Askofu Kakobe ataja vyama vya Kufutwa.

Askofu Kakobe ataja vyama vya Kufutwa.

Status
Not open for further replies.
Naona unatumia akiri ya kuazima mwenzio aliitumia akaichoka wewe bada unaiona mali
Hata Yesu au Mtume Mohamad wakija hapa duniani na kusema hiki Chama Viongozi wake hawafai kabisa ni wachafu kwa jinsi ninavyowajua mtamkejeli hata Yesu au Mtume Mohamad huku mkiwa tayari kuwatetea akina Mbowe kwa nguvu zote!!!
 
Ndg,mchungaji...Siasa huziwezi,ongoza kondoo wako tu kwa njia zako za ki-Nigeria!

Nahisi huipendi nchi yako maana hilo ndilo tumaini la watanzania maskini na wenye maisha magumu.

Ambao kodi,migodi na rasilimali zao zimetumika na zinatumika na wakoloni uchwara na weusi wenye roho ngumu za dhuruma na mauaji!
 
Mbona ht mtoto wa miaka miwili anaelewa kabisa kuwa ni chadema inasemwa hapa
Mboa cdm uongozi wake umetoka kona zote za nchi?Mnyika wa Mwanza,Slaa wa Arusha,Mbowe wa Kilimanjaro,Tundu Lisu wa Singida,Msigwa wa Iringa,Sugu wa Mbeya,Halima Wa Dar,Wenje wa Mwanza.Ebu acheni ujinga mna mdangaya nani?Hizo propaganda za Kitoto na za zamani sana.Mbona husemi CUF ambayo kila kiongozi ni Muislamu hata ukiona ina nguvu sehemu ujue pana waislamu mahali hapo
 
Hapana, nimesikia yote hiyo... Mkisema CHADEMA inaendeshwa kwa misingi ya dini hayo ni maoni yako tu, then ifutwe. alizungumza vitu vingi sana siku ile. ni vyema usikilize mwenyewe. kama ni little perception au unaongelea kichama then ni rahisi kutumia hiyo kuleta hoja tofauti, maana hata swa la kuangalia elimu alisema halina umuhimu, zaidi ni kipaji ndio iwe kipaumbele. sasa hilo si iko in favor ya Chadema kwa sababu ya mwenyekiti wake????? tusipoteze maana zaidi ya kutumia vizuri elimu tunayopewa....
sikiliza link hii
Salaam za Christmas 2013 za Askofu Zachary Kakobe - YouTube
 
Hivi Kakobe ni nani na yuko wapi? Mara ya mwisho nilimwona mwaka 1979 akiwa mtumishi wa Moses Kulola.
 
Nilikuwa namheshimu sana Askofu Kakobe kama A man of God na mtu mzalendo.

Lakini leo natangaza rasmi kutomuani tena, Ninaomba arudi madhabahuni akatubu kwa hii dhambi ya kusaliti na kuhaini harakati za ukombozi.
 
serikali inahitajika kuheshimu na kutii sauti ya Mungu hiyo kupitia mchungaji wake Kakobe.
Kifuteni CHADEMA hiyo ndio sauti ya Mungu.

Hangaikeni kuifuta CDM kwenye makaratasi yenu lakini kumbukeni kuwa watu watabaki na CDM yao kwenye mioyo yao
 
