Askari Auwawa na Majambazi Tazara

Askari Auwawa na Majambazi Tazara

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
27,650
Reaction score
16,731
askari mmoja amepigwa risasi ya kichwa na kufariki hapohapo,na wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya kurushiana risas na majambazi

source
itv habari za lisaa
 
Askari ameuliwa na kitu kizito! R.I.P Askari....umekufa kiume ukiwa kazini kutulinda sisi raia! wewe ni shujaa umetoa maisha yako ili sisi wengine tuwe salama.naomba jeshi la polisi limsaidie mjane wa marehemu kama yupo.
 
Aliye eneo la tukio atujuze kwa kilefu, ili tujue wameiba/walitaka kuiba wapi na ilikuwaje mpaka polisi akauwawa na wengine kujeruhiwa. Na kwa aliyekufa "r.i.p"
 
Askari ameuliwa na kitu kizito! R.I.P Askari....umekufa kiume ukiwa kazini kutulinda sisi raia! wewe ni shujaa umetoa maisha yako ili sisi wengine tuwe salama.naomba jeshi la polisi limsaidie mjane wa marehemu kama yupo.

Mkuu Mgomba101, nimejikuta ninacheka maana inaelekea na wewe ni mtu wa 'system' eti sababu ya kifo ni kitu kizito! kama wanavyosemaga wenzetu kwenye jeshi la polisi!
 
Majambazi waliokuwa ndani ya gari aina ya Toyota Carina, mchana huu katika eneo la Tazara wamewarushia risasi askari polisi waliokuwa katika gari la doria. Majambazi hao walifanya hivyo walipodhani kuwa askari walikuwa wanawafatilia. Askari mmoja alipigwa risasi ya kichwa na kufumiliwa ubongo, na kufariki hapo hapo. Askari wawili wamekimbizwa hospitali ya Temeke ambapo mmoja yupo katika hali mbaya.

Majambazi hao walifanikiwa kutelekeza gari hiyo na kutoroka. Polisi wanaendelea kuwatafuta.
 
Asante kwa habari lkn kiswahili chako cha kipare au? LISAA ndio nini?
 
Niko Bukoba ila intelijensia imenieleza kuwa Askari polisi mmoja ametwangwa risasi maeneo ya Tazara Dar es Salaam. Alikuwa Doria na wengine wamejeruhiwa. Majambazi wanahusika na hili. Asanteni. Mlioko karibu tujuzeni zaidi
 
polisi bana.,wangewazidi nguvu majambazi wangesunda mshiko wote wa wizi..r.i.p afande
 
nimeisikia radio one muda sio mrefu. Yaani nimeruka ruka kwa furaha natamani wangewaua wote. Mimi nilijua wao hawafi!
 
Safi sana bora yafe, wanapenda sifa sana.... bado Mwema!
 
Hii nchi imewashinda viongozi wake.........hamna kuvumiliana tutachinjana mpaka mwisho
 
Si furahii kifo lakini naamini askari wa JK walikuwa na dili na hao majjambazi then wakageukana..Simnajua siku hizi ukikutana na jambazi ni afadhali kuliko ukutane na policcm!!!!Kwangu mimi ningeweza kuripoti Jambazi la serikari limeuwawa na jambazi la kujitegemea
 
Back
Top Bottom