Askofu Dkt. Shoo: Mbowe alikuwa mbunge wangu na nimekuwa naye karibu sijawahi kuona tabia ya ugaidi kwake, nitashangaa sana!

Askofu hayuko sahihi. Mbowe sio gaidi ila ni mtuhumiwa kwenye kesi ya ugaidi. Pia aelewe gaidi sio kibaka wa mtaani anaenyoa kiduku. Magaidi ni watu wasomi wasiojihusisha na mambo ya kipuuzi mtaani. Ni watu ambao wakiwa wanakamatwa utaona wanaonewa ila utaamini siku likitokea tukio. Askofu aache mahakama ifanye kazi yake. Serikali imefanya fair kumshtaki ili apate nafasi ya kujitetea na kujiondolea hizo tuhuma.
 
Askofu mkuu wa KKKT Dr Shoo amesema anamfahamu vizuri Freeman Mbowe ambaye amewahi pia kuwa mbunge wake na hakuwahi kuiona tabia ya ugaidi moyoni kwake, hivyo atashangaa sana kama Freeman ni gaidi

Askofu Shoo amesema haki itendeke katika kesi hii ambayo inafuatiliwa na watu wenye mapenzi mema duniani kote.

Dr Shoo amesema haya kwenye mazishi ya mama mkwe wa Freeman Mbowe amnapo aliongoza misa ya mazishi.

Mungu ni mwema wakati wote!
Mwambie akatoe ushahidi kwa korti.
 
Hii kesi ya Mbowe naona ni script tu..

Najiuliza swali la msingi Sabaya katika ile footage ya kuvamia hotelini kwa Mbowe na mitutu na bodyguards wakaishia kuwapiga walinzi wa hoteli na kuwatupa mbali.

Swali linakuja kama Freeman angekuwa gaidi , kwa aliyokuwa akifanya Sabaya sidhani kama huyo Dogo leo hii angekuwa anasurvive..
Mchezo mchafu wa kijinga kabisa
 
2890080_2865442_JamiiForums1550718452.jpg
 
Hata Mimi nakataa japo siyo Malaika..Ni Mbowe huyu ambaye ni daraja la mafanikio ya watu kibao( Kisiasa) jamani!!? Si angewawezesha tu hao mapema kuwa magaidi wakaripua hivyo visima Vya mafuta na kuua viongozi wa Nchi??!Tuanze ..01.Dr.Kabouru ,02.Dr.Slaa,03.Zitto Kabwe, 04..........
 
Hata sisi tungeshangaa endapo usingemtetea ndugu yako.

Shoo na vyombo vya dola nani mwenye jukumu la ulinzi na usalama? Nani huwa wanachunguza hayo mambo?

Huyu anaingilia mahakamani sasa.
Hicho mnachokilazimisha kukipata, mtakipata soon. Rejea maneno ya Mama "Polisi wanabambikia watu kesi"
 
Mungu akubariki shoo.

Atakufa mtu
Shoo mwenyewe amebakiza muda tu asepe hapa duniani.
Na sasa anakwepana na kifo kwa kuvaa barakoa sas yeye ndo atakie wengine wafe?
Moyo wa mtu anaujua mwenyewe.

Kama ndivyo basi shoo asseme kama yeye ndo alimshauli kutoka nje ya ndoa na mukya,
Na je kanisa linaruhusu hayo?
 
Hayo mambo magumu sana Askofu akae kimya aombe sheria itende haki... sisemi Mbowe gaidi na wala simtetei Mbowe..

Tabia za binadamu anazijua binadamu mwenyewe na Mungu mwenye tabia zake.....binafsi kuna watu ukiwaambia tabia zangu kwa maana ya dark side yangu..basi kuna watu wanaweza kukupiga au hata kuapia miungu yote ila tabia zangu nazijua mwenyewe na Mungu.... ukiambiwa fulani jambazi au malaya usibishe na wala usikubali jipe muda wa kupata uhalisia na ukweli wa jambo...
 
Kamanda Askofu Shoo, lina roho mbaya, mbaguzi wa dini na kikabili pia, sura lake baya kama roho lake.
 
Askofu mkuu wa KKKT Dr Shoo amesema anamfahamu vizuri Freeman Mbowe ambaye amewahi pia kuwa mbunge wake na hakuwahi kuiona tabia ya ugaidi moyoni kwake, hivyo atashangaa sana kama Freeman ni gaidi

Askofu Shoo amesema haki itendeke katika kesi hii ambayo inafuatiliwa na watu wenye mapenzi mema duniani kote.

Dr Shoo amesema haya kwenye mazishi ya mama mkwe wa Freeman Mbowe amnapo aliongoza misa ya mazishi.

Mungu ni mwema wakati wote!
Magaidi wengi huwa wana tabia ya kutofahamika na huwa huwezi kudhani. Lazima afwate utaratibu wa kisheria. Sio kwa vile yeye anamfahamu ndio tuchukulie kuwa hana makosa.
 
Kuna watu wanaugulia mioyoni mwao kwaajili ya swala la Mboe.

Askofu ameona atoe dukuduku yeye kama mshauri au mwananchi wa kawaida au kuongozi.
 
Anaingilia uhuru wa mahakama! Sheria zinasemaje kuhusu hili?!(nimesoma title ya Uzi tu)
 
Back
Top Bottom