Asili ya baa za maziwa

Hemedy Jr Junior

JF-Expert Member
Feb 17, 2023
908
1,064
_230219_153246_920.jpg

Biashara ya kwanza ya baa ya maziwa ilianzishwa na Muingereza huko India mwaka 1930, James Meadow Charles alipofungua baa yake huko Bangalore iliyoitwa Lake View Bar. Wazo hilo likaanza kusambaa kwa kasi katika maeneo mbalimbali duniani, ikiwemo Uingereza. Katika muda mfupi tu zaidi ya baa 1000 zilifunguliwa mpaka kufikia mwaka 1936. Nchini Marekani baa hizo zilianza kushika kasi mwishoni mwa mwaka 1940

Awali baa za maziwa zilikuwa maalumu kwa ajili ya kuuuzia magazeti na vyakula vya harakaharaka kama chipsi, samaki, vitafunwa. Lakini uwepo wa maziwa mengi na mahitaji makubwa ya maziwa, mabaa mengi ya maziwa yakatumika sawia na lengo lake la kuuza kwa wingi maziwa.

Nchi zenye baa nyingi za maziwa duniani




Ikiwa 70% ya wanyarwanda wanajishughulisha na kilimo, kuwa na ng’ombe Rwanda ni ishara au alama ya mtu anyejiweza na mwenye hadhi hasa katika maeneo ya vijijini. Baadhi ya baa za maziwa Rwanda zinauzwa pia na vitafunwa ama chakula cha kuvutia kikienda na maziwa.

Warwanda walianza kuuza maziwa mwanzoni mwa miaka 1990 wakati huo ikitawaliwa na wajerumani. Wakati huo walikuwa wakisafiri umbali mrefu kwenda kujenga barabara, shule na makanisa kama sehemu ya German East Africa. Walishuhudia wenzao wa Sudan, Uganda, na Tanzania waliokuwa wanasafiri na wajerumani wakiuza maziwa waliyoyanunua kwa wenyeji na kuwauzia wafanyakazi.

Hapo ndipo walipoanza kuuziana wao kwa wao, na biashara ikaanza kukua kwa kazi na sasa maziwa ni moja ya vinjwaji pendwa Rwanda na vyenye heshima. Katika maeneo mengi kumefunguliwa baa za maziwa, zinazouza maziwa ya kawaida, yanayouzwa ya moto ama ya baridi, chai ya maziwa, mtindi, siagi na bidhaa zingine za maziwa.

Nchi zingine ambazo baa za maziwa zimeanza kushamiri ni pamoja na New Zealand wanaotumia jina ‘dairy shop’, Poland wao baa zao za maziwa wanaziita ‘bar mleczny’ ambazo awali zilitumika sana kuuza bidhaa zilizopewa ruzuku na serikali ambapo mwaka 2011, serikali ilianza mpango wa kuacha kutoa ruzuku, hatua iliyozodolewa na wengi wakisema, ni kuua baa za maziwa.

Mataifa kama Marekani, Australia na Afrika Kusini kumekuwa na baa za nyingi za maziwa.

Usikose kunifuatilia YouTube @Mwaro Tv na mimi ni Hemedyjrjunior 🙏
 
Back
Top Bottom