Asilimia 50% kwa 50% Bungeni ni kuwa wavivu wa kufikiri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asilimia 50% kwa 50% Bungeni ni kuwa wavivu wa kufikiri!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TumainiEl, May 18, 2010.

 1. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,891
  Likes Received: 1,644
  Trophy Points: 280
  Niwakati umefika kuwa watu wakufikiri na kupima maneno ya kiabunuwazi yanayotolewa na viongozi wetu. Nikweli mwanamke ni injini ya muhimu sana ktk uchumi wetu ila ikiwa sera zakuwawezesha zitakuwa ni za kisiasa nakuuwacha ukweli, basi tutapotoka. Siku zote serikali yoyote duniani haifanyi maamuzi yasio angalia tamaduni zake ila kila mabadiliko yapaswa kufuwata mila na destur za nchi usika. Ukiangalia dhana nzima zakuwawezesha wanawake zipo zaidi kiundugu na kiurafiki kiasi wale wanawake wenye uwezo wanabaki na wale wasio nauwezo ndio wanakuwa viongozi. Hili lanikera nakuona kuwa kuna viongoz wachache ndani ya serikali wanaliujumu taifa hili. Kama kweli wameamua kuwapa nafasi 50% by 50% pia sheria zibadilike. Hivi embu tutafakari na kufikiri what will be a future of men into new generation? Upendeleo huu usio angalia vipawa utawafanya wanaume wataifa hili kuwa sii kitu. Najambo lakushangaza hakuna hata mmoja anashituka nakujiuliza kile kinasemwa. Jaman mim nasema tuache utani maana kama USA taifa kubwa na tajiri bado lina mwangalia mwanaume kama lulu ktk nyanja mbal mbal bas tujiulize kulikoni kwetu. NAPINGA UPENDELEO UNAOPONDA UTU WA MWANAUME NA KUSEMA HILO HALIKUBALIKI, TUNAITAJI WANAWAKE WATAKAO KUWA MSAADA KWA WANAWAKE WENZAO NA SIO KUPIGA MAJUNGU NA UMBEA, NIBORA KUWA NA VIONGOZ KUMI JASIR WA KIKE WATAKAO WAONGOZA WANAWAKE WENZAO KULIKO WABUNGE MIA WASIO NA UJASIR WALA MWELEKEO ILA FITINA NA MAJUNGU BUNGENI. TAIFA HILI BILA KIKWETE INAWEZEKANA, TAIFA HILI NI LA WOTE WANAWAKE NA WANAUME NA UPENDELEO NIKUUWA UTAIFA WETU NA TAMADUNI ZETU. Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mkubwa, fifty fifty inawezekana ila waende majimboni wakagombee siyo kusubiri viti maalum na vile vya kuteuliwa!
   
 3. m

  mtemi Member

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo la 50% 50% ni vigogo kuweka wake zao ,na nyumba ndogo ,binti zao nk yaani ni vurugu tupu......uisadi mwingine.....tuchaguane tuache kuiga yasiyiotufaa
   
 4. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Tumaini El
  Ungeenda mbali zaidi kwa kusema watanzania wengi hasa wasomi ni wavivu wa kufikiri na wengi tunafikiri ki-utopia.
  Pia wengi wetu ni hodari wa kukosoa [tuna PHD kwa hili] bila kutoa alternative options.
  Hata ule msemo wa "maisha bora kwa kila mtanzania" ukiuliza maana yake nini utakuta kila mtu anatafsiri yake.
  Sisi wana JF tunaweza kwa kiwango chetu tukasaidia jamii kwa kuwa na constructive criticisms na kujaribu kutoa alternativi options.
  Mfano mzuri ni kuhusu uchaguzi ujao. Wengi kwenye JF wanamzungumzia JK kuwa hafai kupewa nafasi nyingine lakinni kwa mawazo yangu badala ya kumzungumza mtu tungelenga kwenye kuchambua na kukubaliana attributes za kiongozi afaaye kuwa raisi wetu ni zipi halafu tukatumia hizo sifa kwa kuchambua kila possible candidate wa nafasi hiyo kama wana sifa stahili ni kisha tukapiga debe
   
 5. kmp

  kmp Member

  #5
  May 19, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi kwa mtizamo wangu jambo hili linawezekana kabisa ila suala la kuwa makini ni namna hao wawakilishi wenyewe watakavyopatikana, isije ikawa ni upendeleo kwenda mbele kama mtemi alivyotanabaisha.

  Lakini pia tujiulize mbona Rwanda wameweza... gonga kwenye link for reference

  Rwanda Parliament in Rwanda - Rwanda DG
   
Loading...