Askari wale wa Jeshi, Makonda aliwatoa wapi?

Askari wale wa Jeshi, Makonda aliwatoa wapi?

Hii kolabo ya Chato na Kolomije inacheza mchezo hatari sana
Kuna hatari siku moja Kolomije ataingia vituo vya radio na 'jeshi lake 'na kutangaza kuanzia sasa yeye ndio BWANA MKUBWA
collabo LA chaka kwa chaka yaani Kama vile Chatu
 
Hawa ndio viongozi wa CCM. Wanao uwezo wa kukodi au hata kuunda vikundi vya kijeshi kwaajili ya kutekeleza uhalifu wanaotaka muda wowote na mahali popote.Binafsi siamini kama wale ni wanajeshi wa jeshi letu hili tunalolifahamu JWTZ lenye weledi mkubwa. Au labda Mwamunyange kastaafu.
 
Watz ktk ubora wao wa kujadili mada!

Naona kama wachangiaji mada ni wageni hapa tz maana hawajui kabisa nchi yao na mambo yake

Hawawajui hata aina majeshi ktk nchi yao ya tz aiseee!!

Tuna safari ndefu sana kufikia Maendeleo ya kweli
 
Wadau hebu msomeni huyu dabali T hapo # 42. Kaongea jambo na point ya maana sana. Cha ajabu kaandika herufi na maneno yanayo fanana na sauti yake dabali T.


Ni vizuri mtaala wa askari makirimakiri ukaboreshwa wasome somo la cctv na jinsi ya kuchukua tahadhari dhidi yake.




Na washawasha!
 
Wale sio wanajeshi, ni wale wa kaunda suti na wenyewe huwa wanavaa magwanda ya rangi ya kijivu. Ukipita pale makumbusho jaribu kuchungulia pale utawaona.

Sio wanajeshi mkuu ila si ndio hao wanalinda pale ikulu wanavaa hizo gwanda au??
 
Nafikiri ni wale wa usalama wa taifa ambao hulinda ikulu

Mkuu hebu nieleweshe kwanza wale wanaolinda ikulu ni askari wa aina gani maana zile gwanda sizijui bado au ndio hao wa usalama wa taifa??
 
Nina baba yangu asiye shindwa kamwee, Magu ni baba yangu asiye shindwa kamwee, simama imaraaa asiyeshindwa kamwee, nina babaaaaa. .....................!
 
Wale makirikiri ya mabaka mabaka ni tiss pale Kijitonyama wapo pale gate inn!! Ndio aliwachukua pale akamfuraishe sizonje aone shilawadu
 
Kuna wakati humu jF waliwananga sana majirani zetu kwa kilichotokea lango mangaribi hapo Kenya kwa askari wao walipo naswa na kamera.

Bahati yetu hawa makirimakiri wamefunzwa nidhamu ya hali ya juu na sio wadokozi vinginevyo tungekumbwa na aibu ileile ya jirani zetu.



Na washawasha!
 
Maswali:

1.Ukiacha askari Polisi wa kawaida,Mkuu wa Mkoa ana mandate na majeshi yetu?

2.Kama hana mandate,Wanajeshi wale alipewa kwa amri ya nani na kwa kazi gani?

3.Au Mkuu wa mkoa nyumbani kwake analindwa na wanajeshi na ndio hao siku ile aliamua kuambatana nao?

Naomba uchunguzi unaofanywa(kama ni uchunguzi kweli ni si geresha) uje na majibu kuhusu wale askari ilikuwaje wakafuatana na Makonda na taarifa ya uchunguzi ituambie kama wale si wanajeshi basi ni askari wa Jeshi gani la nchi hii au ni kutoka chombo gani cha ulinzi kinachotambulika kisheria hapa nchini.
Jeshi la mtu mmoja,,
 
Back
Top Bottom