Asili ya kudumaa kwa akili ya Mwafrika kulinganisha na Wanadamu wengine

Mleta mada soma id yangu kabla sijakukosoa mana hiyo historia yako hujatoa citation kana kwamba wewe ni mwandishi .
Ukinijibu maana ya ID yangu nitakuonyesha ulikokosea na ulikopatia.
 
Kwenye post moja, nimeposti hii kitu, naiweka hapa kwa sababu mambo ni yale yale, kwa kujazia tu vitu tunavyosoma kwenye madarasa yetu hapa Tanzania havitukomboi tuweze kufanya shughuli zetu kwa kiwango cha juu kama matarajio ya uumbaji.

The post
''

Suala sio kwamba mzungu ana akili sana suala ni kwamba wenzetu wamejitambua mapema kuliko sisi. Na nchi zetu maskini mtu akijitambua baada kutumia kujitambua kwake kusaidia wengine wajitambue, anatumia kujitambua kwake kuwa kitega uchumi na kuwanyonya wenzake.

Mungu alituumba binadamu wote na mfumo sawa wa utendaji wa akili, ukiacha wale wanaozaliwa na laana, au mapungufu ambao ni sehemu ndogo sana ya jamii.

Tunavyokua, kutokana na mazingira tunayokulia, wengine akili zao zinakua vizuri sawa sawa na matarajio wakati wa uumbaji na wengine akili zao zinadumaa.

Kipi kinaimarisha akili nakufanya kazi sawa sawa na matarajio wakati wa uumbaji. Watu wa dini wana lugha yao kwamba kuna watu waliopo gizani na wengine wapo nuruni. Lakini hii ni lugha tu ya siri, uhalisia ni kwamba kuna watu utendaji wao wa akili uko juu (nuruni) na wengine utendaji wao wa akili uko chini (gizani). Kitu kikubwa cha kwanza cha kutambua wakati unapanga kuimarisha afya ya akili na hivyo kuweza kuvumbua vitu mbalimbali na kutawala ulimwengu ni kwamba tumeumbwa na asili mbili, Roho na mwili. Kwenye asili ya roho kuna asili ya roho ya dhambi na asili ya roho takatifu.

Kinachotokea hapa watu waliopo gizani, yaani utendaji kazi wa akili upo chini, kwa kuongezea yaani wapo jehanum, asili inayofanya kazi ni ya dhambi. Hii asili haiwezi kuleta mabadiliko makubwa duniani, ni asili ya mateso ndiyo ipo nchi maskini. Kwa hiyo ukitambua uwepo wa asili takatifu ya Mungu ya kiroho ambayo ukiifikia unakuwa nuruni yaani mbinguni, ndipo hapo utakapoitafuta kwa bidii na kila mtu ana kibali cha kuifikia bure bila kulipa gharama yeyote.

Tunaifikia vipi asili takatifu ya Mungu, kwa mabudha wana mfumo wao wa kuifikia hiyo asili takatifu ya Mungu, Mimi nimempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wangu kwa hiyo njia yetu sisi wakristo ni neno la Mungu. Watu waliopo gizani hawatambui tu neno la Mungu ni dawa ya akili. Ili upone unahitaji usome neno la Mungu mara nyingi kwa siku, kwa makini, kwa kurudia rudia, taratibu huku ukiweka dhamira ya kulitii.

Neno la Mungu litasafisha moyo wako, na hivyo kufufua asili yako takatifu iliyolala. Baada ya hapo utashangaa unaweza kukaa meza moja na Trump 'ukafanya arguments' kwa sababu siri za maendeleo utakuwa nazo na unaweza kufanya maendeleo.

Ukishaiponya akili kiroho, hapo sasa utajifunza mahitaji mbalimbali ya mwili ambayo ni chakula bora, mazoezi. n.k

Kwa hiyo napinga kwamba Mzungu ana akili zaidi yetu, ila neno analoishi nalo limeboresha afya yake ya akili ukilinganisha na neno tunaloishi nalo sisi.