Askofu Kakobe ataja vyama vya Kufutwa. Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe, amezitaka mamlaka zinazohusika kuvifuta vyama vyote vya siasa vinavyoendeshwa kwa misingi ya ukabila havivurugi nchi. Askofu Kakobe, amezungumza Kanisa kwake hivi karibuni kwenye ibada ya sikukuu ya Krismas alisema miaka kadhaa iliyopita nchi haikuwa akiandamwa na vitendo vya ukabila tofauti na sasa ambapo hali imekuwa mbaya. Alisema kuna baadhi ya vyama vya siasa nchini ambavyo kwa kipindi kirefu kimejulikana kuwa vinendeshwa kikabila tofauti na sasa ambapo hali imekuwa mbaya. Alisema kuna baadhi ya vyama nya siasa nchini ambavyo kwa kipindi kirefu vimeendeshwa kikabila, jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi. Askofu Kakobe, alizishauri mamlaka zinazohusika kuvifuatilia vyama hivyo kuvifuta katika orodha ya vyama vya siasa kwani ni hatari katika mustakabadhi wan chi na wananchi wake. Akizungumza suala zima la uongozi wanachi, hususani kitendo cha mawaziri kadhaa kuondolewa katika nyadhifa zao, alisema ubovu wa viongozi unachangia na mfumo wa kuteua viongozi. Askofu Kakobe alisema kwa kawaida uongozi ni kipaji, hivyo watu wanapoona kunakuwa na viongozi wasiowajibika kikamilifu, wajue kuwa kuna tatizo katika uteuzi wao. Moja ya tatizo kubwa linaloathiri nchi kwa sasa alisema ni kuchagua watu kwa kuangalia maenao wanayotoka.
Nina wasiwasi na mleta uzi kama kweli yalisemwa hayo.Mbona x-mass imepita muda mrefu alikuwa wapi?Mzushi huyu ange fungiwa humu JF kidogo.Aliipata wapi anasali pale?Ni mchonganishi tu.Haiwezekani mbona hotuba yake iliwekwa humu tuka ichangia yote.
 
Hivi Kakobe ni nani na yuko wapi? Mara ya mwisho nilimwona mwaka 1979 akiwa mtumishi wa Moses Kulola.

Mkuu Kakobe kajidhalilisha sana leo, ni heri angefanya dhambi ya uzinzi angesamehewa kuliko kufanya hii dhambi la kusaliti harakati za ukombozi.
 
acha unafiki , hii umeifinyanga wewe mwenyewe na ilishaletwa humu kwa urefu sana , hebu tuwekee hotuba yote tujisomee wenyewe .
 
angalia unasema habari zisizokuwa na ushahidi, utachapwa na mungu na hautaamini machoni mwako, kama huna cha kusema kaa kimya, watu wa mungu uwezi kuwatukana kama mnavyofanya kwa kina zito

Acha kutuletea ujinga hapa hapo kwenye RED unaposema ni watu wa mungu unamaanisha nini? mimi pia ninayeyaandika haya ni mtu wa mungu kama wewe haujatokana na mungu ni wewe pekee na Tambua mchungaji anatakiwa ajikite katika mambo ya kuwahubiria waumini wake juu ya kumwamini yule wanayemuamini na aachane na mambo ya Siasa masuala ya Kabila na dini wapi na wapi CCM mmemnunua Lwakatale na kumpa Ubunge usio na maslahi kwa Taifa na huyu nae mmeishaanza kumrubuni, Msitarajie kama Kakobe anaweza kuwasaidia CCM ili wananchi wawe na imani na nyie, Pia huyu Kakobe ni vema angejikita kukemea hii biashara ya Madawa ya Kulevya kuliko haya anayoyafanya na hapa napata kuamini kuwa hawa viongozi wa dini wanahusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya kwani katika maongezi yote kwa waumini wao huwa madawa ya kulevya hawayapi kipaumbele kwa kuwa ni biashara yao.
 
Nilikuwa namheshimu sana Askofu Kakobe kama A man of God na mtu mzalendo. Lakini leo natangaza rasmi kutomuani tena, Ninaomba arudi madhabahuni akatubu kwa hii dhambi ya kusaliti na kuhaini harakati za ukombozi.
Mkuu usiwe mwepesi kuamimini kila kinacho andikwa humu nyingi ni propaganda.Walitaka ionekane Mtumishi wa Mungu haitaki cdm.Ni uzushi wa muweka uzi
 
acha unafiki , hii umeifinyanga wewe mwenyewe na ilishaletwa humu kwa urefu sana , hebu tuwekee hotuba yote tujisomee wenyewe .
Chama Chakavu na kizee ndio mwasisi wa ukabila, udini, uuzaji sembe mbovu, meremeta, ufisadi, kagoda, EPA, DIV5 ndio anachomaanisha!
By the way nimesikia kuwa kuna watu wamepigwa banned kuingia US eti ni kweli?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom