Askari Polisi Shinyanga,walificha gazeti la UHURU!

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
4,344
6,403
Wana JF,nipo safarini Shinyanga mjini. Kuna tangazo langu,lilitoka kwenye gazeti la Uhuru la jana 17/1/2012.Leo,nimelitafuta mji mzima gazeti hilo,nimelikosa. Naambiwa kuna gari la Polisi limezungukia sehemu zote,ziuzwazo magazeti,na kuyanunua yote! Sababu,naambiwa kuna tuhuma dhidi yao,imeandikwa humo!
JF,ni mtandao mpana. Naomba aliyelisoma,atujuze walichotuhumiwa. Na,je,walichokifanya,kitawasaidia? Ukizingatia,magazeti hayo yanapelekwa kila kona!
Nawasirisha!
 
siku hizi magazeti yanafika shy kwa wakati?au bado halijafika usubiri kidogo!!!
 
Naambiwa yanafika siku husika,mchana!
Nahangaika leo,kumbe yalifika jana,na waliyanunua jana hiyo hiyo!

usihofu,naamini kuna wachache wanaweza kuwa wamelisoma.tuvute subira tutaletewa hapa hapa!!lakini kulificha gazeti ni sawa na kufukia moto kwa pumba!!
 
Hawa Polisi nao ndiyo wa kuwajadili humu. Inakuwaje wapoteze muda kuyazuwia yasisomwe? Kulikuwa na tuhuma za Rushwa Polisi wanataka kwa Madreva khs leseni. Lakini hiyo si ndio Polisi Jamii kuwaanika?
 
hivi bado kuna gazeti linaitwa "Uhuru". mbona silionagi naponunua magazeti?



Lipo!
Kuna mtu,kanitumia MSG,ananifahamisha kuwa,habari hiyo inahusu ULANGUZI wa leseni mpya! Heading yake inasomeka, "LESENI MPYA ZIMEKUWA BIASHARA SHINYANGA?".
Sijui ndani,wametuhumiwa nini zaidi!
 
Lipo!
Kuna mtu,kanitumia MSG,ananifahamisha kuwa,habari hiyo inahusu ULANGUZI wa leseni mpya! Heading yake inasomeka, "LESENI MPYA ZIMEKUWA BIASHARA SHINYANGA?".
Sijui ndani,wametuhumiwa nini zaidi!

Dah!! Si umeona? Yaleyalee. Mimi nilisikia tu wakati linasomwa Redioni asbh ile. Hatujui ndani kuna tuhuma zipi. Lakini Kichwa cha habari kinajieleza.
 
Wanajidanganya kwa kununua gazeti na kudhani taarifa hazitajulikana.
 
Sio ajabu kwa Shinyanga kwani sasa hivi kuna kijana sadist kapewa U-RPC ,enjoyment yake kubwa ni kuvizia askari kuwapiga picha na kuwafukuza kazi,navyojua kiongozi ni mzazi anayepaswa ku-guide watoto wake na kuwaprotect,mzazi anayetega wanawe ili watumbukie ni joka la mdimu,sijui IGP kwa busara zake kama anasupport mambo ya huyu kijana.
 
nenda pale nssf opposite na crdb lipo


Hapo,ndipo nilipo anzia. Binafsi,kuna mtu kaninunulia Mwanza.
Hoja iliyobaki,nani aimwage hapa tuione hiyo tuhuma wanaojaribu kuificha,ili sehemu husika,wasiisome?
 
Back
Top Bottom