Ambaye hajaelewa nasisitiza, nchi maskini sehemu kubwa ya raia wake wapo gizani, yaani wapo jehanum, yaani wana ugonjwa wa akili, yaani utendaji wa akili zao upo chini na tiba ni neno la Mungu''
Hahaha..mzungu ana akili zaidi ya mwafrika ndio maana amekuletea dini yake na wewe umeiamini...Bila mzungu hata huyo Mungu wako unaemuamini usingemjua.,..hehehe niambie kabla ya kuja mzungu waafrika walikuwa na imani gani?....
 
Thanx mzee. Unasema kweli, majukumu ni mengi mpaka inakuwa ngumu kuweza kureact on time kadri hoja zinapowasilishwa na members.
 
Wasiwadanganye, vita huwa ina madhara makubwa sana kwa jamii isiyo na akili na teknolojia. We fikiria baada ya WW I, ukiacha matatizo ya kuanguka na kuweka rekodi sarafu yake ya Mark, Ujerumani iliibuka mwishoni mwa 1920 kuwa na ukuaji mkubwa wa kiuchumi kuliko nchi zilizoinyang'anya makoloni yake (Uingereza na Ufaransa). Pia kumbuka baada ya WW II, kulikuja Marshall Plan kwa nchi zote za Ulaya Magharibi lakini ilikuwa ni Ujerumani tena iliyotia fora kwa kurecover haraka na kuwa na "economic wonders" of 1950s.
Hapa Afrika mnakumbuka kulikuwepo mauajiya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, sasa angalia Rwanda iko wapi kiuchumi? Thubutu vita kutokea Tanzania, maeneo yasiyo na uwezo wa kustawisha mazao ya kudumu kama kahawa, ndizi, na chai, ndiyo yataathirika sana. Si mnakumbuka Vita ya Maji maji mwaka 1905 - 07? Ndiyo iliyoleta umasikini kwa Kiwango kikubwa mikoa ya kusini.
Kwa hiyo vita haijawahi kuathiri ukuaji akili za waafrika, kwa mfano katika Tanzania, hakuna makabila/koo zilizokuwa zikipigana kama Wachagga lakini ndio wamekuwa the considered among the brightest in the whole of Africa. Wanyarwanda na Wachagga wote wanastawisha Mazao ya kudumu kama kahawa na migomba.
Logic.
 
View attachment 586451 Ulimwengu tuishimo na vitu vyote vilivyomo umetawaliwa na binadamu. Hata hivyo kutokana na tofauti kubwa ya binadamu kuna ambao wameitawala "nature" lakini wengine bado hiyo "asili" imewatawala. Hiyo ni kwa sababu ya uwezo tofauti wa kiakili ambao wanadamu wanaonyesha. Kulingana na sayansi na historia, binadamu wa leo ni matokeo ya evolution ya muda mrefu iliyotokea miaka milioni 3 iliyopita.
Utofauti wa wanadamu kubadilika kutoka kuwa weusi kisura na kuwa weupe ulianza baada ya uhamaji wa awali kutoka Afrika miaka 400,000 iliyopita na wa pili kati ya miaka 100,000 - 60,000, kipindi ambacho binadamu weusi walihamia Mabara mengine kupitia eneo la Mlango Bahari wa Bab al Mandab nchini Djibouti lililokuwa limeungana na Arabia. Hiyo ni kwa kuwa nje ya Afrika, eneo kubwa lina baridi.
Mabadiliko ya kiakili yalitokea baadaye hasa miaka ya 10000 BC baada ya vizazi na vizazi kuishi katika maeneo hayo ya nje ya Afrika hasa Fertile Crescent (Levant) na kwenye mito mikubwa ya eneo hilo ipitayo majangwani, kama Bonde la Mto Naili (Egypt) na Euphrates na Tigris (Iraq), yakiwa na sifa kuu zifuatazo:
  • Uwepo wa maji ya kutosha kutokana na mito mikubwa.
  • Uwepo wa udongo wenye rutuba (alluvial) na rahisi kulimika (kwa miti) kwenye kingo za mito.
  • Uwepo wa vyanzo vya kutosha vya samaki hasa mito na maziwa.
  • Uwepo wa joto la kadri kukuza mazao.
  • Uwepo wa mazao yanayositawi kwa urahisi, hasa ngano.
  • Kutokuwepo kwa misitu minene na hivyo kuwa rahisi kuanzisha makazi na mashamba.
  • Kutokuwepo kwa magonjwa ya kitropiki, hasa malaria, yellow fever na sleeping sickness.
  • Kutokuwepo kwa jua linalochoma (scorching sun), lililowezesha kutunza energy zao.
  • Kutokuwepo kwa baridi kali kama iliyoko nchi za Kaskazini mwa dunia.
Sababu hizo ndizo zilisababisha jamii zilizoishi maeneo yenye Hali hizo kuanza Neolithic Revolution kati ya miaka ya 10,000 bc - 8,000 bc ambapo binadamu alianza kupanda mbegu kwa kusia ngano mashambani (maeneo laini yaliyotifuliwa kwa miti) na kuanza kufuga wanyama wakiwemo ng'ombe na mbuzi. Aidha, kutokana na wanadamu hao kufanikiwa kuzalisha chakula kwa wingi kulipelekea kuibuka kwa Civilizations za kwanza kabisa duniani katika eneo la Mesopotamia (Sumerian na Babylonia), Misri na China kuanzia miaka ya 4000 BC, kutokana na maeneo hayo kuwa na sifa hizo hasa maji ya kutosha licha ya kuwa majangwani.
Jamii hizo za Mashariki ya Kati zilianza matumizi ya zana za chuma mapema kabisa ambapo ilipita miaka mingi kabla ya teknolojia hiyo kuletwa kwetu Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia Dola ya Meroe (Sudan) kutokea Misri kwenye miaka ya 400 BC. Kwa hiyo Wabantu waliohama kutoka Cameroon mwaka 1500 BC walikuwa hawajaanza kumiliki teknolojia ya chuma ila walikutana nayo njiani kupitia kwa Nilotes wanaoishi Ukanda wa Sudan (Savannah).

Hata hivyo, kwetu Afrika, kutokana na uwepo wa mvua nyingi, chakula kilikuwa kikipatikana kwa wingi na kwa urahisi na hivyo kufanya akili za binadamu wa Afrika kutojishughulisha sana kama wenzao wa nje ya Afrika ambao walikuwa katika mazingira magumu ya majangwa na baridi kali. Waafrika waliendelea kupata chakula chao kupitia uwindaji wa wanyama, kuokota matunda ya mwituni na kula mizizi. Hivyo mababu zetu hawakuchanganya akili sana kama wenzao kutokana na kutokuwa na uelewa juu ya kilimo na ufugaji. Hivyo kwa yule Mwafrika aliyekuwa na akili sana bado hakuwa na tofauti kubwa na asiye na akili kwa kuwa wote hawakujishughulisha sana na utafutaji wa chakula kama wale waliohama kutokana Afrika. Kwa wanadamu waliohama Afrika ambao walikuwa dhaifu hawakuweza kustahimili mazingira magumu na hivyo vizazi vyao vilifutika duniani na kuacha waliokuwa na nasaba bora wakistahimili mazingira hayo magumu (Refer the Theory of Survival for the Fittest).
Binadamu hao waliotoka Afrika kutokana na kuchangisha sana akili zao waligundua ufugaji wa wanyama hasa mbwa, ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku na bata, miaka kati ya 13000 - 6000 BC. Vilevile, waligundua namna ya upandaji wa mbegu kwenye mashamba yaliyotifuliwa kwa kutumia miti (kipindi kabla hawajagundua kuyeyusha metali "metallurgy") kwenye udongo laini wa mabonde ya mito. Na hawa ndio waliogundua chuma baadaye kwenye 2000 BC na hivyo kuweza kuzalisha chakula kingi zaidi na kuimarisha ulinzi dhidi ya wanyama wa mwituni na jamii nyingine maadui. Uwezo wa chakula cha ziada, ulipelekea kukua kwa shughuli za huduma na maspecialists, kama waashi, wahunzi, askari wa kudumu, viongozi wa dini, na wengine wengi. Nadhani mtakumbuka ujenzi wa Mnara wa Babeli, ambao ni matokeo ya uzalishaji mkubwa chakula cha kulisha watu wengi wasiolima na hivyo walitaka kung'ang'ania eneo moja ili wasitawanyike (vyanzo vya dini ndo vinavyoripoti).
Mambo haya hayakuwezekana kamwe kwenye jamii za kiafrika kipindi hicho kutokana na kutozalisha chakula cha ziada, hivyo kila mtu alipaswa kujua karibia kazi zote (Mpaka sasa sisi Waafrika specialization bado iko nyuma kwani hata mwanachuo analazimishwa kusoma vitu vingi mno).

Teknolojia ya ufuaji wa chuma na utengenezaji wa zana za chuma ilipelekea kuongezeka kwa watu wengi Afrika Kusini mwa Jabgwa la Sahara lakini ilikuja kwa kuchelewa kutokea Mashariki ya Kati, tofauti na mabara mengine ya Old Lands (Asia na Europe).
Ili muone faida ya mapinduzi ya zana za chuma, Wabantu walitokea Cameroon kwenye miaka ya 1500 BC bila teknolojia ya chuma hadi baada ya miaka ya 400 BC. Ndiyo maana walianza kusambaa kwa wingi na kuweza kuvamia na kuzishinda jamii nyingine zote za Kusini na Mashariki ya Afrika za San na Pygmy (na hata Cushites - Mbulu, Gorowa na Mbugu) ambao ndio wakazi wa asili wa eneo hilo na ambao hawakuwa na teknolojia ya chuma. Hata hivyo, Wabantu walishindwa tu kwa Nilotes pekee (waliotokea Sudan) mfano Wajaluo kwa Tanzania.
Nawasilisha hoja.

Nadharia yako ni nzuri sana ILA naomba kupata mwangaza hapa; Je watu wa bara la Asia ya kusini ( Ufilipino, Malaysia, Vietnam n.k ) si wana hali ya hewa sawa na sisi ? Maana wao pia wapo kwenye ikweta (tropiki). Na je wale Maya kule Amerika ya Kati waliojenga piramid , sio hali moja na sisi ? Au Nini kilifanya hizo jamii mbili kuendelea kuliko sisi ?
 
Mlishajiuliza ni kwa nini nchi za kiafrika zilizokuwa na/zenye wazungu wa Kiingereza (SA, Zimbabwe na Kenya) ziko mbele kimaisha kulinganisha na zile zenye wazungu wengi wa mataifa mengine, mfano Wareno (Angola na Msumbiji)?

Kwa sababu hao ni mabepari namba moja ulimwenguni , Ureno (Portugal), Ugiriki n.k wanajitia ubepari ila hawajawafikia Uingereza , kwa hio hivyo vizazi vyao wanavipa mitaji (ukiacha mbali elimu) ya kuweza kuendeleza miradi / wanawawezesha. Nia bila ya matendo imekufa sawa na mtaji bila maarifa (elimu) / au maarifa bila mtaji ....
 
Ugali wa mahindi siyo asili ya Afrika, uliletwa Karne ya 16 na Wareno ni tofauti na mazao mengine yaliyoletwa tangu zamani. Wataalamu huwa wanadai ugali wa jamii za uwele ndio wenye virutubisho vingi kwa akili ukitoa ndizi katika vyakula vikuu vya Waafrika. Mihogo nayo siyo ishu.

Hata hivyo, tunachokosea sisi binadamu ni kudhani kuwa, mtoto anayepewa kila kitu tangu akiwa tumboni mwa mamaye hadi kuwa mtu mzima atakua na uhakika wa akili za darasani. Akili za darasani haziwezi kutegemea "mazingira" ya maisha ya mtu mmoja pekee bali ni nasaba "Genes" alizonazo mtu huyo zilizotokana na historia ya wazazi wake (wapi?), ukoo wake (upi?), Kabila lake (lipi?) na Race yake (Mbantu?).
Hivyo, nawaasa sana kabla sijatoa research yangu juu ya akili za makabila ya Tanzania, anza kufikiria kabila lako lilivyo kwa akili za darasani ili nikiweka hizo hypothesis mniulize na mimi nitazielezea vyema.

Kwa hio nasi tuamini kuwa *mzungu* atakuwa na akili tu hata tukijitahidi ? Au maoni yako binafsi ni yepi katika hili ?
 
Umeulizia juu ya Mji wa Timbuktu lakini nataka kutuambia kuwa, Mji ule haukuwa wa kiafrika, bali ulitawaliwa na nguvu ya jamii za Watuaregi ambao ndio waliokuwa wametawala biashara ya Trans Saharan Trade. Dola zote za Ghana, Mali, Songhai na hata Kanem Bornu, ziliweza tu kustawi as long as hazikuwasumbua wafanyabiashara hao wenye asilimia ya Hamites. Watawala wote waliotaka kuwabughudhi wafanyabiashara hao ndio waliosababisha kuporomoka kwa miji na dola zake. Nadhani unasikia kuhusu Almoravids kuiangusha Ghana na Moroccans kuiangusha Songhai.
So, Timbuktu ambayo ilistawi sana katika utawala wa kuanzia Sundiata Keita hadi Mansa Kankan Mussa karne ya 12 - 14, haukuwa mji wa kiafrika kihivyo bali ulitegemea uwezo wa jamii za kiarabu Kaskazini mwa Afrika, pamoja na Watuaregi na Waberiberi jangwani mwa Sahara.
Hata Chou kikuu ilikuwa siyo ishu ya sisi Negroid bali ilikuwa kazi yao hao Hamites ambao walileta na dini ya Kiislamu katika ukanda wa Sudanic (Savannah) States.

Tuareg ni mchanganyiko wa damu, kuna wengine ni we
Muonekano wetu wa rangi ulianza kubadilika baada ya binadamu wa zamani kutoka barani Afrika na kuingia Eurasia (Ulaya na Asia). Vyanzo vinadai binadamu wa kale aliyekuwa katika hatua ya Homo Erectus ndio walitaka Afrika miaka ipatayo 400,000 iliyopita na kugawanyika barani Ulaya (Neanderthal) na barani Asia. Baadaye binadamu wa kisasa Homo Sapiens ndio walianza kutoka Afrika kwenye miaka 100,000 - 60,000. Kutokana na kuishi maeneo ya baridi kwa muda mrefu, walianza kubadilika hadi kufikia hatua waliyonayo hao watu weupe.
Sijui kama nimekujibu ulichotaka kukijua.

Kama hilo ni la uhakika , je kule Amazon kuna wale wahindi wekundu, hawafanani nasi waafrika ? Mazingira ni 99% sawa ....
 
Nitapita huko mkuu ila nakukumbusha tu kuwa kuna member anaitwa Shana Chuma amekupa challenge katika post #182. Naomba umjibu mimi pia napenda kusikia mawazo yenu.
Sijamwelewa vyema so aliyefahamu anifafanulie anataka nijue nini na hicho kinahusiana na nini na mada hii.
Kumbuka haya nimeyatoa kama accumulated experience ya elimu niliyoipata. Siwezi kucite kila mahali ila nataka mtu anipinge kwa nilichokieleza na mimi nitafafanua kwa mifano. Kumbuka hiyo ni Theory still.
 
Nitapita huko mkuu ila nakukumbusha tu kuwa kuna member anaitwa Shana Chuma amekupa challenge katika post #182. Naomba umjibu mimi pia napenda kusikia mawazo yenu.
Sijamwelewa vyema so aliyefahamu anifafanulie anataka nijue nini na hicho kinahusiana na nini na mada hii.
Kumbuka haya nimeyatoa kama accumulated experience ya elimu niliyoipata. Siwezi kucite kila mahali ila nataka mtu anipinge kwa nilichokieleza na mimi nitafafanua kwa mifano. Kumbuka hiyo ni Theory still.
 
