Asili ya neno "Bodaboda"

Asili ya neno "Bodaboda"

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Unajua watanzania wengi wakisikia neno Bodaboda wanajua ni neno lenye chimbuko la Kiswahili au lililoanzishwa Tanzania. Lakini si kweli

Neno “bodaboda” halikuzaliwa Tanzania —lilizaliwa mpakani. Hapo zamani kidogo, miaka ya 1960–70, mpakani mwa Kenya na Uganda, kulikuwa na usafiri wa baiskeli uliobeba abiria kuvusha watu from border to border (Mpakani wa nchi moja hadi mpakani wa nchi nyingine). Wazungu na Wahindi walikuwa wanaita, “border to border transport.”

Neno bodaboda linatokana na maneno ya Kiingereza "border to border", yaliyokuwa yakitumika miaka ya nyuma katika maeneo ya mpakani kati ya Kenya na Uganda, hasa mji wa Busia. Wakati huo, waendesha baiskeli walikuwa wakisafirisha watu na mizigo kutoka mpaka mmoja hadi mwingine wakipita maeneo ambayo magari yalikuwa hayafiki kirahisi.

Maneno border-border yalivyokuwa yakitamkwa kwa haraka na wenyeji, yakageuka kuwa boda-boda. Sasa hapa ndio lugha ya mtaa ikaingia kazini—border to border ikakatwa, ikageuka taratibu kuwa boda-boda.

Baadaye, huduma hii ilienea zaidi ndani ya Kenya na sehemu nyingine za Afrika Mashariki. Muda ulivyopita na teknolojia ya usafiri kukua basi baiskeli zikawa pikipiki, lakini jina likabaki. Na ndipo jina bodaboda likasambaa hadi Tanzania, Uganda na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Tanzania tulipopokea neno hilo tukapita nalo mazima, lakini asili yake ya matumizi na jina ilianzia Nchini Kenya. Leo ukiwa Kampala, Kisumu, Mwanza, Dar au Mbeya—ukisikia bodaboda, unajua ni usafiri wa haraka, wa mItaani, unaopenya traffic (Jam ya magari), usafiri unaoishi kwenye vumbi na hustle za hapa na pale.

_123614664_boda2.jpg.webp
 
Afu kuna hawa Pikipiki wanaita Bodaboda.
What I know bodaboda ni biashara ya usafirishaji kwa kutumia Pikipiki. Na Pikipiki ikibaki kama chombo cha moto.
 
Mbona bodaboda sisi tumeanza kusikia kutokea Nigeria?🤔
 
Afu kuna hawa Pikipiki wanaita Bodaboda.
What I know bodaboda ni biashara ya usafirishaji kwa kutumia Pikipiki. Na Pikipiki ikibaki kama chombo cha moto.
Hata Neno “pikipiki” halikutoka Ulaya moja kwa moja. Chanzo chake kiko kwenye neno la Kiingereza “motorcycle”, lakini asili ya jina hilo ni Mlio wake. Pikipiki za mwanzo zilikuwa zinapita mitaani zikienda kwa sauti ya “pi-ki-pi-ki-pi-ki…”—kelele nyepesi, ya kukatika-katika. Watu wa mtaani hawakuhitaji kamusi; walichukua mlio, wakaupa jina. Na mpaka leo ndio Jina linalotumika kumaanisha chombo cha magurudumu mawili chenye kutumia injini
 
Arusha wanaita Toyo, mwanzo nilikuwa sielewi anasema nini huyu ariiiifu
 
Back
Top Bottom