Askofu Bagonza: Kuna kitu hakiko sawa

Askofu Bagonza: Kuna kitu hakiko sawa

Kama siyo mali ya serikali mbona zikiingia bidhaa sumu na kuua raia tunaipigia kelele serikali?

Get tour facts right guys...Serikali ni mlinzi namba moja wa afya yako hapa duniani...

Ndiyo maana tunapoenda kupiga kura kama raia tuelewe tunaenda kufanya nini...Hatuendi kishabiki tu au kutimiza ratiba...Tuna decide for our fate as a country!

Kuna shida kubwa naiona kwenye critical thinking ya watu wetu na hasa group la vijana...This is very serious, if we do not take it serious hii itatu cost huko mbeleni.
Nakubaliana na wewe kuwa Serikali inawajibu wa kulinda maisha ya raia wake dhidi ya adui yoyote yule, hata maradhi (Ibara ya 14 ya Katiba). Hata hivyo, hili halimuondolei raia wajibu wa kujilinda dhidi ya adui yoyote - kwa muktadha huu - maradhi.
 
Hili nalo neno, 'Tanzania si makao makuu ya Mungu'
Kama Israel ambalo ni Taifa teule la Mungu Corona inatesa, seuze Tanzania nji ya Jiwe.....!!!!!
Corona is there to stay! It's now one of the silent killer disease...!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Bagonza arudi kwao Lwanda asitumbue,sisi Watanzania tumeisha zoea maisha yetu,atuache na korona yetu.Mtumishi gani anayeogopa korona kiasi hiki?baada ya kuwaondoa watu hofu yeye anawajaza watu hofu, mtumishi anafanye fanya kazi na ibrisi.asome( Isaya 35:5)
CORONA BADO IPO DUNIANI

Kufuatia taharuki inayotokana na vifo kadhaa mwishoni na mwanzoni mwa mwaka hapa Karagwe, watu wengi wamekuwa wanapiga simu kwangu na kwa uongozi wa hospitali teule ya Nyakahanga kuulizia kulikoni? Jibu hili litoshe kusaidia kujibu maswali hayo:

1. Corona BADO iko duniani. Tanzania ni sehemu ya dunia. Malizia sehemu inayobaki. Maswali yaliyobaki waulizeni wenye dhamana na masuala ya Afya ngazi ya Mkoa na Wilaya.

2. Tanzania si makao makuu ya Mungu. Yeye ni wa wakati wote na wa mahali pote. Mahali alipo, Corona yaweza kuwapo pia. Wenye dhambi na watakatifu wote wanaugua na kufa. Makutano yetu ni ufufuko.

3. Uhai tulio nao si mali ya serikali wala ya dini yoyote. Tuna wajibu wa kuulinda. Tuchukue tahadhari zote bila kusubiri maagizo ya serikali au ya dini. Nawa mikono, tumia barakoa, jiepushe na mikusanyiko, nyungu haizuiwi na tiba mbadala nyingine hazizuiwi. Ramli ni marufuku hospitalini.

4. Kama si lazima usiende hospitalini kutembea. Kama si lazima tibiwa nyumbani kwako. Kama si lazima usizushe kuwa una ugonjwa ambao haujathibitishwa kwa vipimo.

5. Tunapakana na nchi zilizojitangaza kuwa zina maambukizi makubwa ya Corona. Majirani wema huzaa watoto wanaofanana kwa sababu ya kuhusiana vizuri. Hii ni vita, ujirani uchukue viwango vipya.

6. Idadi ya wagonjwa wenye matatizo ya kupumua imeongezeka ndani ya muda mfupi. Yawezekana ni uchovu wa mwisho wa mwaka! Idadi ya mitungi ya Oksijeni tuliyo nayo ni ndogo. Wasamaria wema wanakaribishwa kusaidia mitungi zaidi. Siasa safi ni kujitolea mitungi zaidi ili wenye shida ya kupumua wasaidiwe. Karibuni.

Kwa nia njema na kwa mapenzi makubwa kwa watu nilioagizwa kuwachunga na kuwalisha.
 
