Asili ya majina Mikocheni, Masaki na Kariakoo

Asili ya majina Mikocheni, Masaki na Kariakoo

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
10,908
Reaction score
18,876
Mikocheni asili yake ni miti ya mikoche. Mikocheni maana yake mahali penye mikoche. Mikoche yenyewe ni miti iliyo kama miwese/minazi. Miti hii inapatikana pwani ya Afrika Mashariki hadi huko South Afrika. Pia inazaa matunda yaliwaywo.
1745087795306.jpeg


Matunda yake.
1745087844882.jpeg


Masaki limetokana na neno la Kizaramo Saki. Saki maana yake ni eneo wanakougulia watu/wagonjwa. Masaki ni wingi wa saki.

==========================

Jina Kariakoo lilianza tokea enzi kabla ya mjerumani, kijiji hiki kiliitwa "Carrier Corps." Hii sehemu ilipata umaarufu sana kwa sababu ilikuwa frequently raided by slave masters kuja kuchukua watumwa. Kwa mantiki hii, jina halisi ni Carrier Corps ila wenyeji walitamka walivyoweza, hence, Kariakoo.
 
Mikocheni asili yake ni miti ya mikoche. Maana yake mahali penye mikoche. Mikoche yenyewe ni miti iliyo kama miwese/minazi. Mii hii inapatikana pwani ya Afrika Mashariki hadi huko South Afrika. Pia inazaa matunda yaliwaywo.
View attachment 3309803

Matunda yake.
View attachment 3309806

Masaki limetokana na neno la Kizaramo Saki. Saki maana yake ni eneo wanakougulia watu/wagonjwa. Masaki ni wingi wa saki.
Oyster Bay ni Ghuba ya Chaza
 
Asili ya maeneo ya Dar
Mzizima, sehemu ya uzima ya wenyeji wazaramo na wakwere
Kawe ni Cow Way, njia ya kupitisha ngombe kupeleka kiwandani Tangayika Packers
Lugalo mkoloni alipaita Colito baracks baadae ikapewa jina la ngome ya Mkwawa, Lugalo
Kariakoo ni Carrier Corps, kikosi cha wapagazi wa wazungu
Mikocheni - eneo lenye mikoche, aina ya miti
Magomeni - eneo lenye miti yenye magome kwa wingi hasa yaliyotupwa Tanga, Zbar na Mombasa pia lipo, mapipa na makuti yaliezekewa maeneo hayo,
Tabata dampo kulikuwa na sehemu ya kutupa takataka (dump) za Dar kabla halijahamishiwa Pugu, hilo eneo ni landfill ilotokana na taka zote za Dar tangu mkoloni
Msasani ni mti wa msasa au mufuti
Bunju, samaki anaitwa hivyo
Mwananyamala - mwana nyamaza , kulikuwa na mashamba ya mpunga na usiku panatisha sana
Fire - kikosi cha zimamoto, Fire Brigade enzi za mkoloni
Mnazi mmoja - ulikuwepo hapo
Masaki - paliitwa kichangachui zamani lakini pia kuna eneo linaitwa Masaki lipo uzaramoni, asili yake neno saki
Oysterbay - walivua oysters maeneo hayo
Forodhani - bandari panaitwa forodha
Mchafukoge - eneo lenye mafuriko , low lying areas, linaiingiza uchafu sana
Bagamoyo, bwaga moyo - watumwa ilibidi wabwage moyo watulie kabla ya kupanda meli, Senegal kuna door of no return, Ile de Goree
Gerezani kulikuwa na gereza pale ofisi za dawasco zamani na mwembe wa kunyongea pia, mjerumani alitumia wafungwa kujenga reli na kupakia mizigo, baadae likahamishiwa Keko
Chang’ombe lilitumika kutunzia ng’ombe kabla ya kusafirishwa au kuchinnjwa kama ilivyo Dodoma, Mbeya na Morogoro
Goba - eneo lenye rutuba, kizaramo, zamani yalikuwa mashamba
Manzese, aina ya miti ya asili, Nzese kulikuwa na pori la miti hiyo
Ubungo, aina ya miti yenye matunda ya mabungo, kwenye ule mto unatokezea kwa mtogole
Kigamboni- ka sehemu kadogo, kigambo au peninsula
Shekilango alikuwa Waziri enzi za Nyerere
Maeneo mengi yana asili ya ukwere na uzaramo
 
Shamba la Bibi: Wakati wa Wajerumani, wajerumani walitenga maeneo kwa ajili ya familia ya kifalme kuja kuwinda. Humo waafrika hawakuruhusiwa kuwinda wala kurandaranda. Waafrika wakaita maeneo hayo Shamba la Bibi, yaani eneo la mke wa mfalme wa Ujerumani kuja kuwinda. Mengine kama Selous yamekuwa hivyo hadi sasa ni hifadhi za taifa. Leo Shamba la Bibi inamaanisha kinyume kabisa na maana yake, na watu wametafuta hadi explanation kwa ajili ya hiyo maana mpya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom