Askari wa Polisi na JKT watwangana Tabora

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,595
Kumetokea mapambano makali muda huu na yangali yakiendelea. Mapambano hayo ni kati ya askari wa JWTZ na Polisi.

Mapigano hayo yalianza baada ya kusemekana kuwa wanajeshi walikuwa wanapiga raia ndipo polisi walipowasili a kuanza kuwafyatulia risasi ambapo wanajeshi walianza kujibu kwa mawe askari wakazidiwa na kupeleka askari zaidi eneo la tukio, kitu cha kushangaza raia nao wakaungana na wanajeshi.

Polisi ni wengi sana na wanazidi kumiminika kitu ambacho kimewatibua wanajeshi ambao wametangaza kurudi na kuwataka Polisi wakiwa wamekamilika wao ndiyo wanarudi kuanza. Shughuli zimesimama na maduka yamefungwa nitaendelea kuwapa updates.

SAHIHISHO:

Si askari wa JWTZ bali ni askari wa JKT ambao bado wapo depo katika purukushani hizo gari lilikuwa limebeba abiria lilipigwa risasi.
Sasa hivi wameshakamatwa wote kwa msaada wa JWTZ na wamejazwa kwenye toyota cruser mbili.
Doria inaendelea na hali inaanza kurudi kuwa shwari sasa hv naelekea central then kambini kujua kitakachojiri.
 
Haya ni mazito. Majeshi kuanza kupambana naona ndiyo tunaelekea mwanzo wa mwisho
 
Ni kweli mapigano makali yanaendelea maduka yamefungwa,mapigano yapo mtaa wa mwanza road barabara ya kuelekea urambo,hapa mjini Tabora hali ni mbaya
 
Consigliere said:
Polisi ni wengi sana na wanazidi kumiminika kitu ambacho kimewatibua wanajeshi ambao wametangaza kurudi na wamekamilika wao ndiyo wanarudi kuanza. Shughuli zimesimama na maduka yamefungwa nitaendelea kuwapa updates
Hapo kwenye bold ndo pahala ambapo sijakupata kaabisaa!
 
dishi dishuuuuuuuuu, nimekuwahi na wewe kufa, wakitoka hapo waelekee kivukoni ikulu wapindue nchi
 
Ni kama sijakusoma vile!
Hao JWTZ wamewapiga raia mitaa gani? Maana ninavyojua mji huo wa tabora ni mji ambao unaongoza kwa kuwa na makambi mengi ya jeshi, kwa maana kwamba kuna muingiliano mkubwa wa raia na wanajeshi.

Hebu fafanua kidogo mkuu.
 
Nasikia pia kuna uhaba wa mafuta huko. Walioko huko tujuzeni.
 
ninamaanisha askari Polisi.
Nashukuru,ila nilikuwa sijaelewa uliposema "kimewatibua wanajeshi ambao wametangaza kurudi, na wamekamilika,wao ndiyo wanarudi kuanza"

Ina maana vurugu zimesimama na sasa wanarudi kuzianzisha?

Ebu checki tena bandiko mkuu.

Kifupi naelewa umesema kuna ugomvi kati ya polisi na wanajeshi,ila sikukupata hapa....

Consigliere said:
kimewatibua wanajeshi ambao wametangaza kurudi na wamekamilika wao ndiyo wanarudi kuanza.
 
By the time ndiyo kwanza nilikuwa nafika Tabora na kuingia hotelini.
Hivyo story ni nyingi na tofauti kulingana ushabiki. Nilizozirusha ni za awali.
Habari zaidi kufata naona Sheikh wa Mkoa naye ndiyo anaingia hapa central.
 
Na hapo sijui watasema CDM ndio wanahusika?maana hawakawii kuropoka hawa magamba.
 
Ni kweli mapigano makali yanaendelea maduka yamefungwa,mapigano yapo mtaa wa mwanza road barabara ya kuelekea urambo,hapa mjini Tabora hali ni mbaya

Mkuu ni kama sikuamini vile.
Kwani wewe upo wapi, Tabora ama Mbeya?
Mbona unaonekana upo kwenye eneo la tukio katika matukio yote mawili?
Sikusomi mkuu.
 
Nitawajuza zaidi baada ya kurudi hotelini.....
Kwani hapa natumia simu
 
Back
Top Bottom