Asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe

Wana JF na watanzania kwa jumla,tumekuwa wa kwanza kurusha lawama kuhusiana na huduma mbovu serikalini na taasisi mbalimbali nchini.Shutuma nyingi sana tumezielekeza moja kwa moja kwa Rais na wasaidizi wake.
Vile vile taasisi nyingi kama vile TRA,TPA,TANESCO,POSTA,JKN AIRPORT, WIZARA MBALIMBALI,BUNGE,MAHAKAMA n.k.
Nakubaliana na watanzania wengine baadhi ya tuhuma zinazoelekezwa kwenye taasisi hizi na serkali yenyewe ni za kweli na wanastahili kujirekebishwa kama kweli tumenuia kuliendeleza taifa.
Kitu ambacho nimekuwa nikijiuliza,ni nani anayefanyakazi kwenye hizi taasisi?Je sio sisi wananchi ambao kesho na kesho kutwa tunalaumu serikali na taasisi nyingine ambazo sisi hatufanyi kazi?
Mtu wa tanesco atalalamika huduma za tra ni mbovu ilhali yeye nae huko kazini kwako anafanya haya haya anayolalamikia,mfano huu unagusa watu na taasisi mbalimbali nchini.
Je wewe unaelaumu serikali au taasisi fulani mbovu,huko unakofanyia shughuli zako ni msafi?Tujisafishe wenyewe kabla ya kulaumu wenzetu.
Naamini kila mtu akitimiza wajibu wake ipasavyo tutapiga hatu kubwa kimaendeleo.

Binafsi ni mwathirika wa hizo huduma duni uluizoorodhesha hapo juu. Kwangu natimiza wajibu wangu wa kulisha wananchi kwa kile ninachozalisha shambani kwangu.
 
Back
Top Bottom