Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Utofauti wa wanadamu kubadilika kutoka kuwa weusi kisura na kuwa weupe ulianza baada ya uhamaji wa awali kutoka Afrika miaka 400,000 iliyopita na wa pili kati ya miaka 100,000 - 60,000, kipindi ambacho binadamu weusi walihamia Mabara mengine kupitia eneo la Mlango Bahari wa Bab al Mandab nchini Djibouti lililokuwa limeungana na Arabia. Hiyo ni kwa kuwa nje ya Afrika, eneo kubwa lina baridi.
Mabadiliko ya kiakili yalitokea baadaye hasa miaka ya 10000 BC baada ya vizazi na vizazi kuishi katika maeneo hayo ya nje ya Afrika hasa Fertile Crescent (Levant) na kwenye mito mikubwa ya eneo hilo ipitayo majangwani, kama Bonde la Mto Naili (Egypt) na Euphrates na Tigris (Iraq), yakiwa na sifa kuu zifuatazo:
- Uwepo wa maji ya kutosha kutokana na mito mikubwa.
- Uwepo wa udongo wenye rutuba (alluvial) na rahisi kulimika (kwa miti) kwenye kingo za mito.
- Uwepo wa vyanzo vya kutosha vya samaki hasa mito na maziwa.
- Uwepo wa joto la kadri kukuza mazao.
- Uwepo wa mazao yanayositawi kwa urahisi, hasa ngano.
- Kutokuwepo kwa misitu minene na hivyo kuwa rahisi kuanzisha makazi na mashamba.
- Kutokuwepo kwa magonjwa ya kitropiki, hasa malaria, yellow fever na sleeping sickness.
- Kutokuwepo kwa jua linalochoma (scorching sun), lililowezesha kutunza energy zao.
- Kutokuwepo kwa baridi kali kama iliyoko nchi za Kaskazini mwa dunia.
Jamii hizo za Mashariki ya Kati zilianza matumizi ya zana za chuma mapema kabisa ambapo ilipita miaka mingi kabla ya teknolojia hiyo kuletwa kwetu Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia Dola ya Meroe (Sudan) kutokea Misri kwenye miaka ya 400 BC. Kwa hiyo Wabantu waliohama kutoka Cameroon mwaka 1500 BC walikuwa hawajaanza kumiliki teknolojia ya chuma ila walikutana nayo njiani kupitia kwa Nilotes wanaoishi Ukanda wa Sudan (Savannah).
Hata hivyo, kwetu Afrika, kutokana na uwepo wa mvua nyingi, chakula kilikuwa kikipatikana kwa wingi na kwa urahisi na hivyo kufanya akili za binadamu wa Afrika kutojishughulisha sana kama wenzao wa nje ya Afrika ambao walikuwa katika mazingira magumu ya majangwa na baridi kali. Waafrika waliendelea kupata chakula chao kupitia uwindaji wa wanyama, kuokota matunda ya mwituni na kula mizizi. Hivyo mababu zetu hawakuchanganya akili sana kama wenzao kutokana na kutokuwa na uelewa juu ya kilimo na ufugaji. Hivyo kwa yule Mwafrika aliyekuwa na akili sana bado hakuwa na tofauti kubwa na asiye na akili kwa kuwa wote hawakujishughulisha sana na utafutaji wa chakula kama wale waliohama kutokana Afrika. Kwa wanadamu waliohama Afrika ambao walikuwa dhaifu hawakuweza kustahimili mazingira magumu na hivyo vizazi vyao vilifutika duniani na kuacha waliokuwa na nasaba bora wakistahimili mazingira hayo magumu (Refer the Theory of Survival for the Fittest).
Binadamu hao waliotoka Afrika kutokana na kuchangisha sana akili zao waligundua ufugaji wa wanyama hasa mbwa, ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku na bata, miaka kati ya 13000 - 6000 BC. Vilevile, waligundua namna ya upandaji wa mbegu kwenye mashamba yaliyotifuliwa kwa kutumia miti (kipindi kabla hawajagundua kuyeyusha metali "metallurgy") kwenye udongo laini wa mabonde ya mito. Na hawa ndio waliogundua chuma baadaye kwenye 2000 BC na hivyo kuweza kuzalisha chakula kingi zaidi na kuimarisha ulinzi dhidi ya wanyama wa mwituni na jamii nyingine maadui. Uwezo wa chakula cha ziada, ulipelekea kukua kwa shughuli za huduma na maspecialists, kama waashi, wahunzi, askari wa kudumu, viongozi wa dini, na wengine wengi. Nadhani mtakumbuka ujenzi wa Mnara wa Babeli, ambao ni matokeo ya uzalishaji mkubwa chakula cha kulisha watu wengi wasiolima na hivyo walitaka kung'ang'ania eneo moja ili wasitawanyike (vyanzo vya dini ndo vinavyoripoti).
Mambo haya hayakuwezekana kamwe kwenye jamii za kiafrika kipindi hicho kutokana na kutozalisha chakula cha ziada, hivyo kila mtu alipaswa kujua karibia kazi zote (Mpaka sasa sisi Waafrika specialization bado iko nyuma kwani hata mwanachuo analazimishwa kusoma vitu vingi mno).
Teknolojia ya ufuaji wa chuma na utengenezaji wa zana za chuma ilipelekea kuongezeka kwa watu wengi Afrika Kusini mwa Jabgwa la Sahara lakini ilikuja kwa kuchelewa kutokea Mashariki ya Kati, tofauti na mabara mengine ya Old Lands (Asia na Europe).
Ili muone faida ya mapinduzi ya zana za chuma, Wabantu walitokea Cameroon kwenye miaka ya 1500 BC bila teknolojia ya chuma hadi baada ya miaka ya 400 BC. Ndiyo maana walianza kusambaa kwa wingi na kuweza kuvamia na kuzishinda jamii nyingine zote za Kusini na Mashariki ya Afrika za San na Pygmy (na hata Cushites - Mbulu, Gorowa na Mbugu) ambao ndio wakazi wa asili wa eneo hilo na ambao hawakuwa na teknolojia ya chuma. Hata hivyo, Wabantu walishindwa tu kwa Nilotes pekee (waliotokea Sudan) mfano Wajaluo kwa Tanzania.
Nawasilisha hoja.