenye mamlaka kisheria na kikatiba kutangaza hali yoyote ya dharula ktk nchi au sehemu fulani ya nchi na kuweka wazi hatua zunazopaswa kuchukuliwa...

Sasa Waziri fulani tu na labda DC au RC wanatoa wapi haya mamlaka? Rais Samia umelala na unaupiga mwingi tu huku ukiacha nchi ikiwa kwenye auto pilot gear...
Nchi haina Rais, hata wewe ukiamua kesho unaweza toa tamko lako.
 
Kama ni maigizo basi mpira wa yanga na simba mashabiki watapiga nyomi over mbilimbi
 
Back
Top Bottom