Atoto
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 82,147
- 159,068
Marahabaaaa!
Lugha ni sehemu ya jamii nayo huakisi maendeleo na mabadiliko ya jamii hiyo katika nyanja zote za maisha yake. Na kwa vile hakuna jamii ambayo imesimama tisti, lugha nayo hubadilika badilika ili kwenda sambamba na mabadiliko ya jamii. Kwa sababu hiyo maneno hubadilishiwa muktadha na mawanda ya matumizi yake.
Japo kietimolojia salamu hii ya shikamoo ina makandokando hayo ya kitumwa, leo hii imebadilishiwa muktadha na mawanda yake ya kimatumizi na kila mtumia lugha anajua kuwa lengo lake kuu ni kuonyesha heshima mathalani kwa wazee. Na kwa muktadha huu mimi sioni tatizo lolote.
Ukifanya uchunguzi wa kietimolojia kwa maneno mengi (hasa ya mkopo) ukayachunguza kwa makini yalikotoka na yalivyotumika hapo zamani utagundua kwamba maneno mengi tu yana matatizo na utakuwa na kazi ngumu sana ya kubadili kila neno lililokuwa likitumika vibaya hapo zamani. Na itabidi utafute neno jipya mbadala. Isitoshe lugha hai huwa haipendi kutungiwa misheria. Wewe unaweza kupiga marufuku neno unalodhani kuwa lina historia mbaya lakini jamii ikaamua kuendelea kulitumia tu katika matumizi yake mapya, na hakuna utakachofanya. Ndiyo maana BAKITA wanatunga misamiati rasmi kila siku lakini hakuna anayeitumia huku mitaani na misamiati hiyo wamebaki nayo katika makabrasha yao huko.
Shikamoo !!!