Askari Polisi Shinyanga,walificha gazeti la UHURU!

hao polisi wangeliacha tuu manake

sidhani kama kuna mtu mwenye akila yake timamu

anayelisoma labda kwenye ofisi za magamba hasa wale

wenye itikadi za Kimakamba
 
Wana JF,nipo safarini Shinyanga mjini. Kuna tangazo langu,lilitoka kwenye gazeti la Uhuru la jana 17/1/2012.Leo,nimelitafuta mji mzima gazeti hilo,nimelikosa. Naambiwa kuna gari la Polisi limezungukia sehemu zote,ziuzwazo magazeti,na kuyanunua yote! Sababu,naambiwa kuna tuhuma dhidi yao,imeandikwa humo!
JF,ni mtandao mpana. Naomba aliyelisoma,atujuze walichotuhumiwa. Na,je,walichokifanya,kitawasaidia? Ukizingatia,magazeti hayo yanapelekwa kila kona!
Nawasirisha!

Si rahisi gazeti la uhuru kuibua tuhuma za polisi, they are two side of the same coin
 
kwa nini Polisi walizikusanya? Kuna tuhuma dhidi yao? Kwa nini wasijirekebishe na waka acha madhambi?
 
Sio ajabu kwa Shinyanga kwani sasa hivi kuna kijana sadist kapewa U-RPC ,enjoyment yake kubwa ni kuvizia askari kuwapiga picha na kuwafukuza kazi,navyojua kiongozi ni mzazi anayepaswa ku-guide watoto wake na kuwaprotect,mzazi anayetega wanawe ili watumbukie ni joka la mdimu,sijui IGP kwa busara zake kama anasupport mambo ya huyu kijana.

Aaaaa!!! Dah!! Hili nalo jipya. Huyu RPC mbona ana hatari? Kwani nawe ni mmoja wa waliopigwa Picha? Funguka!
 
hili gazeti haliuzwi mahala popotekwani halina soko linasambazwa bure ofisi za serikali na za ccm.
unalitafutia promo ili kesho mkilijaribisha sokoni linunuliwe mmechemka wabongo wako macho.
 
Mtoa thread nami nina shaka nae,gazeti ile inasambazwa maofisini tu,tena ya serikali ikiwemo ofc ya RPC,mtaani hakua wanunuzi.jamaa anafanya Promo flani hivi c suala la kutoa tangazo wala nn
 
Uhuru si gzt la CCM na polisi?Kwa nini wanaficha

Duuuuuuuuuuu! Shangaa na ww! Hili gazeti la uhuru ni la CCM na siku zote hupenda kuvisifia vyombo vya serikali hata kama huwa vinafanya maujinga, Si uhuru peke yake kwani hata TBC nao ni akilio moja na gzt la UHURU.
 
hili gazeti haliuzwi mahala popotekwani halina soko linasambazwa bure ofisi za serikali na za ccm.
unalitafutia promo ili kesho mkilijaribisha sokoni linunuliwe mmechemka wabongo wako macho.

kumbe..!? Maana nape ni hatari sana!
 
Wana JF,nipo safarini Shinyanga mjini. Kuna tangazo langu,lilitoka kwenye gazeti la Uhuru la jana 17/1/2012.Leo,nimelitafuta mji mzima gazeti hilo,nimelikosa. Naambiwa kuna gari la Polisi limezungukia sehemu zote,ziuzwazo magazeti,na kuyanunua yote! Sababu,naambiwa kuna tuhuma dhidi yao,imeandikwa humo!
JF,ni mtandao mpana. Naomba aliyelisoma,atujuze walichotuhumiwa. Na,je,walichokifanya,kitawasaidia? Ukizingatia,magazeti hayo yanapelekwa kila kona!
Nawasirisha!

Bado unasoma gazeti la CCM?
 
Bado unasoma gazeti la CCM?

Sidhani mtu mwenye akili zake,na anajua uwezo wa waliomo humu,anaweza kuwaletea UJANJA WA NAMNA HIYO.
Nilikwisha sema kuwa,nilipeleka tangazo la kuitwa mahakamani,kwenye gazeti hilo! Katika kulitafuta,baada ya tangazo kutoka humo,ndio nikajua hilo!
Nawaheshimu sana wana JF! Najua kabisa,UJANJA UJANJA,hapa,haukatizi! Nilichokileta,ni kweli.
 
Naambiwa yanafika siku husika,mchana!
Nahangaika leo,kumbe yalifika jana,na waliyanunua jana hiyo hiyo!

Aisee afadhari ungeuliza kitu kingine,hilo ni gazeti la kufungia maandazi kawaulize wauza maandazi.
 
aisee afadhari ungeuliza kitu kingine,hilo ni gazeti la kufungia maandazi kawaulize wauza maandazi.

naona sikusomeka vizuri! Hoja yangu,ilikuwa polisi kuyanunua hayo magazeti yote,ili wasomaji wa shinyanga mjini,wasiisome habari iliyoandikwa,kuwatuhumu!
Hoja yangu ilikuwa,njia hiyo itawasaidia,wakati miji mingine yamesomwa?
Sikuhitaji kutafutiwa!
 
Wana JF,nipo safarini Shinyanga mjini. Kuna tangazo langu,lilitoka kwenye gazeti la Uhuru la jana 17/1/2012.Leo,nimelitafuta mji mzima gazeti hilo,nimelikosa. Naambiwa kuna gari la Polisi limezungukia sehemu zote,ziuzwazo magazeti,na kuyanunua yote! Sababu,naambiwa kuna tuhuma dhidi yao,imeandikwa humo!
JF,ni mtandao mpana. Naomba aliyelisoma,atujuze walichotuhumiwa. Na,je,walichokifanya,kitawasaidia? Ukizingatia,magazeti hayo yanapelekwa kila kona!
Nawasirisha!
Kuyanunua magazeti yote kwa lengo la kuwafanya watu wasipate habari, ni kosa dhidhi ya haki za kupata habari kadiri ya Katiba yetu ya sasa kifungu namba 18. Kumbe kama wamefanya hivyo na kwa lengo hilo basi ni makosa. Ninavyofahamu magazeti mengine yamepoteza mvuto kwa wasomaji, kumbe pengine mikoani zinaenda nakala chache sana na kama wewe ni mgeni maeneo hayo utakuta nakala zote zimeuzwa kwa wateja wao wa kila siku. Mwisho, watu hawaelewi hili kwamba " huwezi ukanyamazisha sauti za vyombo vya habari bali unaweza kuzikwepa ukiamua na kutaka!"
 
Nimefurahi nimeeleweka!!
 
Afadhali kutembea barabarani usome mabango ya matangazo ya biashara kuliko kusoma gzt uhuru
 
Ningekuwa mimi mhariri wa UHURU (nashukuru Mungu siyo) kesho ningeirudia habari hiyo na nakala zote ninpgezipeleka shinyanga maana soko ni kubwa.
 
Back
Top Bottom