Akili mkichwa Mkuu corona ipo sana tu na inaondoka na Watanzania wengi kila leo. Anayedai corona haipo kaikimbia Dodoma for more than a week now kwani kule inachakata tena bila huruma. Je, huko chato atajificha dhidi ya corona hadi lini? Itakuwa ni miezi miwili tena kama 2020?

Kama Israel ambalo ni Taifa teule la Mungu Corona inatesa, seuze Tanzania nji ya Jiwe.....!!!!!
Corona is there to stay! It's now one of the silent killer disease...!
 
Nakubaliana na wewe kuwa Serikali inawajibu wa kulinda maisha ya raia wake dhidi ya adui yoyote yule, hata maradhi (Ibara ya 14 ya Katiba). Hata hivyo, hili halimuondolei raia wajibu wa kujilinda dhidi ya adui yoyote - kwa muktadha huu - maradhi.
Nashukuru kulitambua hilo, ahsante...
 
CORONA BADO IPO DUNIANI

Kufuatia taharuki inayotokana na vifo kadhaa mwishoni na mwanzoni mwa mwaka hapa Karagwe, watu wengi wamekuwa wanapiga simu kwangu na kwa uongozi wa hospitali teule ya Nyakahanga kuulizia kulikoni? Jibu hili litoshe kusaidia kujibu maswali hayo:

1. Corona BADO iko duniani. Tanzania ni sehemu ya dunia. Malizia sehemu inayobaki. Maswali yaliyobaki waulizeni wenye dhamana na masuala ya Afya ngazi ya Mkoa na Wilaya.

2. Tanzania si makao makuu ya Mungu. Yeye ni wa wakati wote na wa mahali pote. Mahali alipo, Corona yaweza kuwapo pia. Wenye dhambi na watakatifu wote wanaugua na kufa. Makutano yetu ni ufufuko.

3. Uhai tulio nao si mali ya serikali wala ya dini yoyote. Tuna wajibu wa kuulinda. Tuchukue tahadhari zote bila kusubiri maagizo ya serikali au ya dini. Nawa mikono, tumia barakoa, jiepushe na mikusanyiko, nyungu haizuiwi na tiba mbadala nyingine hazizuiwi. Ramli ni marufuku hospitalini.

4. Kama si lazima usiende hospitalini kutembea. Kama si lazima tibiwa nyumbani kwako. Kama si lazima usizushe kuwa una ugonjwa ambao haujathibitishwa kwa vipimo.

5. Tunapakana na nchi zilizojitangaza kuwa zina maambukizi makubwa ya Corona. Majirani wema huzaa watoto wanaofanana kwa sababu ya kuhusiana vizuri. Hii ni vita, ujirani uchukue viwango vipya.

6. Idadi ya wagonjwa wenye matatizo ya kupumua imeongezeka ndani ya muda mfupi. Yawezekana ni uchovu wa mwisho wa mwaka! Idadi ya mitungi ya Oksijeni tuliyo nayo ni ndogo. Wasamaria wema wanakaribishwa kusaidia mitungi zaidi. Siasa safi ni kujitolea mitungi zaidi ili wenye shida ya kupumua wasaidiwe. Karibuni.

Kwa nia njema na kwa mapenzi makubwa kwa watu nilioagizwa kuwachunga na kuwalisha.
hiyo mitungi ya gesi tunaileta wapi?
 
Huyu jamaa thinking capacity yake ni ndogo sana anafikiri corona inaweza kuisha kabisa! Corona tutaishi nayo kama mafua tunavyoishi nayo.
Hatuwezi kukaa na kushindwa kufanya maisha ati kisa ugonjwa.
 
Kwani chanjo kuchoma ni lazima?

Chanjo itakuwa lazima huko mbele kwenye kusafiri lakini kwa Tanzania chanjo italinda wazee wetu bila hivyo tutapoteza wengi. Rafiki yangu mmoja Mama na Baba wote walipelekwa ICU Agha khan Mama kaweza kotoka lakini Baba hali mbaya sana na wanadaiwa milioni 50 mpaka sasa kwa ujumla. Agha khana wamekatazwa kusema wazi kuwa ni Corona lakini binafsi wanasema na hata kutumia dawa za majaribio za Corona. Hivyo hulazimishwi mtu lakini wasizuie wengine ambao tunaamini Mungu anatupenda kama Kenya, Uganda na Zambia
 
Hatuwezi kukaa na kushindwa kufanya maisha ati kisa ugonjwa.

