Askofu Kakobe jana leo na kesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Kakobe jana leo na kesho

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gurudumu, Oct 23, 2010.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nina miaka mingi tangu nilipokwenda kanisani kusali tofauti na kusindikiza maharusi. Mimi hupinga ulokole kwa sababu ni brainwashing na haina tofauti na uganga wa kienyeji.

  Lakini kuna wakati nasikiliza mahubiri ya walokole kwenye tv. Baada ya muda sasa nimegundua yafuatayo;

  1. Kuna wahubiri ambao wanaigiza, wanapiga kelele hovyo hovyo

  2. Kuna wahubiri wanahubiri chuki dhidi ya wenzao na hawa hawana mantiki

  3.kuna wahubiri wanaosoma biblia peke yake, inawezekana hata magazeti hawasomi hivyo wana uchambuzi mwembamba sana kuhusu maisha na utawala wa nchi

  4. Kuna kakobe peke yake, anasoma tafiti na nadharia nyingi na anachambua mambo kwa upana sana. Anajua sana kupangilia hoja kimamtiki. Lakini mwisho humalizia na vile vitendo vya uganga wa kienyeji - majini, maradhi, ajira, kutozaa, n.k

  tangu wiki mbili zilizopita kakobe amekuwa akitoa elimu pana sana ya uraia kusaidia upigaji kura kwa kuchambua hoja badala ya kushabikia.

  Ndiyo maana nasema askofu kakobe Jana Leo na kesho. Naomba aendelee hadi siku ya tarehe 30 October. Anatoa elimu pana yenye mantiki zisizo na ukakasi. Anafanya kazi waliyoshindwa NEC na TAKUKURU. Jana na leo kapiga shule ya rushwa elimu ambayo inatoboa mfupa. Anatumia tv ya channel ten

  Asante askofu kakobe, anatoa mchango mkubwa sana kwa gharama kidogo wakati serikali inatumia mabilioni kwa taasisi ya rushwa ili isimamie na kuwalinda wala rushwa.

  Siyo kila kifanywacho na viongozi wa dini ni udini
   
 2. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Well said
   
 3. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Thanks
   
 4. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Gurudumu, hata mimi nimeona kwa wiki ya pili sasa Askofu anatoa elimu ya nguvu. Big up Bishop wetu:thumb:
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  namkubali.
  jamaa ni mshindi kwa ushawiwshi.
  amefanya kazi nzuri kweli kweli
   
 6. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Kakobe ni mdini na opportunisty mfano mwaka 1995 alisema A.L Mrema ni chaguo la mungu na amepewa maono kuwa lazima atakuwa Rais wa Tanzania, Kakobe akaacha kazi ya kanisa akaingia kwenye siasa na kuzunguka na Mrema nchi nzima. Wote tunajua Mrema alishindwa vibaya na Kakobe hakusema kitu akanyamaza kimya. 2005 KaKOBE akasema JK ni chaguo la mungu na akashinda. Sasa anawahubiria waumini wake wampigie kura Dr Slaa.
  Binafsi naona si sahihi yeye kuwa direct kuwataka waumini mpigie mgombea fulani. Ambacho ]Kakobe na viongozi wa dini wa madhehebu yote walitakiwa kuhamasisha waumini wao kupiga kura kwa mgombea wanae muona anawafaa, kuwe very neutral and objective. Anavyofanya kakobe ni unaweza kutafasiriwa kama udini, ingawa 2005 alimtaka JK hapo tuseme alikuwa fanatic wa JK kwa sababu ya kutaja specifically mtu anaepaswa kuchaguliwa na waumini wake, vivyo hivyo baadhi ya mashekhe
   
 7. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Sasa tukasali jumamosi 30October ili jumapili ya 31October tupige kura TU..
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Kakobe ana elimu nzuri ya kuona mamboa kwa mapana yake, lakini ni opportunist na mbinafsi anayetafuta manufaa yake binafsi kwa kupitia migongo ya wafuasi wake.
   
 9. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  elimu ya uraia muhimu. lazima watu kujua thamani yao. big up askofu.
   
 10. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mnyonge mnyongeni, haki yake mpe
   
 11. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Guuud kakobe
   
 12. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Unakosimamia kunaeleweka. So wewe kusema yote haya mi sishangai.

  1.Si kweli kwamba Mrema alishindwa ... aliibiwa kura zake zote. Kama hutaki acha!

  2. Sijawahi kusikia akiwadirect waumini wake wamchague Dr, slaaa ... hizo ni conclusion zako based ktk mtizamo wako mfinyu wa kidini.

  3. unasema ni "opportunist" , kwa vipi? hategemei ruzuku kutoka serikalini na serikali haimpi msaada wowote, sasa ajikombe ili apate nini?
   
 13. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Yaani wewe kama unasema Mrema alishinda uchaguzi 1995 lakini akaibiwa kura ili Mkapa ashinde basi wewe si wakujibishana kwa hoja na mimi, saizi yako katika kujibishana ni watoto wa primary school na chekechea, period.
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Leo Lusekelo kamcrush Kakobe indirectly kwa kuondoa ibada Jpili ijayo kwa ajili ya uchaguzi akisema siasa ni mambo ya mpito ila Mungu ni wa milele
   
 15. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
   
 16. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Muhuni yule achana nae!#
   
 17. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Lusekelo anatakiwa pia kutambua tarehe 31 kila mtu aache shughuli zake zote za maana akapige kura. Kura hupigwa Mara moja tu kila baada ya miaka 5, wanasema mungu yuko popote hata kwenye foleni ya kupiga kura unaweza kumwomba
   
 18. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hapo nakuunga mkono asilimia mia moja na huyu baba anafaa kuwa mwalimu pia maana anajua kufundisha sana somo la uraia
   
Loading...