Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,275
- 18,352
Habari wanabodi
Naomba niingie kwenye mada, kama ni mtumiaji wa barabara ya Mandela na mfuatiliaji wa mambo nyakati za jioni utagundua kuna jambo la kutengeneza.
Iko hivi, wakati unatoka Ubungo kwenda Tazara au kinyume chake, mara nyingi utakuta foleni imeanzia mbali sana hata Mwananchi, utasogea kidogo kidogo hadi Njia Panda Tabata na Buguruni Sheli kwa shida sana.
Sasa katika ufuatiliaji wangu nimebaini jambo kwa hawa askari trafiki, ikifika jioni wanajua magari ni mengi kwa sababu watu wanatoka makazini, askari wanajazana mitaa ya Buguruni Sheli hadi maeneo ya darajani wakisubiri gari linalotanua.
Kwa bahati mbaya daladala ndio hutanua sana kupita service road wanazikamata na kula chao ukibisha unaandikiwa. Fedha inayotolewa ni kuanzia Tsh.2,000 hadi 5,000. Kwa gari binafsi mtu anatoa hadi 10K kupunguza kucheleweshwa zaidi.
Kingine nilichobaini hawa askari wa Buguruni sheli wanaongea na Askari wa Tazara (Mfugale flyover) ili magari ya Mandela road yasiitwe badala yake wanaitwa magari ya Nyerere road kwenda au kutoka City center, na askari wa Buguruni wanaita zaidi magari yanayoelekea au kutoka Tabata na mengine yanayoenda au kutoka Ilala.
Huu mchezo inahitaji ufuatiliaji sana mpaka kuubaini kwa sababu ukifanikiwa kuvuka njia panda ya Tabata unakuta huku mbele kati ya Buguruni na Tazara ni kweupe na magari yanayokatiza sio mengi ni ya kuhesabu.
Sasa niziombe Mamlaka zinazosimamia hawa jamaa ziwaambie waache kutunyanyasa na wafanye kazi kwa haki, hii nchi ni yetu sote na tunalipa kodi.
Kila mmoja anayo njaa kwa kipimo chake lakini wasitufanyie hivi wanatuonea sana na wakati mwingine mtu una emergency lakini jamaa wanafanya kusudi wanakuweka wakijua kabisa ukishindwa kuvumilia utatanua service road watakukamata walambe chao.
Asanteni.