Sanyambila
JF-Expert Member
- Jan 24, 2018
- 339
- 457
Na Askofu Bagonza
1. Rushwa
Rushwa bandarini ndiyo imesababisha bandari ifanywe inachofanyiwa. Wakiishapeana rushwa, serikali inakosa mapato, mizigo inachelewa, inapotea, na bandari limekuwa pango la majizi.
Swali ni je, kila penye rushwa tuuze? Tubinafsishe? Tukabidhi sekta binafsi?
2 . Umoja na Utaifa
Mjadala umeonyesha, wanaodai wanaujenga/kuutetea umoja na utaifa, ndio wanaubomoa. Wanaoonekana kuubomoa, ndio wanaujenga. Bandari imeujeruhi umoja na utaifa wetu. Hii ina gharama mbeleni. Tumejuana, tuishi kwa tahadhari.
3 . Udini na Siasa Zetu
Viongozi wetu wana dini zao. Sitamani kuchagua kiongozi asiye na dini. Tatizo tunalo viongozi wa dini. Tunawakosoa viongozi wa dini ileee na kupongeza wa dini zetu. Au tunanyamaza mpaka tupigwe sindano ya kupongeza badala ya kushauri.
Inapendeza kumkosoa na kumshauri kiongozi wa dini yako japo haizuiwi kumkosoa wa dini isiyo yako.
4. Ujuzi wa Sheria na Uchumi.
Ajabu Wanasheria walioongea tukaelewa ni wachache sana. Walio wengi ujanja wao unaishia Kisutu.
Wanauchumi wetu ujanja wao unaishia Kariakoo.
Mkataba huu hawauelewi na wakiuelewa hawatuelezi tukaelewa. Huu ni ufa wa hatari.
5. Bunge
Hili lingebinafsishwa kabla ya bandari. Walichoongea bungeni sicho wanachoongea mitaani na kwenye baa. Wanamdanganya rais kuwa wanamuunga mkono wakati wamebeba mishale ya kumwangamiza.
6. Serikali
Mjadala na tabia za watu vimeonyesha serikali hii si ya rais Samia hata kama kaiteua yeye. Hii ni mchanganyiko wa serikali zilizopita. Ina utii uliogawanyika - kiapo kimoja Chamwino na vingine huko makaburini, Msufini, na Butiama.
Serikali bila “Uwajibikaji wa pamoja” ni sawa na genge la wasela. Ufa huu unadai tuanze upya.
7 . Rushwa part 2.
Katika Mjadala wa Bandari tumesikia malalamiko ya rushwa za aina tatu: Wanaonufaika na uzembe wa bandari wakikazana kukwamisha mkataba;

8. Rais Wetu
Rais SSH ni wetu sote. Ni muhimu kama taifa kumkinga na mipasuko inayotokana na mjadala huu. Kuna maisha baada ya mjadala wa bandari. Yeye analo jukumu la kutuongoza sote na makundi yote mpaka tuvuke. Subira itatufundisha kuliko haraka.
9 . Miafaka yetu
Mjadala huu umejeruhi miafaka yetu na kufukua baadhi ya makaburi. Baadhi ya makaburi tumekuta marehemu hawajaoza.
Katiba, maridhiano, Muungano, maelewano ya kidini, uhuru wa maoni na mamlaka ya wananchi bila bunge ni mambo muhimu sana katika kuziba nyufa.
10. Upinzani wetu
Mjadala unaonyesha aina mpya ya upinzani. Ndani ya chama tawala na serikali kuna upinzani mkali dhidi ya suala la bandari. Hii ni afya kwa nchi lakini hatari kwa utawala. Vyombo vyetu vijifunze kutotumia nguvu kupambana na maoni.
11. Bandari na Mipaka yetu
Bandari ya DSM ni mpaka kama ilivyo Tunduma, Namanga, Sirari, Mtukula na kwingineko. Kuharakisha mizigo bandarini wakati inaenda kukwama mipakani haisaidii. Kero za barabarani na rushwa zake haziwezi kumalizwa na DP World.
Mipaka yetu yote inanuka kwa uzembe, rushwa na ufisadi. Tusisafishe uso (bandari ya DsM) tukasahau makalio (mipaka mingine inayokwamisha mizigo ya nchi za jirani)
Nawashukuru wooote wanaochangia kwa hoja na kutuelimisha tulio wajinga wa sheria, uchumi na mikataba ya kimataifa
Chawa sijui watajibu hoja gani? Zaidi ya matusi tu