SI KWELI PreGE2025 Askofu Gwajima ameandika barua kuomba msamaha kwa Rais na Watanzania

SI KWELI PreGE2025 Askofu Gwajima ameandika barua kuomba msamaha kwa Rais na Watanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Askofu Gwajima MSamaha Julai 2, 025.jpg
 
Tunachokijua
Madai

Julai 30, 2025 iliibuka barua ikieleza kutoka kwa Askofu Josephat Gwajima ikiwa na kichwa kinachosomeka “YAH: OMBI LA MSAMAHA KWA WATANZANIA NA KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA”.

Barua hiyo inaendelea kwa kueleza Askofu Gwajima anaomba msamaha kwa matamshi yake aliyoyatoa na hivyo huenda yalileta chuki ama mpasuka na hivyo Watanzania, Waumini wake pamoja na Rais wamsamehe.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa barua ama taarifa hiyo haikutolewa wala kuandikwa na Askofu Josephat Gwajima.

Taarifa hiyo ni ya kughushi ambayo imeandikwa na hivyo kupotosha Umma juu ya msimamo wa Askofu huyo. Barua hiyo imekuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo ya kiundishi jambo linaloitofautisha taarifa hiyo na taarfa halisi zilizowahi kutolewa na Askofu Gwajima.

Aidha tumebaini pia, taarifa hiyo si halisi kwani inamtambulisha Gwajima kama mwanachama wa halmashauri kuu ya CCM (NEC), uhalisia ni kuwa (NEC) huwa haina wanachama bali huitwa wajumbe yaani Wajumbe/Mjumbe wa halamshauri kuu ya CCM Taifa (NEC).

Pia, Askofu Gwajima nafasi yake katika kanisa haitambuliwi kama mchungaji mkuu bali ni muanzilishi na Askofu mkuu wa makanisa ya ufufuo na uzima hivyo kujitambulisha kama mchungaji kwenye taarifa hiyo ni kuonesha kuwa ni ya kughushi.

Taarifa hiyo potoshi imetumia muonekano wa taarifa aliyoitoa Askofu Gwajima Julai 16 alipokuwa akieleza kuwa atazungumza na waandishi wa habari siku hiyo. Ambapo licha ya kughushi muoenekano huo ila bado imekuwa na mapungufu kama ilivyobainishwa hapo awali.

Taarifa hiyo pia haipo katika kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.
Kwa HIYO Ina maana, JAMAA kaona, kama noma na IWE nomaa.


Kwishaaaaaaa
 
Back
Top Bottom