Askofu Liberatus Sangu ataka Ulinzi Kwa Watoto wa Kiume Dhidi ya Ushoga

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
1688833548695.png

ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga, Mhashamu Liberatus Sangu, amewataka wazazi na walezi nchini kujenga misingi imara ya imani na maadili kwa watoto wao na kuwalinda dhidi ya ushoga.

Kiongozi huyo wa kiroho alitoa rai hivo juzi wakati wa sherehe za kumpa daraja. la upadre James Mrema wa
Parokia уа Mwadui wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Alisema wazazi wanapaswa kuwa karibu na watoto wao. Wafuatilie mienendo yao ili kuwaepusha na janga la ushoga, alilolitaja sasa linachochewa kwa nguvu kubwa na makundi mbalimbali yakiwamo baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.

"Vitendo vya ushoga vikifumbiwa macho vitavuruga familia na ustawi wa jamii, ikiwamo wito mtakatifu wa upadre ambao unatoka katika familia," alisema Askofu Sangu.
 
Ah! Kumbe ni askofu wa kikatoliki? Ningeona ajabu kama askofu wa kipentekoste angelalama kuhusu ulinzi kwa mtoto wa kiume. Ukatolikini hakuna maadili huko
 
Back
Top Bottom