Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
- Thread starter
- #121
Nina ufahamu wa kutosha juu ya Carbon 14 kutotoa precise date ya tukio but it's still the most reliable technology out there.ni kweli binadamu wa leo tuna mabadiliko kadhaa miilini mwetu tofauti na wa karne zilizopita iliyosababishwa na sababu tofauti tofauti kama utofauti wa eneo kijiografia,shughuli za jamii husika nk. vilevile naamini kweli dinosaurs walikuwepo kipindi hicho bila ubishi maana kama vile ulivyosema tunao ushahidi wa mabaki yao.
ninachopinga mkuu ni hiyo hoja yako hapo juu kuwa Waafrika IQ yetu ni ndogo tangu kitambo...hii si kweli kabisa!kama mifano niliyokutolea hapo juu ya 'civilizations' zilizopita ambazo mpk leo alama zake duniani bado zipo...kama IQ yao ingekuwa ndogo wangefanikiwa yote hayo?? mfano kuna mfalme alipata kutawala kutoka Kushi(Ethiopia) alieitwa Nimrod ambae ufalme wake ulisambaa karibia dunia yote ya kale kama miji ya Babylon,Erech,Accad(Akkad). ndie alieasisi mpango wa kuwajumuisha jamii zote ziwe nchi moja chini yake...na ndie anaedhania na baadhi ya wataalamu kuwa ndie mfalme wa kwanza duniani. huyu jamaa alikuwa ni mtu MWEUSI! na pia lazima ujue mkuu kuwa ktk 'dating' ya mafuvu pamoja na 'fossils' zingine njia inayopenda kutumiwa na wataalamu ni carbon 14 ambayo ndio inaaminiwa kuwa ina uwezo wa kufanya hiyo kazi kwa usahihi zaidi. lakini kuna ushahidi(uniwie radhi sina rejea hapa nilipo mkuu) ya kuwa carbon 14 ina matatizo yake lukuki ambayo yanaweza sababisha ikatoa makadirio potofu! na ndio maana kuna baadhi ya wataalamu duniani wanasita kuitumia mara nyingine ktk kazi zao.
Ukichukulia kuwa sisi Waafrika tulizaliwa na mtu mmoja utapata shida sana kuelewa hypothesis yangu.
Nilishasema baada ya wanadamu wa kwanza kutoka Afrika, vizazi vyoo vya baadaye vilianza kurudi barani Afrika na ndiyo hao Waafrika ya Kaskazini kuanza Tanzania (Wairaq na Wagorowa) hadi Kenya, Ethiopia, Somalia, Djibouti na Eritrea.
Kukimbilia tu kusema ni waafrika siyo tatizo bali ni je wana nasaba gani iliyotawala kwao? Ni ya kizungu ama kiafrika?