Askofu Dkt. Shoo: Mbowe alikuwa mbunge wangu na nimekuwa naye karibu sijawahi kuona tabia ya ugaidi kwake, nitashangaa sana!

Askofu mkuu wa KKKT Dr Shoo amesema anamfahamu vizuri Freeman Mbowe ambaye amewahi pia kuwa mbunge wake na hakuwahi kuiona tabia ya ugaidi moyoni kwake, hivyo atashangaa sana kama Freeman ni gaidi...
Hivi mtu kuwa mbunge wako tayari kunakufanya uwe karibu na mbunge huyo kiasi kwamba ufahamu hata uwezekano wa mtu kuwa gaidi?

Naona Askofu ameparamia mambo na kuanza kutetea vitu ambavyo ni wale tu waliokuwa wakishirikiana katika mipango hiyo ndiyo wanaweza kufahamu ukweli.

Wengine tukae kimya mpaka mambo yatakapothibitishwa au yatakaposhindikana kuthibitishwa ndiyo tushangae kwamba mambo yalikuwa hivo.
 
MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Askofu Dk. Fredrick Shoo amewaomba watu wote wanaojua kuomba waungane kumuomba Mungu ili yale yanayotendeka hapa nchini yatendeke Kwa haki na si Kwa kuonea watu.

Akizungumza katika ibada ya mazishi ya kumpumzisha mke wa Edwin Mtei, Johara Mtei nyumbani kwake Tengeru wilayani Arumeru, Dk. Shoo alitoa pole kwa mke wa Mbowe Lilian Mbowe Kwa kuondolewa na mama yake na kumtaka ajipe moyo hasa katika kipindi hiki ambacho mumewe ameshindwa kumzika mama mkwe wake sababu ya kesi ya ugaidi.

"Najua shauri la Mbowe lipo mahakamani naomba sana wale ambao wamepewa dhamana ya kutoa haki wakatende yake ambayo ni mapenzi ya mungu na haki ikasimame"alisema Askofu

Askofu Shoo alisema anashangaa kusikia Mbowe anashtakiwa Kwa ugaidi kwani Kuna wakati walipanga maandamano ya Ukuta viongozi wa dini walimwita Mbowe na kumshauri asiende barabarani Kwa kuwa damu za watu zitamwagika Jambo ambalo Mbowe alikubali kwa unyenyekevu kwa kusema hatapenda kuona damu za watu zikimwagika.

"Nitashangaa kama mbowe amebadilika na kuwa gaidi namfahamu Mbowe nikiwa Askofu wake na Mbunge wangu Jimbo la Hai, hakuwa na tabia hiyo naomba haki ituongoze, uzuie ulimi wako na mabaya, mambo ya kusingizia wengine ni mbaya Sana"alisema Dr Shoo

"Kibinadamu yanaumiza ukiona yanayotendeka mambo ya ajabu nchini maana Freeman Mbowe ameshindwa kumzika baba mdogo wake na mama mkwe hakika sisi tunaofuatilia mambo haya yanaumiza kibinadamu,"alisema

Alisema wale wanaoonewa ipo siku watamlilia mungu na sauti zao zitasikika na mungu atajibu maombi yao

"Ukiwa na mamlaka yoyote yatumie kwa kutenda haki na tuangalie yale tunayosema kweli na haki ,tusisingiziane uwongo,"alisema

Aidha alisema shauri la Mbowe lipo mahakamani hivyo aliomba wale wote waliopewa dhamana ya kutrnda haki wakatende haki na haki ikasimame.

Alisema mambo magumu na mazito ya kusingiziana vema yakazuiwa na kila mtu kupitia ndimi zao.

"Wapo watu mioyo yao inaugua hata bila kuwa na sehemu ya kusemea hivyo ili ipone lazima haki itendeke,sababu hata ukimuuliza kipofu hapa kuna haki yoyote inasikitisha,"alisema

Alisema pamoja watu wanasema siasa mchezo mchafu lakini vema watu wasifanye kupitiliza kwa sababu wapo watu watamlilia mungu na atajibu.

Aliomba watu watafute kufanya siasa za kistaarabu na kukaa katika maridhiano ambalo ndilo ombi lao siku zote.

Alimalizia kusema nchi ili ifanikiwe nilazima iweze kutenda haki sababu wapo watu wanaomba pale haki inapotoweka na Mungu hujibu.

Screenshot_20210825-102610_1.jpg
 
Hivi mtu kuwa mbunge wako tayari kunakufanya uwe karibu na mbunge huyo kiasi kwamba ufahamu hata uwezekano wa mtu kuwa gaidi? Naona Askofu ameparamia mambo na kuanza kutetea vitu ambavyo ni wale tu waliokuwa wakishirikiana katika mipango hiyo ndiyo wanaweza kufahamu ukweli. Wengine tukae kimya mpaka mambo yatakapothibitishwa au yatakaposhindikana kuthibitishwa ndiyo tushangae kwamba mambo yalikuwa hivo.
Mbunge na askofu wake ni lazima wawe karibu labda kama wewe siyo muumini.
 
Utetezi wa kijinga sana,rohoni kwa mtu ni mbali sana,askofu aache upuuzi,dola ina mkono mrefu sana
Dola la wizi wa kura na kubambikia wananchi wake kesi za kipuuzi, hata humu JF walitubambikia kesi, waoga kama makunguru
 
Lakini Huu ugaidi wa Mbowe Ni wa kusingiziwa tuu.Yaani Ni ugaidi gani Sasa ambao unaweza kuufanya kwa laki SITA ? Ati Mbowe aliwatumia watu sh laki 6 wakafanye ugaidi.Hakuna ugaidi wa kufanywa kwa Bei rahisi hivyo.Ugaidi unatumia mabilioni ya US DOLLARS.Kweli duniani Kuna Mambo.Dunia nzima inatucheka kwa hoja dhaifu Namna hii.Yaani Hapa Serikali inahujumu uchumi wake yenyewe.Inatumia mabilioni ya pesa za walipa Kodi kwenye case ya ugaidi wa shs laki 6 ya Mbowe.Hii Ni Ajabu Sana.
 
Wewe Shoo acha kuingilia mambo ya gaidi kwani wewe si Joyce Mkuya
Hata kama ni bangi au kete zinakusumbua jiangalie sana hivyo vi likes unavyopata hapo kwa kumdhihaki huyo kiongozi wa dini vitageuka laaanaa...
 
Ugaidi wenyewe ni kumpa mlinzi wake laki sita na kukutwa na risasi tatu za bastola. Bogus kabisa
Tena hiyo laki sita yenyewe leo katumiwa laki moja, baada ya siku mbili laki moja na nusu, siku nyingine laki mbili na nusu daah...
 
Mwambieni huyo Shoo aisome vizuri sheria ya Ugaidi ya mwaka 2002, apate picha kamili kuhusu Ugaidi ni kitu gani na makosa yake yakoje.

Kuna baadhi ya wapuuzi wanadhani bei ya kufadhili Ugaidi zimebandikwa ukutani kama Price tag zikiwa na bei tofauti tofauti, na kwamba ile bei inayoonekana ni kiwango cha chini eti bei hiyo haiwezi kufadhili Ugaidi. Je, huu si UNYUMBU.

Kuna mtu aliwahi kusema SUMU HAIONJWI, sijajua mantiki ilikuwa ni nini, but is it hard to guess?
Ni wakosefu wa akili pekee yao ndio wanaweza kuamini kwamba Mbowe ni gaidi, wapumbavu pekee yao otherwise wengi wanao comment kwamba Mbowe ni gaidi wana chuki either na Mbowe au chama chake, nje ya hapo ni wapumbavu tu ndio wanaweza kuamini hi case iliotengenezwa maabara
 
Askofu mkuu wa KKKT Dr Shoo amesema anamfahamu vizuri Freeman Mbowe ambaye amewahi pia kuwa mbunge wake na hakuwahi kuiona tabia ya ugaidi moyoni kwake, hivyo atashangaa sana kama Freeman ni gaidi

Askofu Shoo amesema haki itendeke katika kesi hii ambayo inafuatiliwa na watu wenye mapenzi mema duniani kote.

Dr Shoo amesema haya kwenye mazishi ya mama mkwe wa Freeman Mbowe amnapo aliongoza misa ya mazishi.

Mungu ni mwema wakati wote!
Hata yeye Askofu anaweza kuwa GAIDI kwakuwa magaidi wana camouflage ya hali ya juu!
 
Back
Top Bottom