Nadharia yako ni nzuri sana ILA naomba kupata mwangaza hapa; Je watu wa bara la Asia ya kusini ( Ufilipino, Malaysia, Vietnam n.k ) si wana hali ya hewa sawa na sisi ? Maana wao pia wapo kwenye ikweta (tropiki). Na je wale Maya kule Amerika ya Kati waliojenga piramid , sio hali moja na sisi ? Au Nini kilifanya hizo jamii mbili kuendelea kuliko sisi ?
Hao sio Waafrika, ni jamii ya Homo Sapiens (kutoka Afrika) waliozaliana na Denisovars (Homo Erectus waliohama Afrika zaidi ya miaka milioni 1 iliyopita). So, watu weupe (Wazungu, Waasia na Waamerika) ni mchanganyiko wa aina mbalimbali za watu tofauti na sisi WaAfrika ambao ni matokeo ya Homo Sapiens Evolution kutoka Afrika Mashariki na kusambaa West hadi South Afrika.
Tunapoongelea Wazungu na Waasia, pamoja na Waarabu, msisahau kufikiria juu ya Anunnaki.

Vilevile, kumbukeni kuwa, kilicho- na kinachotutesa sana Waafrika ni magonjwa hasa Malaria, trypanosomiasis, na yellow fever. Haya magonjwa yamekuwa na effect kubwa sana kwa akili ya Mwafrika. Kwa wenzetu, hawana magonjwa haya, isipokuwa tu South America ambako kumekuwepo Yellow Fever. Vilevile, baadhi ya maeneo ya India yana malaria lakini siyo kali kama malaria ya Afrika.
 
Nadharia yako ni nzuri sana ILA naomba kupata mwangaza hapa; Je watu wa bara la Asia ya kusini ( Ufilipino, Malaysia, Vietnam n.k ) si wana hali ya hewa sawa na sisi ? Maana wao pia wapo kwenye ikweta (tropiki). Na je wale Maya kule Amerika ya Kati waliojenga piramid , sio hali moja na sisi ? Au Nini kilifanya hizo jamii mbili kuendelea kuliko sisi ?
Wale Maya waliojenga mapiramid mpaka sasa imekuwa myth juu ya wapi walitoa uwezo huo. But hiyo ni mwendelezo wa myth zinazohusisha pia uwezo wa Wamisri kwenye mapiramidi pamoja na Uwezo wa Sumerians. Pliz recall the Anunnaki.
 
Kwa sababu hao ni mabepari namba moja ulimwenguni , Ureno (Portugal), Ugiriki n.k wanajitia ubepari ila hawajawafikia Uingereza , kwa hio hivyo vizazi vyao wanavipa mitaji (ukiacha mbali elimu) ya kuweza kuendeleza miradi / wanawawezesha. Nia bila ya matendo imekufa sawa na mtaji bila maarifa (elimu) / au maarifa bila mtaji ....
Unazifahamu vyema Nchi za Iberian Pensinsula (Spain & Portugal) kweli? Fuatilia kwenye Karne ya 15 - 17, wapi kati ya Iberia vs Western Europe (Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji na Uholanzi) walikuwa foremost katika Capitalism (Mercantile Capitalism).
 
Kwa hio nasi tuamini kuwa *mzungu* atakuwa na akili tu hata tukijitahidi ? Au maoni yako binafsi ni yepi katika hili ?
No, kadri muda unavyoendelea, vikwazo vya akili kwa Mwafrika vimezidi kuwa vinapungua sana, hasa Magonjwa, hivyo as time goes on, itafikia uwezo wa Waafrika nao ukiwa juu na hata kuweza kuwapita Wazungu. But am doubt hilo suala haliwezi kutokea kwenye Karne hii ya 21 probably after 2100.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom