Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2007
Messages
24,185
Points
2,000
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2007
24,185 2,000
Nimeipenda

Wanangu na kusoma shule za kuongea kimombo.. hiyo salamu kwa kweli najivunia kuwafundisha kuwa ni lazima waitumie

Miaka ya siku hizi watoto wengi nawashangaa wazazi wao hawawakazanii kuamkia na neno hilo..

Halafu unaona watoto wanakulia hapa nchini wanajisikia kutokutumia salamu hiyo kwa watu wakubwa kwao hata wazazi..

Haya tunasubiri mengine tujifunze.. hivi kiswahili kwanini kigumu?.. yaani eeeeh
 
MATHIAS KABYEMERA

MATHIAS KABYEMERA

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2013
Messages
1,799
Points
1,500
MATHIAS KABYEMERA

MATHIAS KABYEMERA

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2013
1,799 1,500
bora nitumie lugha yangu!
 
ANCIENT FROM EGYPT

ANCIENT FROM EGYPT

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2015
Messages
469
Points
500
ANCIENT FROM EGYPT

ANCIENT FROM EGYPT

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2015
469 500
Sipendi hili neno shikamoo
 
P

Psiteshio72

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2016
Messages
579
Points
500
P

Psiteshio72

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2016
579 500
Jifunze nami kingereza kwa kiswahili kwa bei cheee, kwa mwezi. Masomo ni online na ni kwa miezi miwili 2,Tunasoma kwa video, pich, audio no kupitia WhatsApp peke,Nipigie sasa na utokwe na aibu ya kutojua kingereza fasah ingali wew ni msomi, many a bias hara ama mtendaji wa serikali,Piga 0753093869,baada ya kuhitimu tutakupatia ajira ukitaka, katika mataw yetu yotee... Mfano wa masomo yetu:

Somo la 1

(SECTION A; TENSES IN THE ACTIVE VOICE )

(A)Simple Tenses ,:

1. Simple Past Tense ( ‘li’)
- Wakati huu huongelea jambo lililofanyika na kukamilika mara moja wakati uliopita.
Mifano ; tulikuja ,walitembea, alicheza.
- Wakati huu huashiriwa na silabi ‘li’ ambayo hufanya tutambue kuwa tunaongelea jambo lililofanyika mara moja na likamalizika kufanyika katika wakati uliopita. Hii silabi ‘li’ ni lazima iunganishwe na kitendo moja kwa moja kabla ya kitendo. Mfano ; ‘Tuliimba’, tofauti na ‘Tulikuwa tunaimba’ ambapo ‘li’ imefuatiwa na kifungu ‘kuwa’ na sio kitendo. Katika maneno ‘tulikuwa tunaimba’, kitendo ‘imba’ kimetanguliwa na ‘na’ na sio ‘li’ kwa hivyo maneno hayo hayapo katika wakati huu wa Simple Past Tense, ‘li’.

Kanuni za kutumia Simple Past Tense ‘li’

a) Sentensi za taarifa/kutoa taarifa
Katika wakati huu, huwa tunapoelezea jambo tunatanguliza mtendaji wa jambo, (I/We/You/They/He/She/It) kisha tunafuatisha kitendo moja kwa moja kikiwa katika umbo la wakati uliopita.
Mfano ; - kitenda ‘enda’ ni ‘go’. Umbo lake la wakati uliopita, yaani ‘-lienda’ ni ‘went’. Tutatanguliza mtendaji wa jambo kisha tufuatishe neno ‘went’.

Sentensi za mifano;
- Juma alienda. ………. Juma went.
- Tulienda. ……… We went.
- Basi liliondoka. ……. The bus left.
- Nilicheza. ……. I played.
- Uliimba. ….. You sang.
- Walikimbia. ….. They ran.
- Maria alipika. ……. Maria cooked.
NB : Hatuweki kitu chochote katikati mwa mtendaji na kitendo.

b) Kuuliza maswali katika Simple Past Tense

- Maswali katika wakati huu huanzia na neon ‘did’. ‘Did’ ikitumika ni lazima kitendo kiwe katika umbo la kawaida kwa sababu ‘did’ ina ‘li’ ndani yake hivyo ‘li’ nyingine haihitajiki. Ina maana hiyo ‘did’ tayari imeshawakilisha wakati uliopita.
- ‘Did’ hufuatwa na nafasi inayouliziwa swali.
Mifano ya tafsiri :
- ‘Did Juma _______ ?’ …….. ‘Je, Juma ali______?’
- ‘Did they _______ ?’ ………. ‘Je, wao wali______ ?’

Sentesi za mifano :

1. Did Juma go?
Je, Juma ali enda ?

Jibu ; ( Hapana, hakuenda)…..( Kukanusha)
No, he didn’t go.
Au ; ( Ndio, alienda)…. Kukubali
Yes, he went.

2. Did she cook?
Je, alipika?

Jibu ; ( Hapana, hakupika)…..Kukanusha
No, she didn’t cook.
Au ; Ndio, alipika….. (Kukubali)
Yes, she cooked.

** katika kitabu kuna michoro ambayo inaonyesha tafsiri ya moja kwa moja ya kila kipengele cha sentensi kutoka kiswahili hadi kingereza ila hapa hatujaionyesha.

NB ; Tukiongeza neno ‘did’ katikati mwa jibu la kukubali, huwa ni kuweka msisitizo kama vile ambavyo kwa Kiswahili huwa tunaandisha sauti ili kuweka msisistizo ila sasa kwa Kingereza sauti haipandishwi ila msisitizo upo pale pale.

Mifano ; 1. Did Juma go ? …… Je, Juma alienda?
- Yes, he did go. ….. Ndio, alienda! (KWA MSISITIZO)

2. Did they cook? …….. Je, walipika?
- Yes, they did cook. …… Ndio, walipika! (KWA MSISITIZO)

NB ; Tunapokanusha sentensi kwa kutumia ‘did not’/ ‘didn’t’ , huwa hatutumii kitendo kikiwa katika umbo la wakati uliopita maana ile ‘did’ inakuwa imeshawakilisha wakati uliopita (‘li’ ambayo kinume chake ni ‘haku’) kwa hivyo hatuhitaji wakati uliopita kwa mara ya pili. Tukitumia umbo la wakati uliopita pia kwa kuuliza swali lililoanzia na ‘did’ pia tunakuwa tumeweka ‘li’ mbili katika sentensi, jambo ambalo sio sahihi.

Mifano ; 1. She didn’t went yesterday. ( Badala ya ‘She didn’t go yesterday.’)
Haku lienda jana. ( Badala ya ‘Hakuenda jana.’)

Au; 2. Did she went yesterday?
( Badala ya ‘Did she go yesterday?’)

- Je, yeye ali lienda jana?
( Badala ya ‘Je, yeye alienda jana?)
 
A

Amonni

Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
11
Points
45
A

Amonni

Member
Joined Jul 29, 2015
11 45
Shikamoo ni salamu ambayo Mtumwa nyakati zile alilazimika kumsujudia Bwana wake huku akimshika miguu na kusema Sikamoo (yaani nipo chini ya miguu yako) na Bwana wake anaitika na kusema marahabaa (yaani akimaanisha sawasawa wewe upo chini yangu).

Kumwambia mtu nipo chini ya miguu yako ni udhalilishaji na unaondoa utu kwa mtu hasa anayesalimia. Tunasema siku zote binadamu wate ni sawa! sasa inakuwaje binadamu mmoja hasa mdogo kiumri awe chini ya mtu mwingine? Natamani kama Taifa tungeipiga marufuku hii salamu ya kitumwa.

Kwani kumsalimia anayekuzidi umri Habari za leo, mchana au za jioni mzee, mama, kaka,dada nk kuna ubaya gani?. Ingekuwa salamu nzuri hata waarabu wangesalimiana shikamoo. Ila kwa sababu ina dhana ya kitumwa ndo maana wao hawasalimiani.
 
Faru Kabula

Faru Kabula

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Messages
12,042
Points
2,000
Faru Kabula

Faru Kabula

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2009
12,042 2,000
Kwa kuwa lengo la watumiaji wa hiyo salamu sio la kitumwa bali kutoa heshima, basi mimi naona iko poa tu na iendelee kutumika. Lugha ni sauti zilizokubaliwa na jamii katika kuwasiliana, so maadam jamii yetu ya Waswahili imelikubali neno shikamoo kama ni salamu ya heshima, basi imeshakuwa rasmi katika lugha yetu, sio yao tena.
Tusifanye mambo yaonekane Kama vile complex kumbe simple tu.
 
Coco

Coco

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2019
Messages
406
Points
1,000
Coco

Coco

JF-Expert Member
Joined May 13, 2019
406 1,000
Utumwa haupo kwa neno wala maana ya neno bali application yake!
Hakuna mahali nimedharirika kwa kusema salamu hiyo kwa mtu aliye nizidi umri.
 
Nakubaliana nawe.
 
SHIMBA YA BUYENZE

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2014
Messages
107,567
Points
2,000
SHIMBA YA BUYENZE

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2014
107,567 2,000
Lugha ni sehemu ya jamii nayo huakisi maendeleo na mabadiliko ya jamii hiyo katika nyanja zote za maisha yake. Na kwa vile hakuna jamii ambayo imesimama tisti, lugha nayo hubadilika badilika ili kwenda sambamba na mabadiliko ya jamii. Kwa sababu hiyo maneno hubadilishiwa muktadha na mawanda ya matumizi yake.

Japo kietimolojia salamu hii ya shikamoo ina makandokando hayo ya kitumwa, leo hii imebadilishiwa muktadha na mawanda yake ya kimatumizi na kila mtumia lugha anajua kuwa lengo lake kuu ni kuonyesha heshima mathalani kwa wazee. Na kwa muktadha huu mimi sioni tatizo lolote.

Ukifanya uchunguzi wa kietimolojia kwa maneno mengi (hasa ya mkopo) ukayachunguza kwa makini yalikotoka na yalivyotumika hapo zamani utagundua kwamba maneno mengi tu yana matatizo na utakuwa na kazi ngumu sana ya kubadili kila neno lililokuwa likitumika vibaya hapo zamani. Na itabidi utafute neno jipya mbadala. Isitoshe lugha hai huwa haipendi kutungiwa misheria. Wewe unaweza kupiga marufuku neno unalodhani kuwa lina historia mbaya lakini jamii ikaamua kuendelea kulitumia tu katika matumizi yake mapya, na hakuna utakachofanya. Ndiyo maana BAKITA wanatunga misamiati rasmi kila siku lakini hakuna anayeitumia huku mitaani na misamiati hiyo wamebaki nayo katika makabrasha yao huko.

Shikamoo !!!
 
A

Amonni

Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
11
Points
45
A

Amonni

Member
Joined Jul 29, 2015
11 45
Utumwa haupo kwa neno wala maana ya neno bali application yake!
Hakuna mahali nimedharirika kwa kusema salamu hiyo kwa mtu aliye nizidi umri.
Kwa sababu asili ya hilo neno ni utumwa basi hata km unalitumia kwa maana nyingine uasili wake hauondoki! Mfano unapomwita mtoto wa mateso kuna karoho katamfuatilia kwa namna moja ua nyingine
 
A

Amonni

Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
11
Points
45
A

Amonni

Member
Joined Jul 29, 2015
11 45
Lugha ni sehemu ya jamii nayo huakisi maendeleo na mabadiliko ya jamii hiyo katika nyanja zote za maisha yake. Na kwa vile hakuna jamii ambayo imesimama tisti, lugha nayo hubadilika badilika ili kwenda sambamba na mabadiliko ya jamii. Kwa sababu hiyo maneno hubadilishiwa muktadha na mawanda ya matumizi yake.

Japo kietimolojia salamu hii ya shikamoo ina makandokando hayo ya kitumwa, leo hii imebadilishiwa muktadha na mawanda yake ya kimatumizi na kila mtumia lugha anajua kuwa lengo lake kuu ni kuonyesha heshima mathalani kwa wazee. Na kwa muktadha huu mimi sioni tatizo lolote.

Ukifanya uchunguzi wa kietimolojia kwa maneno mengi (hasa ya mkopo) ukayachunguza kwa makini yalikotoka na yalivyotumika hapo zamani utagundua kwamba maneno mengi tu yana matatizo na utakuwa na kazi ngumu sana ya kubadili kila neno lililokuwa likitumika vibaya hapo zamani. Na itabidi utafute neno jipya mbadala. Isitoshe lugha hai huwa haipendi kutungiwa misheria. Wewe unaweza kupiga marufuku neno unalodhani kuwa lina historia mbaya lakini jamii ikaamua kuendelea kulitumia tu katika matumizi yake mapya, na hakuna utakachofanya. Ndiyo maana BAKITA wanatunga misamiati rasmi kila siku lakini hakuna anayeitumia huku mitaani na misamiati hiyo wamebaki nayo katika makabrasha yao huko.

Shikamoo !!!
Nimekuelewa ila pia matumizi ya kitu chochote hutokana na jamii husika. Pia sehemu hiyo hiyo ya jamii ikiamua kutokufanya au kufanya jambo fulan wengine hufuata hasa wakijua ukweli wa hilo jambo.
 
SHIMBA YA BUYENZE

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2014
Messages
107,567
Points
2,000
SHIMBA YA BUYENZE

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2014
107,567 2,000
Nimekuelewa ila pia matumizi ya kitu chochote hutokana na jamii husika. Pia sehemu hiyo hiyo ya jamii ikiamua kutokufanya au kufanya jambo fulan wengine hufuata hasa wakijua ukweli wa hilo jambo.
Nadhani hata mimi, kimsingi, nimesema hivyo hivyo. Lugha ni mali ya jamii na jamii inaweza kuamua cho chote. Na kukurupuka kutunga misheria na kupiga marufuku matumizi ya maneno haitasaidia lolote kama jamii husika haioni sababu ya msingi ya kufanya hivyo. Wengi walishajaribu na wakashindwa. Lugha haiko hivyo !!!
 
B

Blac kid

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Messages
4,219
Points
2,000
B

Blac kid

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2012
4,219 2,000
Sikubaliani na hoja zako ila naweza pia kusapoti kama taifa tubuni salamu mpya na tuipigie promo Kama salamu mbadala inayokubalika na rika zote, salamu ya shikamoo ina changomoto nyingi ukilinganisha na salamu za mataifa mengine ama makabila ya hapa nchini naomba tu tuzijadili
 
Atoto

Atoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Messages
60,120
Points
2,000
Atoto

Atoto

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2013
60,120 2,000
Mkuu kunywa soda hapo kwa mangi.
Kwa kuwa lengo la watumiaji wa hiyo salamu sio la kitumwa bali kutoa heshima, basi mimi naona iko poa tu na iendelee kutumika. Lugha ni sauti zilizokubaliwa na jamii katika kuwasiliana, so maadam jamii yetu ya Waswahili imelikubali neno shikamoo kama ni salamu ya heshima, basi imeshakuwa rasmi katika lugha yetu, sio yao tena.
Tusifanye mambo yaonekane Kama vile complex kumbe simple tu.
 
Forum statistics

Threads 1,334,518
Members 512,012
Posts 32,478,860
Top