Askofu Kakobe ataja vyama vya Kufutwa.

Status
Not open for further replies.
Askofu Kakobe ataja vyama vya Kufutwa.

Askofu Mkuu wa Kanisa la
Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe, amezitaka mamlaka zinazohusika kuvifuta vyama vyote vya siasa vinavyoendeshwa kwa misingi ya ukabila havivurugi nchi.

Askofu Kakobe, amezungumza Kanisa kwake hivi karibuni kwenye ibada ya sikukuu ya Krismas alisema miaka kadhaa iliyopita nchi haikuwa akiandamwa na vitendo vya ukabila tofauti na sasa ambapo hali imekuwa mbaya.

Alisema kuna baadhi ya vyama vya siasa nchini ambavyo kwa kipindi kirefu kimejulikana kuwa vinendeshwa kikabila tofauti na sasa ambapo hali imekuwa mbaya.

Alisema kuna baadhi ya vyama nya siasa nchini ambavyo kwa kipindi kirefu vimeendeshwa kikabila, jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.

Askofu Kakobe, alizishauri mamlaka zinazohusika kuvifuatilia vyama hivyo kuvifuta katika orodha ya vyama vya siasa kwani ni hatari katika mustakabadhi wan chi na wananchi wake.

Akizungumza suala zima la uongozi wanachi, hususani kitendo cha mawaziri kadhaa kuondolewa katika nyadhifa zao, alisema ubovu wa viongozi unachangia na mfumo wa kuteua viongozi.

Askofu Kakobe alisema kwa kawaida uongozi ni kipaji, hivyo watu wanapoona kunakuwa na viongozi wasiowajibika kikamilifu, wajue kuwa kuna tatizo katika uteuzi wao. Moja ya tatizo kubwa linaloathiri nchi kwa sasa alisema ni kuchagua watu kwa kuangalia maenao wanayotoka.

R.I.P chacha wangwe
 
Kakobe ameludia tu Yale ya Marehemu Chacha Wangwe juu ya Ukabila na Ukanda lakini kasahau Ufisadi wa ndani kwa ndani ya Chama .
 
Watu kama KAKOBE, GWAJIMA, MAMA RWAKATARE, MTIKILA And the likes ni wapiga dili wa hapa mjin. Amesoma nyakati kuna FURSA kaiona tuwavumilie tu.
 
Hivi kweli Zito angelikuwa amepokea pesa yote hii angelikuwa Tajiri sana angelikuwa na vitega uchumi Kama Mbowe lakini Maisha yake hayaashirii Kuwa na pesa nyingi hv !
 
Kakobe anatafuta pa kutokea kama si hivyo ni njaa inamsumbua, katika wachungaji wenye dhambi katika nchi hii huyu anaongoza kwani akiwa kanisani upokonya fedha na pete na mikufu ya thamani ya waumini kwa kuwarubuni kwa kupitia USHIRIKINA wake na ni vema wewe mjumbe wake ebu tuambie tunasikia yupo kwenye kundi la imani ya FREEMASON(ILLUMINANT) je ni kweli?

Toa ushahidi mzee, kinyume na hapo wewe ni mjinga sana!!
 
Askofu Kakobe ataja vyama vya Kufutwa.

Askofu Mkuu wa Kanisa la
Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe, amezitaka mamlaka zinazohusika kuvifuta vyama vyote vya siasa vinavyoendeshwa kwa misingi ya ukabila havivurugi nchi.

Askofu Kakobe, amezungumza Kanisa kwake hivi karibuni kwenye ibada ya sikukuu ya Krismas alisema miaka kadhaa iliyopita nchi haikuwa akiandamwa na vitendo vya ukabila tofauti na sasa ambapo hali imekuwa mbaya.

Alisema kuna baadhi ya vyama vya siasa nchini ambavyo kwa kipindi kirefu kimejulikana kuwa vinendeshwa kikabila tofauti na sasa ambapo hali imekuwa mbaya.

Alisema kuna baadhi ya vyama nya siasa nchini ambavyo kwa kipindi kirefu vimeendeshwa kikabila, jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.

Askofu Kakobe, alizishauri mamlaka zinazohusika kuvifuatilia vyama hivyo kuvifuta katika orodha ya vyama vya siasa kwani ni hatari katika mustakabadhi wan chi na wananchi wake.

Akizungumza suala zima la uongozi wanachi, hususani kitendo cha mawaziri kadhaa kuondolewa katika nyadhifa zao, alisema ubovu wa viongozi unachangia na mfumo wa kuteua viongozi.

Askofu Kakobe alisema kwa kawaida uongozi ni kipaji, hivyo watu wanapoona kunakuwa na viongozi wasiowajibika kikamilifu, wajue kuwa kuna tatizo katika uteuzi wao. Moja ya tatizo kubwa linaloathiri nchi kwa sasa alisema ni kuchagua watu kwa kuangalia maenao wanayotoka.

Mimi nakupongeza kwa jinsi ulivyofanikiwa kuwadanganya wajinga humu ambao wanaweza kuwa wepesi wa kuchangia mada bila kufuatilia .
Ni dhahiri kwamba sisi tunaofuatilia mambo ya siasa tulipata mapema CD ya mahubili yote ya Askofu kakobe na wengine ambayo ilishaletwa humu ndani kabla hata wewe hujaleta ujinga huu.

Mimi nilikuwa najiuliza ni kwa nini CCM makao Makuu wamekuwa wanafuatilia sana ile CD sasa nimepata jibu kuwa walikuwa wanatafuta namna ya kuwapata Wajinga wasiofuatilia Mambo na kuteka hoja zao kwa mambo mepesi.

Nina uhakika wewe umetumwa au umejituma ili upate kupeleta tathimini kwa waliokutuma.
Ungekuwa hujatumwa unge elezea Mambo yalivyo katika CD hiyo ambayo ipo kwenye Youtube kwa Kichwa cha Salamu za Chrimas 2012 za askofu kakobe.

Amekoso Serikali ya Kikwete katika mambo yalijiri Mwaka 2013 na kupengeza mambo ya kikwete katika Mwaka huo huo.
CD n yamasaa mawili lakini kwa wewe ulivyotumwa umeamua kupindisha kweli na kuleta ujinga!!
Kwa kuwa hiyo ndo kazi ya Shetani ndio maana nimekupongeza kwa upotoshaji mkubwa lakini kumbika mshahara wa dhambi ni mauti.

Akina Clement Mabina walikuwa majambazi wakubwa na kufanya uongo kama wako yalikini Mungu amejitenga na uongo!!
Upatapo ujumbe huu kumbuka ulipokosea baada ya kupokea mshahara wa uongo ili unyoshe sawa sawa na CD inavyosema vinginevyo utahukumiwa na na watu wataosoma ukweli uliopo!!!
 
Moderator, mtu huyu aliyeweka thread hii hapa, ni mwongo na mpotoshaji mkubwa. Ameupotosha ujumbe uliotolewa na Askofu Kakobe wakati wa Christmas, kwa maslahi yake. Baada tu ya Christmas, thread iliwekwa hapa iliyohusiana na ujumbe wake. Angalia thread hii hapa:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...acheni-siasa-za-chumbani-siasa-za-haramu.html

WanaJF, Askofu Kakobe si wa kihivyo. Msiweke michango hapa inayotokana na upotoshaji huu, chukueni muda ninyi wenyewe kusikiliza ujumbe wote alioutoa Askofu Kakobe wakati wa Christmas (Full unedited Version), ili mjue upotoshaji wa mtu huyu. Sikilizeni ujumbe wote hapa:

Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom