Askari ajiua kwa kujipiga Risasi Mdomoni

Askari ajiua kwa kujipiga Risasi Mdomoni

Nikiikumbuka video ya Lipumba hata sisikitiki sana
 
Bado RPC Mihayo wa Ruvuma, naye ana damu inayomilia. Anaweza kuishia hatua kama hiyo

damu gani na kwa tukio lipi? usilete kashfa isiyo na maana hapa nakusubiri ujibu vinginevyo ni uongo.
 
Ha Preta, umeolewa na POLISI? Basi na Wewe li-mme lako lijiue, tumechoka nayo haya!!

Kumbe unapenda niwe mjane eeeeh.........sikujua kama umenichoka hivyo........
 
Napata shida na hiyo picha. Ebu tutafakari kidogo. Wote tunajua namna hiyo bunduki ilivyokuwa na nguvu. Kama kweli alijipiga mwenyewe aliishikaje hiyo bunduki hadi imlalie hivyo kifuani. Mie najua bunduki ingeruka kule na yeye huku.

Lkn pia ebu tuchunguze kutokwa kwa damu. Mtu alijipiga risasi mdomoni tungeona kichwa kimefumuliwa na damu zimetapakaa. Napata wasi wasi kuwa hiyo bunduki kawekewa kifuani.

Napata wasi wasi. Angalia hiyo michulizi ya damu inatokea puani, risasi ilipita wapi hadi hiyo michirizi tena miwili na sio damu iliyotapakaa. Napata wasiwasi na hili.
 
Hii picha kwa kweli siamini kwa asilimia mia moja kuwa jamaa kajiua, mimi sio forensic photo reader lakini naona kuna makosa madogo wameyaacha, kuna kitu kinaitwa blood sparter eneo la mauaji, hapa hakuna.

Ukiangalia marehemu haiwezekani damu ikapanda juu, nilitegemea nione damu imeshuka na mto aliolalia umejaa damu, kwa short distance kama aliyotumia lazima risasi imetoka upande wa pili haiwezekani ikabakia kichwani, kama ingetokea upande wa pili obvious mto ungelowa damu sana.

Hata kwa instant death bukundi haiwezi kukaa hapo maana jamaa lazima atajinyonga kidogo labda kama alikuwa na roho ya mende. kama ningekuwa ni polisi ninayechunguza hii kitu nisingekubaliana na maelezo ya hawa jamaa ningetafute sababu nyingine iliyomuua huyu jamaa!
 
Handsome kajisepesha loh...loh watu tumekiwa wabishi mpaka igonge 80+ uwiii
 
huyu kabla ya kumzika wamlazimishe atoe maelezo ..kifo chake ni cha mashaka sana kama cha yule mzee wa putuluuuu mmiliki wa linaz pub...hatareeeeee
 
Najaribu kuwaza uzito wa hii silaha ikiwa loaded, umbali kutoka kwenye mdomo wa mtutu hadi ilipo trigger kwa mantiki kwamba aklijielekezea... mbili uelekeo wa trigger ukiwa umeshika bunduki inatakiwa kuvutwa nyuma kwa maana hii inawezekana vipi mkono mmoja uweze kuhihili bunduki na mwingine kufuta trigger kukamilisha recommended actions?

Hapa kuna maswali mengi kuliko majibu! Pia nikifuatilia posts kwenye uzi huu naona pengo la mahusiano mema kati ya polisi na raia linavyozidi kuwa kubwa!
 
Depression + poor reasoning + temper + self rejection = suiside!! R.I.P Polisi wetu. Kijana mdogo kweli aisee
 
Kwa picha iliyowekwa hapo juu ni uongo wa ASILIMIA MIA MOJA 100% kwa vigezo hivi viwili.

1.kwa tulio wahi kutumia bunduki ukiangalia pale kwenye triger(sehemu ya kufyatulia risasi) huwa kuna kitu kinaitwa triger pine au usalama kwa jina rahisi ambacho kinazuia triger isifyatuke bila ridhaa ya mtumiaji kwa hiyo ukitaka kufyatua risasi lazima kwanza ukikunjue sasa ukiangalia kwenye hiyo picha kifaa hicho hakijakunjuliwa sasa huyo marehemu alijilipua vipi?

2.bunduki inayotolewa kwa ajiri ya safari/escort lazima iwe na mkanda wa kumuwezesha mbebaji kubeba kwa usalama zaidi sasa hapo pichani bunduki haina mkanda.
 
Back
Top Bottom