R.I.P polisi uliyeuawa. lakini polisi wamezidi pia kuchunguza mpaka vitu ambavyo havifai, kwamfano juzi nimeshuhudia polisi wanamkata dada amepakiza vitu vyake kwenye pickup anahama kutoka nyumba moja kwenda nyingine kukwepa adha za mama mwenye nyumba, wakamwambia onyesha risiti ya vitu alivyopakia kwenye ile gari heb fikiria risiti ya vyombo vya ndani; godoro, sufuria vijiko kitanda..... utaipata wapi sa hizo? boring! nashuhudia polisi wakikamata mikokoteni kibao yenye mizigo eti onyesha risiti ya VAT, kwani TRA wameshindwa kazi yao? yani polisi pale kariakoo na vitongoji kadhaa vya dsm wamegeuka mgambo, uko na private car yako umefunga kibox cha kwa mfano kina nguo, sukari, mafuta unapeleka kutumia ubungo kuwatumia ndugu na jamaa wanakurukia onyesha risiti ya VAT tangu lini dukani kwa Mangi amenunua mashine ya risiti za Riz1? By the way sishabikii polisi kuuawa bt najaribu kueleza wajibu wao wanautekelezaje wanapotoka vituoni kuelekea mtaani-