Askari Auwawa na Majambazi Tazara

nikikumbuka polisi walivyo muua jirani yangu na wakadai ni bahati mbaya walihisi ni jambazi kumbe walitaka pesa zake zilizo kuwa kwenye gari sitaki hata kuwasikia majambazi haya yaliyo chini ya magamba.wafe waishe huwezi jua huyo polisi aliua wangapi


... Mkuu umenena' hiyo ni kweli kabisa.
Siku hizi Polisi makigudua kuwa una fedha nzuri unawekwa kwenye timing, then waripoti kuwa "RIJAMBAZI LA MUDA MREFU LIMEUAWA LIKIWA NA MENGINE' YAMETOROKA"
 
Hawa jamaa vifo wanavitafuta. Ni askari wa "TIGO" huwa wamejenga mazoea ya kujificha pale karibu na ofisi mpya za Zima moto Tazara Mchicha wakivizia kuwakamata wananchi hasa wenye Bodaboda ili wawatoe chochote.
 
askari nao wawe wanabeba risasi za kueleweka lirisasi zeee unakoki dakika tatu kwa nini ukistukizwa usishindwe. any way pole zao majeruhi
 
halafu unakuwa lindoni upoupo kama vile nchi hii ina amani sanaaaaa wana sahau kuwa tanzania ya leo sio ya jana.
kuna ujambazi, alshababu,uamsho na mengine mengi sasa ilitakiwa kuwa wakati wa doria za uhakika na si mchezo mchezo
 
R.I.P polisi uliyeuawa. lakini polisi wamezidi pia kuchunguza mpaka vitu ambavyo havifai, kwamfano juzi nimeshuhudia polisi wanamkata dada amepakiza vitu vyake kwenye pickup anahama kutoka nyumba moja kwenda nyingine kukwepa adha za mama mwenye nyumba, wakamwambia onyesha risiti ya vitu alivyopakia kwenye ile gari heb fikiria risiti ya vyombo vya ndani; godoro, sufuria vijiko kitanda..... utaipata wapi sa hizo? boring! nashuhudia polisi wakikamata mikokoteni kibao yenye mizigo eti onyesha risiti ya VAT, kwani TRA wameshindwa kazi yao? yani polisi pale kariakoo na vitongoji kadhaa vya dsm wamegeuka mgambo, uko na private car yako umefunga kibox cha kwa mfano kina nguo, sukari, mafuta unapeleka kutumia ubungo kuwatumia ndugu na jamaa wanakurukia onyesha risiti ya VAT tangu lini dukani kwa Mangi amenunua mashine ya risiti za Riz1? By the way sishabikii polisi kuuawa bt najaribu kueleza wajibu wao wanautekelezaje wanapotoka vituoni kuelekea mtaani-
 
hao majambazi wajinga kwanini wamewabakisha wengine,majambazi koko.r.i.p mwangosi
 
Unaona sasa, wao polisi wakiwakamata majambazi wanawachia sasa imekula kwao hii ni saaaaaaaafi ssaaaaaana. ninaposikia polisi kauawa na jambazi mimi huwa naona kama kawaida tu ila nikisikia jambazi wameua raia ukweli huwa nasikitika sana
 
Mimi nikiwaona polisi kwa kweli nakumbuka matukio yote hawa polisi wanayowafanyia wasio na hatia. halafu natamani ........
ila jambazi nao sio wazuri yani wote wabaya.
 
busara zako nikama vyoooo vya uwanjan, kaa mbali na wenye busara, hivi ulijiunga jf kwa ujinga huo?
 
Mimi nikiwaona polisi kwa kweli nakumbuka matukio yote hawa polisi wanayowafanyia wasio na hatia. halafu natamani ........
ila jambazi nao sio wazuri yani wote wabaya.

kuna wakati ni bora majambazi..ref. zombe kuli msituni
 
Hvi inakuwaje watu mnaotegemewa kuongoza nchi mnaleta marumbano ya kisiasa msibani? Mwenzetu kapoteza maisha, wengine majeruhi taabani hv mmekosa utu kiasi hicho? "Ee Mungu tuepushe na roho za kinyama waja wako." R.I.P kamanda, Mungu watazame majeruhi wetu. AMINA.
 
Back
Top Bottom