Nani kasema tusifanye maisha? Anasama ukweli watu wameacha hata kunawa mikono na chanjo zikipatokana zitolewe usiri na kujidanganya sio mzuri
 
Chanjo itakuwa lazima huko mbele kwenye kusafiri lakini kwa Tanzania chanjo italinda wazee wetu bila hivyo tutapoteza wengi. Rafiki yangu mmoja Mama na Baba wote walipelekwa ICU Agha khan Mama kaweza kotoka lakini Baba hali mbaya sana na wanadaiwa milioni 50 mpaka sasa kwa ujumla. Agha khana wamekatazwa kusema wazi kuwa ni Corona lakini binafsi wanasema na hata kutumia dawa za majaribio za Corona. Hivyo hulazimishwi mtu lakini wasizuie wengine ambao tunaamini Mungu anatupenda kama Kenya, Uganda na Zambia
Kwahiyo itakuwa lazima kwa wenye kutaka kusafiri tu?
 
Hii ni uthibitisho wa wazi kuwa ASkofu Bagonza ni mpagani sio Mkristo

Corona na Mungu haviwezi kuwa mahali pamoja Mungu

Lipagani hili Askofu kwa hiyo hata mbinguni kwaweza kuwa na Corona?
Ukishachanganya dini na siasa matokeo yake ndio kama haya..anakufuru akidhani yupo sawa..huyu anaonekana anaitukuza corona kuliko Mungu..awaache waaminio basi.
 
Akili mkichwa Mkuu corona ipo sana tu na inaondoka na Watanzania wengi kila leo. Anayedai corona haipo kaikimbia Dodoma for more than a week now kwani kule inachakata tena bila huruma. Je, huko chato atajificha dhidi ya corona hadi lini? Itakuwa ni miezi miwili tena kama 2020?
Unatuchanganya..mara kakimbia corona..mara atajificha hadi lini.
 
Kwa wenye akili kubwa wanaelewa, wewe endelea kujichanganya na usiwasemee wengine. Mimi sikuwa chanzo cha wewe kuukimbia umande.

Askofu anafeli sana mahali pengine, afu huyu askofu ndio aje aseme Mungu alipasua bahari ya shamu NITAKATAA
 
Hii ni uthibitisho wa wazi kuwa ASkofu Bagonza ni mpagani sio Mkristo

Corona na Mungu haviwezi kuwa mahali pamoja Mungu

Lipagani hili Askofu kwa hiyo hata mbinguni kwaweza kuwa na Corona?

Kiukweli ameyumba sanaa kwa hili

Huyu Askofu ndio aje kunifundisha kwamba wakati wa Israeli damu iliyopakwa kwenye nyumba za israel hakuna aliekufa na walikua sehemu ya Misri
 
Kwa wenye akili kubwa wanaelewa, wewe endelea kujichanganya na usiwasemee wengine. Mimi sikuwa chanzo cha wewe kuukimbia umande.
Jifunze kufikiri kabla ya kuandika..punguza mihemko ya kisiasa.
 
Wakati wa kampeni mlikuwa mnasifia watu kujaa kwenye mikutano ya kampeni na watu hawakuwa wakichukua tahadhari zozote za kujikinga na corona,hatukuwa tukiwasikia kuwatahadharisha hao watu japo wavae barakoa ila sasa mnakuja kusema et matatizo ya kushindwa kupumua yameongezeka,et corona ipo chukua tahadhari kana kwamba kipindi cha kampeni corona ilipumzika na ndio maana hamkuwa mkiwaambia watu wachukue tahadhari maana corona ipo.
Na walikuwa wanafanya kampeni za mitandaoni watu wajae kwenye mikutano..wabongo bwana.
 
Hakuna Corona Tanzania nyie. Big up Mh. JPM kwa kusimama imara na kutoyumbishwa. Msitutisheeeeeee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom