Asili ya majina Mikocheni, Masaki na Kariakoo

Asili ya majina Mikocheni, Masaki na Kariakoo

Kivukoni sehemu ya kuvukia kwenda Kigamboni/peninsular ya upande wa pili, Stand ya mkoa ilikuwa Kisutu, eneo la miti yaani Msutu/Msitu
Mlimani city kuanzia UDSM paliitwa Mlimani kwani ndiyo eneo liliopo juu zaidi kwa Dar, kuna Mlimani Park pia eneo la Mwenge, ambao ni eneo la kukutana wafanya biashara na wasafiri
Mbezi Luis kuna mzungu Louis alikuwa na mashamba ya mananasi
Kwa Msuguri , jina la CDF wa zamani Gen Musuguri
Ubungo Maziwa kulikuwa na kiwanda cha maziwa ya paketi
Bakhressa pale Buguruni kiwanda cha mikate ya siha/NMC
Buguruni eneo la nyuma kule viwandani paliitwa Makuburi baadae watu wakahamishiwa Kigogo - sehemu ya kukusanyia magogo ya kuni
Mtoni limetokana na mto Kizinga/Mzinga unaanzia vilima vya Pugu
Mbagala na Tandika maeneo tambarare ya kulima
Vingunguti kwenye aina ya nyumba za kienyeji kama tembe, Gungu,
Madale eneo lenye mwinuko, kidale, vidale
Msimbazi - mfereji unaitwa simbazi

Maeneo ya Mzizima (DSM) kuanzia Fire, kuelekea Upanga l, Muhimbili mpaka kituo cha Polisi Selander, Mnazi Mmoja mpaka Posta Mpya (Mchafukoge) yalikuwa mashamba ya minazi na miembe yakimilikiwa na familia za Wazaramo kina Abdallah Mfaume, Mwinyiheri Akida, Mohamed Tambaza, Mwinyiwaziri Mwinyi, Kidato bt Mwinyi Abdallah, Mwinyishehe Mwinyikheri na Mmanga Mwinyimkuu. Serikali ya Mkoloni iliwaomba kujenga barabara, shule, hospital nk Wakapewa baadhi ya maeneo ya Magomeni, Temeke na Ilala ambapo walihamia na wengine wakabaki Kariakoo. Familia ya Tambaza bado inamiliki eneo la makaburi na Msikiti wa Tambaza
 
Wameiga tu, hata Dodoma kuna Oysterbay, wakifananisha na ushuani
Dah, hatari sana.

Hata New York kuna Oysterbay, lakini iko Long Island baharini, kuna hiyo ghuba, na nafikiri pana chaza au walikuwapo. Kwa hivyo hiyo Oysterbay ya New York inaakisi jina.

Hata Alabama kuna Oysterbay. Na yenyewe iko baharini hivyo hivyo.

Lakini kuwa na Oysterbay Dodoma au Iramba, sehemu ambazo hazina bahari wala ghuba, kwa mtu anayelielewa hilo jina na maana yaje, ni kichekesho.
 
admin unganisha huu uzi na ule wa tangu 2018
 
Kuna maeneo yanatajwa bila kujua asili yake kutaka kuonekana wako mbele, wangebaki tu na Majengo au Uzunguni kama ilivyo mikoa mingi
Oysterbay Afrika zipo hiyo ya Dar, Freetown Sierra Leone na ya Eastern Cape, South Africa
 
Tuangalie tu tusije kuambiana kwamba Machinga ilitokana na Marching Guys.... na sio Chinga wa kule Uchingani..
 
Tuangalie tu tusije kuambiana kwamba Machinga ilitokana na Marching Guys.... na sio Chinga wa kule Uchingani..
Yeah, hizi story za chanzo cha jina fulani zina version kibao. Wengine wanasema majina au maneno ya kizungu yaliyoshindwa kutamkwa wengine wanasema hayo ni majina ya wazawa
 
Uzunguni sehemu waliyokaa wazungu, uhindini sehemu waliyokaa wahindi, uswahilini sehemu waliyokaa wazawa. Hizi sehemu zilikuwa maarufu enzi za ukoloni ingawa ziliendelea kuitwa hivyo hata baada ya uhuru.

Cc: Mimi Wewe Yule
Wamakonde dar ndiyo watu waliyokuwa wameyashika maeneo"prime areas "ila sehemu nyingi walihamishwa hawakuwa na mahesabu ya mbali 😄

Ova
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom