Ndugu wana JF wakati Kanisa linajiandaa na mapambano dhifi ya Ufisani wakristo wa Jimbo Katoliki Mwanza wame ondokewa na Askofu wao Mhashamu Mayalaa.Mayala atakumbukwa kwa uchapaji wake wa kazi nakuweka Elimu mbele , namkumbuka kuanzia niko kule Seminary wakati akiendesha majimbo 2 kwa wakati mmoja kabla ya Marehemu Samba. Mapadre wa Jimbo la Mwanza watamkumbuka kwa kuwa karibu nao na kusimamia kazi za kichungaji na maendeleo katika Jimbo la Mwanza .
Pole sana ndugu Pendo .Katika mazishi yake na hasa muda huu tutumie pia neno kufa kufaana maana masikio yote yatakuwa Mwanza msimo na mkazo wa Waraka kwa Nchi nzima uongezewe kasi .
Ahsante Mama Mdogo, sikumfahamu marehemu, wala kanisa lake. Waumini wa Kanisa Katoliki na Tanzania kwa ujumla hili ni pigo; Ajuae Bwana Mungu kwa mzima kuwa mfu, mgonjwa kuwa salama, leo tunawapa pole. Au hongera, maana ameenda kuliko bora zaidi.
Si lazima nijue kila kitu, kweli, na haiwezekani kabisa. Nani ajua yote zaidi ya Mwenye Enzi Mungu?
Lakini katika swala kama la kutangaza msiba sikuona ubaya wa kuuliza marehemu askofu wa jimbo la Mwanza alikuwa kanisa gani? Habari za kilio nilidhani tunataarifiana na tusiomjua marehemu tujumuike pamoja katika kipindi hiki kigumu. Sijui wanilaania nini.
Mungu Mtakatifu katika Jina la Yesu, ambaye alimuumba Mpendwa wetu Askofu Antony Mayala, hatimaye amemrudisha kwake.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.