Asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by RRONDO, Feb 23, 2010.

 1. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 30,307
  Likes Received: 29,018
  Trophy Points: 280
  Wana JF na watanzania kwa jumla,tumekuwa wa kwanza kurusha lawama kuhusiana na huduma mbovu serikalini na taasisi mbalimbali nchini.Shutuma nyingi sana tumezielekeza moja kwa moja kwa Rais na wasaidizi wake.
  Vile vile taasisi nyingi kama vile TRA,TPA,TANESCO,POSTA,JKN AIRPORT, WIZARA MBALIMBALI,BUNGE,MAHAKAMA n.k.
  Nakubaliana na watanzania wengine baadhi ya tuhuma zinazoelekezwa kwenye taasisi hizi na serkali yenyewe ni za kweli na wanastahili kujirekebishwa kama kweli tumenuia kuliendeleza taifa.
  Kitu ambacho nimekuwa nikijiuliza,ni nani anayefanyakazi kwenye hizi taasisi?Je sio sisi wananchi ambao kesho na kesho kutwa tunalaumu serikali na taasisi nyingine ambazo sisi hatufanyi kazi?
  Mtu wa tanesco atalalamika huduma za tra ni mbovu ilhali yeye nae huko kazini kwako anafanya haya haya anayolalamikia,mfano huu unagusa watu na taasisi mbalimbali nchini.
  Je wewe unaelaumu serikali au taasisi fulani mbovu,huko unakofanyia shughuli zako ni msafi?Tujisafishe wenyewe kabla ya kulaumu wenzetu.
  Naamini kila mtu akitimiza wajibu wake ipasavyo tutapiga hatu kubwa kimaendeleo.
   
 2. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Mm natimiza shaka ondoa
   
 3. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Umesema vyema Mkulu.
  Si wote tunaweza kukubali hili.
   
 4. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kweli...!? na wewe una amini hivyo?
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Feb 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  [
  [/QUOTE]
  aah bana wewe kwakua Ofisini kwako ni mchafu basi unadhani kila mpinga ufisadi nae anakaufisadi kake hufanya......
  kuishi bila ufisadi si ngumu zaidi ya kuishi bila kutamani mwanamke..hivyo inawezekana kwa mtu kuwa msafi, mwaminifu na mwadilifu hadi mauti.
   
 6. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa ukitaka weka kamati inichunguze!
   
 7. m

  mob JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2010
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,131
  Likes Received: 643
  Trophy Points: 280
  ndugu zangu tatizo lililopo ni mfumo wa kufanya kazi kimazoea.hii ni mbaya sana fikiria ni mara ngapi unakuta nguzo imeanguka unapiga simu tanesco au unandugu yako anaiba umeme unawafahamisha teneco?chukua hatua madthubuti ya kupambana na nafsi yako kwa kufanya kazi kwa bidii na sio kutegemea serikali itafanya kila kitu.kwa mfano we huna uwezo wa kufunga bomba lililopasuka hadi usubirie idara za maji(daswco-dar,muwasco )
   
 8. m

  mob JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2010
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,131
  Likes Received: 643
  Trophy Points: 280
  tatizo si kuchunguzwa we hujapata mahali pa kufanyia huo ufisadi kama ingekuwepo ungekuwa unachukua seringeti boys maana nawaogopa sana dada zetu wenye hela
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280

  tunaweza kuwa si watakatifu ..ila ukinambia swala la tanesco kwangu mie linaniboa sana .
  Hii kata umeme rudisha kata rudisha ,wakituuunguzia vitu vyetu huwa wanalipa.
   
 10. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Tupo wengi kweli watoa kibanzi machoni pa wenzetu,ilhali boriti zikiangamiza mboni zetu!!
   
 11. m

  mob JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2010
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,131
  Likes Received: 643
  Trophy Points: 280
   
 12. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wapi jiwe nianze kutupa mimi!
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,524
  Likes Received: 573
  Trophy Points: 280
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
   
 15. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sisi si watakatifu ila tunataka watakatifu watuongoze..
   
 16. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
   
 17. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #17
  Feb 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli mimi nimsafi.nathubutu kusema hili.
   
 18. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Wako watu wazuri tu na waaminifu kazini kwao ila huangushwa na mabosi wao. Chukulia mfano wa richmond, wataalamu wa TANESCO walishatoa maoni yao ya kitaalamu kuhusu kampuni hiyo lakini yakaachwa na wakubwa kuunda kamati zao za kuhalalisha wizi wao. Sasa ndo maana tunailamu serikali kwasababu wao ndo wenye maamuzi makubwa na hali mbaya ya kiuchumi na wizi wa mali ya umma chanzo ni wakubwa na si watu wa chini. Kwamfano nani alisaini mikataba ya madini, nani aliwapa Richmond tender, nani aliidhinisha wizi wa EPA, nani aliwapa RITES kuendesha TRA, nani aliwapa TICS tender ya kupakua mizigo bandarini, nani alisaini mkataba wa IPTL etc. Haya yote yamefanywa na watu wa ngazi za juu sana serikali na watu wa chini walishinikizwa tu kutekeleza. Kwahiyo hatuwezi kuacha kuilamu serikali hata siku moja.
   
 19. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 30,307
  Likes Received: 29,018
  Trophy Points: 280
  wengi wangekuwa kama wewe,tungefika mbali.
   
 20. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 30,307
  Likes Received: 29,018
  Trophy Points: 280
  nakubaliana na wewe mkuu,
  je vpi kuhusu wale jamaa pale airport wanavyosumbua watu wawape tsh walizobakisha kabla kupanda ndege?vipi kuhusu bandarini hadi mlinzi getini anadai hongo ndio utoe gari?na hao tra wanavyosumbua watu ili mradi uwape hela ili mambo yako yaende sawa je?hawa si wananchi kama mimi na wewe?hapa sizungumzii top management,nazungumzia watu wadogo unaogongana nao kila siku kwenye idara mbalimbali.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...